Jiunge nami kusema hapana kwa udhalilishaji na ubaguzi anaoufanya mmliki wa clock tower café Iringa

Sijajua labda kuna utaratibu umeukiuka wakati unaingia kwa kuchukulia kuwa wewe anakufahamu ni nani katika mji wa Iringa na pengine wewe ni wakili maarufu.

Kwa kuwa wewe ni mwanasheria, unatambua kabisa kuwa tukimhukumu na kumwadhibu huyu mtu kwa kusikiliza upande mmoja pekee, yaani wewe tutakuwa hatujamtendea haki. Ni lazima asikilizwe kwanini ametenda vile.

Pia tukisema kususa biashara yake si tu kwamba tunamuumiza yeye, la hasha! Tunaumiza pia wafanyakazi na wategemezi wao kwani hawatapata mshahara. Pia tunapunguza pato la Taifa kwani huyo ni mlipa kodi.

USHAURI
Mfuate tu kwa ustaarabu na kumuuliza.... sheikh... nini nimetenda kinyume, kisha msameheane na muendeleze mahusiano kwa ustawi wa jamii, Iringa na nchi yetu.

Take care.
CC. jaji mfawidhi
Mtoa mada take this piece of advice halafu chukua maji unywe utapata kisukari bure kwa kulimbikiza hasira
 
unazidi kuyakuza, wewe ni mbaguzi, jiandae na TRA wanajua kukwepa kwako kodi, jiandae na watu wa Afya na OSHa, watumishi hapo hawajapima, hujakidhi vigezo, na siyo hayo tu, kuna mengi ya ukwepaji kodi tutaweka hadharani na manyanyaso ya wafanyakazi hawana mikataba, hawana nssf , unauza hutoi risiti, hatuta kuacha,
Hahaaaah sasa mkuu yote haya yanatoka wapi....kumbe mnayenu mengine hahaaaaah
 
Hata mimi naungana na wewe
huyu atakuwa ameleta mazoea kwenye biashara za watu sasa mwenye biashara kwa kuwa hataki makuu na mtu kamwambia tu bwana we sihitaji tena mteja kama wewe hapa...kuna wateja wengine tabia zao hazivumiliki
 
Eti vyoo havipo kila baada ya hatua mbili...kwa hiyo kuzidiwa kunatokeaga ghafla tu ndani ya sekunde???...na ukijifanya msamaria mwema kwa kila anayezidiwa sehemu kama kariakoo na mzunguko kama ule utafanya usamaria wema kwa watu wangapi mwisho si choo chako cha biashara kitageuka public toilet....hekima gani unataka nitumie wakati hekima ya wewe kuomba kwanza kabda ya kuingia huna...aya umeingia bila kuomba unatoka unashindwa hata kuzuga ujifanye unanunua vimaji vidogo badala yake unajibu eti mimi nanunuaga chakula hapa...jifunze kuheshimu biashara za watu pale sio kwako kama kuna huduma unaiomba omba kwanza utapewa but si unatumia bila kuomba alafu ukiulizwa unaleta ujinga...ukitaka watu wakufanyie ustaarabu na ubinadamu kuwa kwanza mstaarabu wewe
Mambo hayako hivyo wasamaria wema kariakoo wapo wengi, nadhani una asili yaugumu wa kuelewa, maana muda wote hapa mimi nazungumzia dharula, na wewe umeng'ang'ana na mazoea haya umeshinda.
 
Mambo hayako hivyo wasamaria wema kariakoo wapo wengi, nadhani una asili yaugumu wa kuelewa, maana muda wote hapa mimi nazungumzia dharula, na wewe umeng'ang'ana na mazoea haya umeshinda.
Msamaria mwema gani yupo kariakoo 😂 😂 😂 ....alafu swala la wasamaria wema linatoka wapi wakati kuna vyoo vya kulipia...unaongelea dharura za haja...wewe haja zako huwa zinakubana ndani ya sekunde....alafu huyo mtoa mada kwenye hiyo restaurant anayosema pembeni kidogo tu kuna vyoo vya kulipia hakuviona akataka kwenda kuleta mazoea kwenye biashara za watu
 
Mwanasheria akikwambia summary ni kurasa kumi, akikwambia anaandika kwa kirefu ni kurasa 100 kuendelea.
asante sana kwa kufupisha, hapo imefupishwa sana .

naomba upige kura hapo juu, tupinge ubaguzi alioanzisha nyerere na mandela
Wewe utakuwa ulienda kukazia swaumu!
 
Umeandika/Umecopy Mkeka mrefu sanaa
Jinsi wabongo walivyo wavivu,watakuwa Wamesoma na ilipofika Juu juu Waka scroll.

In summary

Hilo bandiko Linahusu Ubaguzi (kwa mujibu Wake)
Muandishi Ni mwanasheria/wakili
anaishi Iringa.
Ni mteja mzuri sana wa Mgahawa uliopo Clock Tower Iringa dodoma road.
Akiwa katika harakati Zake za Kuweka mkono kinywaji,alibanwa na haja Sasa kwa Kuwa Ni mteja wa pale na Ni mwez mtukufuku (ramadhani) akaon ngoja nikaji sitili pale (kujisaidia japo hajasema Kama ilikuwa kubwa au ndogo haha yamkini Kubwa).

wakati kashamaliza kuji hajabisha,ghafla mhudumu akamuambia Kuwa "Yeye c Mteja mzuri na anatakiwa asikanyage Tena pale"

na hiyo ndiyo hoja yake Kuwa. aliambiwa asikanyage Tena hapo.bila sababu ya Maana.
so akaona Kuwa ame baguliwa (C unajua Wanasheria tena?!).

Kupitia Ubaguzi wake akatumia ref za wakati wa ukoloni jinsi watu walivyokuwa wanabaguliwa katika nchi yao.

Ni Hayo TU.
 
Sijajua labda kuna utaratibu umeukiuka wakati unaingia kwa kuchukulia kuwa wewe anakufahamu ni nani katika mji wa Iringa na pengine wewe ni wakili maarufu.

Kwa kuwa wewe ni mwanasheria, unatambua kabisa kuwa tukimhukumu na kumwadhibu huyu mtu kwa kusikiliza upande mmoja pekee, yaani wewe tutakuwa hatujamtendea haki. Ni lazima asikilizwe kwanini ametenda vile.

Pia tukisema kususa biashara yake si tu kwamba tunamuumiza yeye, la hasha! Tunaumiza pia wafanyakazi na wategemezi wao kwani hawatapata mshahara. Pia tunapunguza pato la Taifa kwani huyo ni mlipa kodi.

USHAURI
Mfuate tu kwa ustaarabu na kumuuliza.... sheikh... nini nimetenda kinyume, kisha msameheane na muendeleze mahusiano kwa ustawi wa jamii, Iringa na nchi yetu.

Take care.
CC. jaji mfawidhi
Huyu mleta mada huenda kuna kitu kaficha.Miaka yote hiyo asibaguliwe kwanini iwe Leo?

Sent from my Fero L100 using JamiiForums mobile app
 
Mwanasheria Mkubwa huna choo ofisini kwako?
Mie nafikiri ni ugomvi wenu binafsi.
 
Pengine ndugu yetu wakili msomi angetuhabarisha kama tangazo lililobandikwa ndani ya mghahawa anaosema lisemalo''management reserves the right to refuse admission" liko kisheria au la kama jibu ni ndiyo basi awe mpole na kutii agizo.
 
Back
Top Bottom