Jitihada za JK ni "SIFULI" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jitihada za JK ni "SIFULI"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ngoshwe, Jun 9, 2010.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Haya ni baadhi tu ya orodha ya majaribio ambayo binafsi nayaona yanaweza kumfanya JK akose raha hata kama atakuwa bado ana kiburi cha kuendelea na awamu nyingine ya Uongozi.
  1. Mikopo kwa wajasiliamali kupitia mabilioni ya JK = 0
  2. Kupunguza ukubwa wa Serikali kwa kuunganisha Wizara na Idara ili kuleta ufanisi = 0
  3. Kufanya Kilimo chetu kiwe endelevu kupitia umwagiliaji = 0
  4. Kutoa ruzuku ya pembejeo ili kuboresha kilimo = 0
  5. Kumleta Maximo kwa gharama kubwa ili kuinua soka la Bongo = 0
  6. Kuileta Real Madrid = 0
  7. Kushawishi watanzania waliopo ughaibuni kurejea ili wawekeze nyumbani = 0
  8. Kuwasaidia wachimbaji wadogo wa madini = 0
  9. Kuweka mfumo mzuri wa wazawa kunufaika kutokana madini yetu sawa na wawekezaji = 0
  10. Kuileta Brazil ili kutangaza Tanzannia ikiwemo utalii wetu pia kupata kafaida kidogo = 0
  11. kuitangaza Tz kwa safari zake kibao za nje ya nchi hasa USA= 0
  12. Kuleta mkutano wa kimataifa wa Lionel Sullivan hapa Bongo ili kutangaza wajasiliamali wetu = 0
  13. Kuanzisha vituo vya kukodisha matrekta na kuleta matrekta = 0
  14. Kujenga madarasa =0
  15. Kujenga zahanati = 0
  16. Kuongeza ajira za waalimu na kuboresha maslahi yao = 0
  17. Kuongeza mishahara ya watumishi wa umma =0
  18. Kupunguza matukio ya uhalifu = 0
  19. Kuwachukulia hatua wote watakaojisisha na ufisadi = 1x 0
  20. Kupunguza kero za foleni = 0
  21. Kupunguza ajali za barabarani = 0
  22. Kupunuza foleni kwa utaratibu wa njia tatu = 0
  23. Kupunguza utegemezi wa wahisani kwenye bajeti ya Serikali = 0
  24. kupunguza mfumuko wa bei = 0.
  Angalau amefanikiwa katika haya:
  1. Kuongeza idadi ya akina wanawake katika sekta ya uongozi na utawala
  2. Kuinua vipaji vya wasanii ikiwemo kuwahusiha katika masuala mbalimbali ya kitaifa kama mradi wa maralia, changia CCM ns kula nao pilau IKULU.
  3. Mpango wa walimu wa "voda fasta" ambao wengi walifeli ili watumike kuwafundisha wanafuzin kwenye shule za kata..
  4. Kuwa karibu na wananchi kwenye hitima, misiba na majanga mengine ya kitaifa kwa kuwatembelea kwenye mapagale yao wanayoishi..
  5. Kuwasaidia vijana kuingia na kujijenga kwenye ulingo wa kisiasa ikiwemo Kijana wake Ridhiwani, Shy- Rose, Nape, Januari Makamba, nk.
  6. Kushawishi baadhi ya watanzania ughaibuni kurejea nyumbani ili kushika nafasi nyeti akiwemo Tido Mhando pale TBC nk.
   
 2. Whisper

  Whisper JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2010
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 502
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  7. Kuendelea kumbeba Sophia Simba pamoja na madudu yake
  8. Kuizunguka dunia na kukutana na macelebrities wa dunia
  9. Kutupeleka katika ulimwengu wa mbayuwayu


   
 3. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #3
  Jun 9, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  10. Amefanikiwa kuongeza mke mwingine
  11. Ameshindwa kutimiza ahadi ya kurudisha nyumba za serikali zilizouzwa kwa bei chee
  12. Ame-develop hobby mpya ya kubembea
   
 4. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #4
  Jun 9, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,468
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Nadhani anataka aweke rekodi ya kuwa kiongozi aliyeizunguka dunia yote, hapa bado miaka mingine mitano..........atafika hadi MWEZINI au sayari ya MARS!
   
 5. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  jamaa anaujasiri wa ajabu kuendelea kuwania tena nafasi hii...hali sijui itakuaje next...
   
 6. Nyange

  Nyange JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 2,180
  Likes Received: 229
  Trophy Points: 160
  Nyongeza:-
  • Amefanikiwa kupiga picha na wasanii kuhusu Malaria inakubalika Tanzania.
  • Amefanikiwa kuteua Mawaziri kibao wenye skendo ya vyeti hewa.
  • Idadi ya wanafunzi wanao maliza kidato channe imeongezeka.
  • Ameanzisha na amesaidia askari wa TIGO kupata marupurupu zaidi barabarani kwa kuwapa pikipiki na kuongezeka kwa rushwa.
  Ameshindwa:-
  • Idadi ya wanafunzi wanao shindwa mitihani imeongezeka.
  • Thamani ya fedha ya TZ inakimbizana na ya Zimbabwe.
  • Maisha bora kwa watanzaia=0
   
 7. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2010
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  ni SIFURI si SIFULI rekebisha wengine tunakereka
   
 8. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Mkuu lakini si umeelewa??
   
