Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Ni afadhali CCM wameamua kukaa kimya kuhusu kujisifia kwamba wameleta maendeleo nchini sijui wamenunua Dreamliner mbili, wamejenga flyover Tazara na nyingine Ubngo kwa hiyo wameleta maendeleo Tanzania, na hiyo iwe sababu ya kuwachagua tena. Maendeleo kwa ajili ya nani? Bibi yangu kule kwetu Kishimundu?
Inakuwaje CCM wanashindwa kuwa na macho ya kuona kwamba karibu kila mwezi hapa nchini Wa-Ethiopia wanakamatwa kwenye malori wakisafirishwa kimagendo kwenda Afrika Kusini, na wengine kufia ndani ya malori hayo na maiti zao kutupwa porini?
Kama kuwa na SGR, floover, Dreamliner sijui ni maendeleo, kwa nini Wa-Ethiopia kwa maelefu wanazikimbia Dreamliner zao 25, Boeing 777 zaidi ya 16, Airbus 350-900 mpya 14, SGR, flyovers kila mahali, l na kuzamia Afrika Kusini?
Iweje Tanzania tunakuwa wepesi wa kusema tunamuenzi Nyerere huku tunasahau maneno yake kwamba maendeleo sio kuwa na majengo au barabara za ghorofa au ndege? Kwa nini tunasahau Nyerere alikataa kwa miaka mingi Tanzania kuwa na Television akisema kuna mambo muhimu ya kufanya kwanza?
Tafadhali niambieni bibi yangu kule Kishimundu atafaidika vipi na Mfugale flyover hapa Dar es Salaam, au daraja la juu ya bahari, na hapo mtakuwa mmenishawishi kwamba Tanzania tumeendelea sana katika kipindi cha miaka mitano iliyopita!