Jiwe La Nyoka Na Utapeli Mwengineo

Doctor Decima

New Member
Sep 11, 2019
2
0
Kiufupi, Mawe ya nyoka au Jiwe la sumu ya nyoka au Jiwe jeusi, hayafanyi kazi hata kidogo, hasa tukiongelea kuondoa sumu kwenye eneo la mwili lililong’atwa na nyoka.

Dunia ina vituko vingi mno, na mara nyingi vituko hivi huweza kwenda miaka mingi, kizazi baada ya kizazi pasipo kujulikana na wengi kutojiuliza nini hasa kinachotokea. Vituko hivi vinaweza visiwe na madhara, lakini pale mtu anapojitungia “tiba” fulani haswa kwenye maswala ya dharura, ni wajibu wetu kama madaktari kujaribu kufumbua macho.

nyoka-akingata.jpg



Kuanzia kumkojolea mtu ili kuzuia degedege, kumwagia maji aliyezimia n.k na vitimbi vyengine nilivyosikia wagonjwa wakifanya toka nasomea udaktari mpaka leo hii, hebu tuangaze kuhusu haya “mawe yanayonyonya sumu ya nyoka” na kujua yanafanyaje kazi ili kuelewa kwa nini watu wengi (mpaka wenye elimu za juu) wanayaamini.

Nimechagua kuandika kuhusu hili kwa sababu mahala ninapoishi kunajulikana kuwa na nyoka wengi sana hivyo kila nyumba na familia huwa na mbinu walizojiwekea kukwepa nyoka hawa (ya kwangu ni kutotoka nje bila sababu za msingi).

Jinsi hesabu zinavyofanya kazi

Kati ya jamii ya nyoka zaidi ya 3000 duniani, karibu nyoka 600 tu wana sumu, na kati ya hao, ni chini ya nyoka mia mbili tu wana sumu inayoweza kuhatarisha maisha yako.

Kutokana na nyoka wengi walio na sumu na wasio na sumu kufanana, na watu wengi kuwa na elimu ndogo kuhusu nyoka (au kutojua kabisa) ni sawa kimahesabu kusema kuwa mawe haya hutumika zaidi kwa nyoka wasiokuwa na sumu kutokana na wingi wa nyoka hao.

Zaidi ya hapo hata nyoka waliokuwa na sumu hawatoi sumu muda wote wanapogonga (dry bites), inakadiriwa zaidi ya asilimia 20 ya majeraha ya nyoka ni nyoka kujilinda ambapo sumu haitolewi.

Endelea kusoma zaidi hapa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom