Baba Vladmir
JF-Expert Member
- Aug 31, 2021
- 248
- 381
Ni matumaini yangu kuwa wanajukwaa wenzangu hamjambo kabisa na mnaendelea na mapambano juu ya maisha yenu kama nifanyavvo mimi.Kwa wale wenye changamoto kiafya poleni sana Mungu ni mwema siku zote.
Rejea mada tajwa hapo juu;
Andaa mizizi ya mlonge kadri unavyoweza,kwa ajili ya kuelekeza napendelea uandae angalau mizizi mitatu yenye ukubwa wa kati ambayo ukikatakata inaweza kujaa angalau sifuria ya kupika kilo moja ya mchele na kuendelea.Andaa angalau nusu kilo ya tangawizi.Mchanganyo wa mwisho andaa limao/ ndimu nusu kilo.
Kata mzizi wako wa mlonge katika vipande vidogovidogo,kata limao/ndimu katika vipande vidogovidogo(kwa zile limao kubwa unaweza kukata kwa vipande vinne,kwa zile ndogo ni mara mbili tu) Twanga tangawizi yako ili iweze kupondeka vizuri.
Weka mchanganyo wote kwenye sifuria kubwa na ulijaze maji(angalau kwa mchanganyo huo sifuria yenye kutoa lita kumi).Injika mchanganyo wako kwenye jiko lako na hakikisha unachemka vizuri na kutokota(usitokoteshe kupita kiasi)
Baada ya kuchemsha ipua na subiri mchanganyo wako upoe vizuri na kisha chuja kwa ajili ya matumizi.Kwa mchanganyo huo jitahidi usipungue lita kumi.
Tumia kila siku gilasi moja asubuhi mchana na jioni,mchanganyiko huu usiutumie kwa watoto chini ya umri wa miaka sita.
Mchanganyo huu unatibu magonjwa yafuatayo:
#Matatizo yote ya mfumo wa upumuaji.
#Huondoa sumu mwilini na kusafisha kabisa damu,kuondoa lehemu kwenye mishipa ya damu,hivyo kuongeza na kurahisisha msukumo wa damu.
#Uzito kupita kiasi.
#Matatizo na maumivu ya mishipa ya damu.
#Husafisha mkojo na kibofu cha mkojo,hivyo unatibu kabisa matatizo ya UTI sugu
#Shinikizo la juu damu na magonjwa ya moyo na kisukari.
#Maumivu ya mwili wote
#Upungufu wa nguvu za kiume na huongeza maradufu hamu ya tendo la ndoa
#Tumbo kujaa gesi
#Matatizo ya tumbo na uvimbe
#Baridi yabisi
#Matatizo ya hedhi kwa wanawake na matatizo mengine mengi ambayo siwezi kuyaorodhesha hapa yote.
Unaweza kutumia mchanganyo huu kwa matumizi ya wiki mbili na kuendelea na matokeo yake utayaona.
MUNGU awabariki sana!