 9. S

  Semanao JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2010
  Joined: Jul 25, 2007
  Messages: 208
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Kwa mara ya kwanza gari la Rais kuchomoka tairi,
   
 10. bona

  bona JF-Expert Member

  #10
  Jun 10, 2010
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  1.mfumuko wa bei, vyakula bei mara 3 ya zaidi kipindi anaingia
  2. kutoanzisha chanzo cha mapato kwa serikali
  3. kutokua na priority
   
 11. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #11
  Jun 10, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,147
  Likes Received: 1,242
  Trophy Points: 280
  Ujenzi wa barabara za kwa hela za ndani = 0
   
 12. w

  wasp JF-Expert Member

  #12
  Jun 10, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bigirita naomba nitonje jina la huyo mke mwingine wa JK. Je ni wa kidhungu, kimatumbi au kiarabu? Je chemwali Salma anahabari na mke mwenza?
   
 13. p

  pareto 8020 Member

  #13
  Jun 10, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani mbona orodha zinazotolewa hapa ni negatives tu? Mbona yapo mengi mazuri amefanikisha hayatajwi.. Kabla sijaorodhesha mazuri yaliyo kwenye public domain..
  Lazima tukubali fact kwamba JK ameingia madarakani katika kipindi tofauti ambacho, uchumi wa dunia umeyumba na hivyo, fursa nyingi zilizokuwepo huko nyuma zilitoweka. Aliingia kipindi ambacho bei ya mafuta ilipanda hadi kufikia record price ya USD 147 per barrel, aliingia kipindi ambacho dunia ilikumbwa na uhaba wa chakula na kupanda kwa bei za vyakula. Ni katika kipindi chake pia ambapo mtikisiko wa uchumi duniani umeziathiri nchi zote tajiri na masikini... Hivyo, tunapo review kipindi chake, lazima kuangalia in that context ya environment....Ofcourse,kama viongozi wengine wowote katika kipidi chake kumekuwa na mapungufu pia.....lakini mapungufu hayafuti mafanikio....

  · Amefanikisha Tanzania kupata MCC grant ya USD 698 Millions ambazo zitajenga miundombinu mbalimbali ikiwa ni pamoja na barabara,maji na nishati

  · Amefanikiwa kupigania ajenda ya kupunguza vifo vya akina Mama na Watoto mpaka serikali ya Norway ime commit NOK 225 million kusaidia akina Mama na watoto

  · Amesimamia na kuwezesha kuanzishwa kwa Chuo Kikuu cha Dodoma ambacho kwa sasa kinatoa fursa za wanafunzi zaidi ya 5000 na miaka michache ijayo kitafikisha enrollment ya 20,000

  · Ameweza kutatua kero ya vivuko kwa kufanikisha pantoni mpya katika visiwa vya ukerewe, pamoja na pantoni ya kigamboni

  · Ameweza kuishawishi serikali ya China kufinance National ICT broadband infrastructure Backbone Network Project (Phase II), yenye thamani ya USD 100 M

  · Kufuatia ziara yake China, ameweza kufanikisha Serikali ya China kuisaidia Tanzania kujenga taasisi ya kisasa ya mafunzo ya tiba za Moyo; amepata commitment ya serikali ya China kuanzisha benki ya Kilimo yenye mtaji wa USD 100M

  · Kufuatia ziara yake Japan, amepata commitment ya Japan kufinance revamping ya Port ya Mtwara ambayo itagharimu USD 100. Aidha ameivutia kampuni ya kijapani kuwekeza katika kilimo kikubwa cha miti kwa ajili ya soko la karatasi

  · Kufuatia ziara yake ya Korea, Serikali ya huko inajenga new campus ya Chuo Kikuu cha Muhimbili kule Kwembe, na pia inajenga vyuo 8 vya VETA nchini

  Haya ni machache tu ambayo yanapatikana kwenye mtandao…..bado mengine mengi tu ambayo hatuyajui…
   
 14. M

  Msharika JF-Expert Member

  #14
  Jun 13, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 936
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mafanikio mengine ni;
  1. kafanikiwa kuwaeleza wanafunzi kuwa mimba ni kimbelembele chao na watulie.
  2. Kujenga four ways chalinze segera, ambayo haina priority kwenye kupunguza msongamano wa dar.
   
 15. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2010
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Japokuwa hizo jitihada zinasemekana ni sifuri ila atachaguliwa tena kuwa Rais,nahisi na wananchi pia ni sifuri mana tutamchagua tu hata kama siyo kuchaguliwa na mimi au wewe unayesoma post hii.. hivyo 0+0=0, funny country!!
   
 16. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  hii kali..hata ingekuwa 0x0 = ( ).

  TANZANIA YETU JAMANI
  1. TAZAMA RAMANI UTAONA NCHI NZURI..YENYE MITO NA MABONDE MENGI YA FANAKA..
  2. NCHI YANGU TANZANIA, JINA LAKO NI TAMU SANA, NI LALAPO NAKUOTA WEWE, NI AMKAPO NI HERI MAMA EEH...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. A

  Akili Kichwani JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 1,504
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  kupimwa akili kuona kama ziko sawa =100%
  kutoa majibu ya vipimo vya akili kabla hajaamua tena kugombea = 0%
   
 18. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 232
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 60
  Hawa CHADEMA wanaudhi na kelele zao za chura, mwazilishi wa mada anaandika sifuli badala ya sifuri halafu anasema wenzake vihiyo?

  Hamuoni ya UDOM? Hamuoni ya vyuo vikuu zaidi ya 20 wakati huko nyuma vilikuwa havizidi vitano?

  Nyie toeni kashfa tu ambazo nyingi ni kwasababu CHADEMA wamepigwa chini.
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Duh! Huku sasa ndo kumchoka muungwana. Basi angalau hili la kibinafsi lingeachwa. Isiwe taabu kwani kwetu siye waswahili kuoa tena na tena iwe rasmi au sio rasmi si suala sana; ni mtiririko wa kawaida kabisa katika maisha :wink2:
   
Loading...