Jivunie kuwa mwanaume

Itovanilo

JF-Expert Member
Jul 30, 2018
2,314
5,137
Habari wana JamiiForums wote, natumai mu wazima wa afya na kwa wenye matatizo poleni shida kaumbiwa binadamu.

Kama kichwa kinavyojieleza nachukua nafasi hii kumuelezea MWANAUME japo kwa kifupi.

Ni Jambo la kujivunia mtu kuwa mwanaume, kiumbe wa pekee kabisa kuanzia binadamu, mnyama n.k.

Inafahamika duniani kote mwanaume ndiyo kichwa cha familia hata kama mwanamke ana kipato zaidi.

Pia hata kwenye familia duni kiuchumi, kielimu wanaume ndio watafutaji wafanyao kazi zote ngumu ili kuhudumia familia zao

Pia hata kwenye maombi ya nafasi fulani iwe, mkopo au ajira bado mwanaume hutumia nguvu kidogo rushwa n.k.

Huyu ni mwanaume aliyepewa koromeo, mwenye uvumilivu na busara nyingi kifuani mwake.

Ndio maana wakati mwingine, ukashindwa kuonesha ukomavu kwenye Jambo flani, unaambiwa "unakuwa kama mwanamke"

Kwasababu ni rahisi mwanamke kutamani kuwa mwanaume ila siyo man kutamani jinsia ya kike, na kama wapo labda wale wenzetu wa ajabu ajabu.

Jitahidi kuwa care pindi ufanyapo kazi na mwanamke iwe ofisini, vibaruani na popote pale maana unaweza kuwekeza nguvu na akili kwao ukaja shtuka mtu anaapishwa bungeni(joke's)

Wanaume tuna majukumu mengi hadi MUNGU katupunguzia majukumu, maana kuwahi kufika kileleni ni moja kupungua kwa mambo Ili ufanye kazi zingine.

Hivyo basi,punguzeni kutumia nguvu kubwa kuhangaika,kutaka kumridhisha mwanamke badala yake tafuta pesa tu,watakuja wenyewe.

Mwanamme pambana lete kitu nyumbani, upendo, amani, utulivu havitoshi Kama hutajituma kuhakikisha, unaimudu familia

Mwanamme siyo unamuona mfanyakazi mwenzio ana miliki Subaru, na wewe unataka kufanya hivo, hapana

Fanya kitu ambacho kitamnufaisha kila mmoja kwenye familia.

Jikite kuwatengenezea future nzuri watoto wako ikiwa ni pamoja na kuwapeleka shule Bora na si Ili mradi,

Vitu unavyomiliki visadifu kipato chako (hii kwa vijana walio wengi) kutumia simu ya Bei Hali wakati kazi yako unalinda godauni la korosho.

Nimalizie kuwatakia mafanikio mema vidume, wanaume wore wanaovuja jasho la halali ili kutimiza ndoto zao.

Special for men
 
Sasa hilo la kuwahi kufika kileleni unadhani ni jambo zuri sana? Mi naona litashusha heshima, kwani nasema uongo?
 
Wanawake jivuneni kuwe wanawake kwa sababu..

Kwanza nyie ndio mnaijaza dunia,bila nyie kuzaa hata hawa wanaume wasingekuepo.

Pili wanawake hamnna stress kwamba huyu mtoto wangu au sio wanguu,siku zote mwanamke habambikiwi mimbaa ikikaa ndo yake hiyoo,hii inafanya wanawake wawe na amani sana kwamba huyu ni mtoto wao kweli.

Tatu wanawake nyie sio watu wa kuhangaika kutafuta(na pia mtoa mada anasapoti)nyie mnatulia vyakula viletwe mle mvae mlale vizuri,lau hili lingetekelezwa mngefaidi utamu wa dunia.

Wanawake ndio viumbe pekee wanaoweza kufanya mambo yote anayoweza mwanaume lakini wanaume ndio kiumbe pekee asiyeweza kufanya baadhi ya mambo anayofanya mwanamke.
 
Uzi ndani ya uzi
 
Back
Top Bottom