Masanjaone
JF-Expert Member
- Nov 15, 2019
- 844
- 596
Wewe km hutaki acha wale tuliotayari kuchangia tuchange! Chadema tuliwachangia mbona? Mi nitachanga.Wakuu kuna vichekesho vinafanywa na hii serikali ya wanyonge,eti inawataka wananchi wachange pesa ili kupambana na virus vya Corona
Binafsi nimeshaangaa sana baada ya kuona bango la kuwataka raia wachangie pesa ili khali wagonjwa tangu tupatiwe taarifa kuwa kuna wagonjwa 11 Tanzania bara na watatu visiwani,sasa ni wiki tatu kwa Tanzania bara hatujapewa updates zozote,kwa akili nyepesi serikali imeshaudhibiti huu ugonjwa maana hadi sasa ni wiki tatu hakuna kesi mpya ya maambukizi sasa hizo pesa wanazochangisha raia ni za kazi gani wakati serikali imeshadhibiti huu ugonjwa.
Na kama serikali inaficha taarifa za maambukizi je ni kwa faida ya nani ili khali anayeumia ni Raia wa chini
Mwisho sioni haja ya wananchi kuchangishwa pesa ikhali wagonjwa tulio nao ni 13 na hawaongezeki kwa dhana hii inaonesha tayari serikali imeshadhibiti huu ugonjwa sasa pesa za nini tena ,chukulia mfano afrika kusini ina maambukizi 1000+ mbona hatujaona wananchi wakichangishwa pesa, serikali acheni upuuzi tupeni taarifa sahihi za maambukizi ya huu ugonjwa kwa manufaa mapana ya taifa ,tofauti na hilo hauna haja kwa raia kuchangia pesa zao
Sent using Jamii Forums mobile app