Jiuzulu Ngeleja kazi imekushinda, acha usanii! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiuzulu Ngeleja kazi imekushinda, acha usanii!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Nov 11, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading, width: 100%"]Ngeleja atuhumu vigogo Tanesco kukwamisha wawekezaji umeme [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"] Friday, 11 November 2011 09:16 [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  Burhani Yakub,Tanga
  Mwananchi

  WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja amesema Shirika la Ugavi wa Umeme nchini (Tanesco) limekuwa kikwazo cha jitihada za Serikali za kumaliza tatizo la umeme nchini kwa kuwa baadhi ya viongozi wake waandamizi wanawakwamisha wawekezaji.

  Ngeleja alitoa shutuma hizo jana katika hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano wa 42 wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Tanesco, iliyosomwa kwa niaba yake na Mwenyekiti wa Bodi ya Tanesco, Generali Mstaafu, Robert Mboma.

  Alisema wizara yake imepokea malalamiko kutoka kwa baadhi ya waendelezaji na wawekezaji kutoka nje, ambao wameonyesha nia ya kusaidia kutatua tatizo la nishati hiyo wakitoa malalamiko yanayoelekezwa kwa baadhi ya viongozi waandamizi wa Tanesco.

  “Viongozi waandamizi wa Tanesco wanalalamikiwa kuwakatisha tamaa wawekezaji, pia hawajali muda wala hawatoi ushirikiano wa kutosha katika hatua zote za kuendeleza miradi,”alisema Ngeleja katika hotuba hiyo.

  Ngeleja alisema Serikali inapenda kuona Tanesco inachukua nafasi ya kuwa mwezeshaji badala ya kuwa kikwazo kwa wawekezaji na hivyo kuwamisha jitihada zinazofanyika kuondosha tatizo la uhaba wa nishati nchini.

  Katika hotuba hiyo, Ngeleja alisema miradi mikubwa ya ufuaji na usafirishaji umeme inayotarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha muda mfupi (2010-2013) na ile ya muda wa kati ya (2010 -1026) ipo katika hatua mbalimbali za mchakato wa maandalizi.

  Awali akimkaribisha mgeni rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco,William Mhando alisema katika kukabiliana na upungufu wa umeme kwenye gridi ya Taifa, Baraza la Mawaziri liliagiza kuwa mitambo ya dharura ifungwe na ikamilike ifikapo Desemba 31 mwaka huu.

  Mhando alisema Tanesco ilifanya juhudi ya dharura na kuanzia Julai 2011 hadi Oktoba Kampuni ya Symbion imefunga mitambo ya kuzalish Megawati112 na IPTL wameongeza Megawati 80 kufikia Megawati 100 toka Megawati 20 za awali.

  Katika mchanganuo huo, Mhando alisema kampuni ya Aggreko wamefunga mtambo wa Megawti 100 ambapo hadi sasa jumla ya mitambo iliyofungwa ina uwezo wa kuzalisha Megawati 292 na kwamba hali ya mgowo wa umeme imepungua kwa kiasi kikubwa.

  Mkurugenzi huyo alisema ni matumaini ya Tanesco kuwa ifikapo Desemba 31 mwaka huu mgao utakuwa umemalizika kabisa nchini.
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. Msarendo

  Msarendo JF-Expert Member

  #2
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 9,131
  Likes Received: 3,320
  Trophy Points: 280
  Wasanii mbona ni wengi sana kwenye hii serikali ya Jk, wengine ni kawambwa, mkullo, kombani n.k
   
 3. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #3
  Nov 11, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ukiona Waziri analalamika subordinates wake wanamgeuka na kumkaidi ujue kuna tatizo. Sielewi kwanini anashindwa kuwafukuza hao vigogo wanarudisha nyuma wawekezaji unless anahofia asiwe anagusa miradi ya vigogo na wakubwa wa nchi hii. Hii nchi imejaa usanii tu!
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Nov 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,572
  Likes Received: 82,100
  Trophy Points: 280
  Mkuu huyu Ngeleja ndiye aliyestahili kufukuzwa kazi siku nyingi sana, lakini pamoja na kashfa chungu nzima ndani ya Wizara yake na ushahidi chungu nzima kwamba kazi imemshinda lakini bado anapeta tu na huku asilimia kubwa ya nchi ikiendelea kuwa gizani.
   
 5. s

  sihofu Member

  #5
  Nov 11, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwisha kwa mgao wa umeme kabisa imekua ni ahadi za kisiasa ambazo wamekua wakitoa kila siku bila kuzikamilisha,its high time administration upheaval ili taifa hili lisonge mbele
   
 6. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #6
  Nov 11, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ngeleja ni kiazi na hakuna kitakachombadilisha.
   
 7. n

  nyangasese Senior Member

  #7
  Nov 11, 2011
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  viongozi tuliowapa dhamana wanaimaliza nchi hii.Nina taarifa ndefu sana juu ya tuhuma za huyu ndugu moja ikiwa ni kutaka kudhulumu nyumba ya watoto yatima hapa jijini Mwanza kwa lengo la kuvunja ili apate parking kwa ajili ya hotel anayojenga.Nyumba tayari alikwisha ichukua kwa kupitia diwani mmoja wa ccm bila warithi kujua,lakini mahakama kuu ikarudisha hiyo nyumba kwa wamiliki.lkn yeye na wakili wake wameweka pingamizi kuzuia hiyo hotel kuvunjwa kwani amemega sehemu ya eneo lao.Hilo jengo ni ghorofa nane.nitaweka picha yake hapa jf
   
Loading...