Jitibu U.T.I kwa mmea huu kwa matokeo yenye ufanisi zaidi

Wakuu habari za leo ! Poleni na mihangaiko ya hapa na pale katika kutafuta riziki.

Nimekaa na kufikiri ni jinsi gani wazee wetu walikuwa wataalamu Wa tiba asilia lakini walikuwa wagumu sana kufundisha watu wakaribu yao ,matokeo yake walikufa na maarifa yao,kwa Leo Mimi sitaki kufanana na hao wahenga...
Unaitwa mzungwa
 
Huo wa super market hauna afya tuu lakini ndo huo oregano mkuu,na ukipandwa sehemu yenye rutuba majani yake huwa mapana ZAIDI.
Huwa najitahidi kununua ambayo ni organic ila sema ndo hivyo imekuzwa kwenye ma green house huko na kwingineko.
 
Huu mti unaitwa mpatakufa/mpata kuva/ oregano unatibu u.T.I, typhoid. Kwa wagonjwa wa kisukari na presha kuwa makini ktumia kwani hushusha sukari ghafla na kuipandisha presha ghafla yaani hufanya kiwango cha maradhi hayo kisiwe stable jambo ambalo ni hatari kwa wenye nayo.
Oregano ni mvuje km sijakosea. Wanatumia sana wahindi kama kiungo. Inasaidia sana kwa gesi
 
Hapana mkuu kivumbasi Ni nyingine hi ni OREGANO huwa Pana zaidi penye rutba.lakini pia OREGANO ZIPO ZA AINA 2 Ndogondogo na hi kubwa toauti nyingine Ndogondogo huwa kijani zaidi ( dark green)
Hii ni kivumbasi lakini yenye majani mapana ni tofauti na kivumbasi lenye majani madogo madogo.
 
Hii ni dawa safi sana,kwetu tunauita mkingili(ikingili) ukiacha magonjwa madogomadogo mengi ambayo mmea huu huweza kutibu kwa mafanikio makubwa nilipata jingine kwa rafiki yangu muhindi,yeye kwake ameyapanda kila sehemu kuzunguka ua wake.

Nikamuuliza kwa nini ameyaweka mengi kuliko maua mengine mazuri? Yeye akanijibu kuwa kwanza ni tiba ya magonjwa mbalimbali,lakini zaidi huwa anayatumia kiimani zaidi, anasema ukiwa na mimea hiyo nyumbani kwako basi watu wenye macho mabaya(ya husda) ambayo huleta madhara kwa watu na vitu hudhibitiwa barabara.

Anasema hata kama mchawi akija kwako kwa lengo baya basi mmea huu humfanya ashindwe kutimiza lengo lake,wachina pia wanauheshimu sana mmea huu kwa sababu kama hizo hizo, wao pia hudai kuwa mmea huu ukiupanda nyumbani huleta bahati njema, wahindi wa jamii ya ki hindu huchuma majani yake na kuyafunga pamoja na majani ya mwembe na kuyatundika mlangoni kama kinga dhidi ya wote wanaoingia ndani ya nyumba zao, hasa siku za sherehe au shughuli zinazokutanisha watu wengi,asante
hili jani ni lile Ikingi la moshi nini?
 
Back
Top Bottom