Jiulize hili.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jiulize hili..

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtama, Nov 12, 2010.

 1. M

  Mtama Member

  #1
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi umewahi kujiuliza hasa maisha ni kitu gani?Au unaenda enda tu?Je maisha ni kusoma,kuoa/kuolewa,kupata watoto kuzeka kisha kufa??Au kuna kitu kingine kinatakiwa kufanywa ili kukamilisha kitu kinachoitwa maisha,mi naamini Mungu hajatuumba tuje kusoma,ndoa,watoto kisha kuzeeka na kufa,kuna kitu kingine zaidi tuwe tunajua au hatujui,wewe wasemaje?
   
 2. M

  Mgalatia JF-Expert Member

  #2
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 28, 2007
  Messages: 297
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Mungu ametuumba binadamu kwa sababu ametupenda na amependa kutushirikisha upendo wake ili tumjue, tumpende, tumtumikie na mwisho wa maisha haya turudi kwake mbinguni.
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Nov 12, 2010
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Maisha ni historia yako yote , ulipo kuwa jana , ulipo leo na utakapokuwa kesho yote ni maisha. Usije jidanganya eti sijaanza maisha .maisha ya kiumbe chochote huanzia kinapoumbwa hadi kufa..
   
 4. chiko

  chiko JF-Expert Member

  #4
  Nov 12, 2010
  Joined: Feb 24, 2010
  Messages: 465
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Maisha ni GAME, baada ya game, Kuna kuulizwa ulichezaje!!!, mbona kucheza RAFU, mbona kacheza ***** *****, yoooote hayo uwe tayari kumjibu Maanani.
   
 5. D

  DR. Mlay Member

  #5
  Nov 12, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Ebwana kweli MUNGU si mwadamu hata atuumbe bila sababu. Sababu ni moja tu ametuumba ilikuitenda na kuifuata kweli yake katika maisha yetu. Ila jaribu kutafakari maana hii ya maisha: MAISHA NI MTIRIRIKO WA SHIDA NA MATATIZO MENGI NA CHECHEMBE KIDOGO ZA BURUDANI.:smile-big:
   
 6. Lasikoki

  Lasikoki JF-Expert Member

  #6
  Nov 12, 2010
  Joined: Jan 10, 2010
  Messages: 642
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  maisha ni kuishi and that's it...........let's not fear what we don't know or have prove of it.........:hippie:
   
 7. St. Paka Mweusi

  St. Paka Mweusi JF-Expert Member

  #7
  Nov 13, 2010
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 5,900
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145

  Swali lako ni zuri sana kama mtu atakaa chini na kujiuliza, maana binadamu pamoja na ugunduzi wake wa vitu vyote uvionavyo leo hii bado hajatumia hata robo ya uwezo wa akili yake katika kufikiri.Wengi wetu hata tuwe tumesoma kiasi gani tunakuwa tunafuata yale yaliyokwishafanywa na watu wengine ni kama vile tunakariri.Ni bora mwanadamu akakaa chini na kutafakari nini maana ya maisha na jinsi ya kuyaendeleza.
   
 8. Mdau Mkuu

  Mdau Mkuu JF-Expert Member

  #8
  Nov 13, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 236
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Ukiyafikiria hayo yote utakufa muda c wako bana
   
 9. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #9
  Nov 13, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  kweli sijui maisha ni nini mimi naishi tu ...... kwangu mimi maisha ni mafumbo.... leo nafumbua kesho ni siku nyingine....
   
 10. H

  Hemed Maronda Senior Member

  #10
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mungu hawezi kufanya kitu pasipo sababu kama tunafutata maelekezo katika Vitabu vyake Vitakatifu basi sababu kubwa ya sisi kuumbwa ni KUMUABUDU YEYE TU,kutokana na mapenzi makubwa ya Mungu kwa watu wake akaamua kutufanyia wepesi kwa kila jambo tufanyalo hivyo maisha ni KUABUDU MUNGU.
   
 11. F

  Ferds JF-Expert Member

  #11
  Nov 13, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 1,267
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  :bowl::tape::doh::nono::smile-big:[​IMG]:hippie::yield:
   
Loading...