JITAMBUE NA UJIKUMBUKE: Unaweza lolote lile na wewe ndiye mmliki wa dunia. usipojijua hapa hutajijua tena

Lesutu

Member
Jul 8, 2017
35
150
Kiukweli Mkuu Rakims ndio aliefanya nikajiunga rasmi JF miaka kadhaa iliyopita(ID ile nimeacha nayo). Nilikuwa msomaji tu ila uzi wa "Meditation" ndio ulipoanza nikajiunga rasmi. Hongera mkuu umenisaidia vingi sana mpaka sasa kwenye matumizi sahihi ya ubongo na kiroho.
Mwenyezi Mungu akupe kila lililo na Kheri kwako Brother.
 
Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,038
2,000

Asante sana mkuu
Tupo pamoja

Rakims

Sent from my TECNO KB8 using JamiiForums mobile app
 
Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
243
500
Mtiririko wa mawazo yako ni mazuri kwa fikra nyumbulifu nikupongeze kwa hilo ila sikubaliani na fikra za mwanadamu kujikweza juu ya viumbe wenzake kuwa ni mungu wao(mtawala) eti kisa kwa akili zako wajiisi umeumbwa special kuliko wao,

Umeelezea kuusiana na maumbile ya mwanadamu ukioanisha na nyakati,maumbile ya ulimwengu na vilivyomo,upande mzuri na mbaya n.k ambavyo vyote vimepangwa/kugunduliwa au ku-originate kutokana na fikra za mwanadamu hili vitumike na mwanadamu kuweza kuyamudu mazingira yake(hili aweze kuishi yampasa kusaka maarifa)

Pointi yangu ni kuwa kama walivyo viumbe wengine(wasivyojua uwepo wao duniani na purpose) hata mwanadamu ni mjinga kwenye hilo pia
Kama wewe utamzidi bundi au paka kwa maarifa yakibinahadamu kwa kufanya/kuunda vitu kwaajili ya matumizi yako na ukahisi kuwa paka au kuku ataelewa/ku-appreciate ulichofanya ni ujinga

kwa maana kila kiumbe anaishi katika mipaka ya ufahamu wake mwenyewe na kile afanyacho nikulingana na mazingira ya uwepo wake katika ulimwengu huu hivyo wewe na mwewe mnaishi dunia mbili tofauti ndani ya dunia moja kila mmoja wenu akimjaji mwenzake juu ya uelewa wake.
Mwanadamu ni bora kwa lipi ikiwa anakufa kama viumbe wengine?
Ni kiumbe gani mwenye mwili mkubwa(umbo) aliyeumbwa dhaifu kuhimili hostility ya mazingira yake tu ikawa mtihani kama siyo binadamu?

-Kwa maana hiyo akawa na/akatumia uwezo wa kufikiri zaidi hili kuweza kusurvive kama wenzake na siyo kuwa ni bora kuliko wengine wanaoweza kuhisi zaidi,kunusa zaidi,kuona usiku, kukimbia zaidi,kulala kwenye mvua na barafu,kujitafutia au kujitengenezea chakula chao wenyewe kama miti n.k

Ni binadamu tu ndo mwenye hizo 4 Elements na viumbe wengine hawana hizo sifa,Je ni kitu gani mwanadamu anacho cha ziada kuliko hao wanyama?

Itoshe kusema tu kwamba mimi naamini kuwa kila kiumbe yupo tofauti kimaumbile na kiakili katika hali ya msawazo(balanced) inayomfanya aendane na mazingira ambayo ndo chanzo chake na uwepo wake na hiyo akili uliyonayo/au anayokuwa nayo mnyama inawatosheleza wote

na hakuna aliyezaidi ya mwingine mkivaa uhusika wa kila mmoja wenu mtajishangaa kuwa hakuna penye kasoro bali ni kipimo cha kusurvive na kila kiumbe anatafakari usiku na mchana atasurvive vipi na kile kinachotekea kama matokeo ya struggle hii ndo kinachomtofautisha binadamu na miti,wadudu au wanyama kimtizamo,

Wakati ukweli hapo ni kuwa licha ya akili tofauti(mitizamo) kulingana na uwezo waliopewa kimazingira viumbe wote hapo hakuna anayeweza kung'amua fumbo lakuishi pasipo mwenzake/dunia au kuacha kuangaikia kusurvive nakuchange/kushepu ulimwengu kuwa wanachotaka na wasife n.k hivyo wote bado wanaukomo wa maarifa na hawajapiga hatua kubwa katika ufahamu.
 
Deeplowmatt

Member
Aug 11, 2021
41
125
Yeah hili thread iko ina nyama za kutosha,hongera
JITAMBUE:
View attachment 1550261
Habari wakuu,

Natumaini nyie wote ni wazima wa afya na mnaendelea vema katika mambo yenu ya hapa na pale ambayo yanaendelea kuwatesa na kuwapumbaza katika maisha.

Leo nataka niwakumbushe ili muache kuishi katika system ambayo wengi hamzipendi lakini hamna la kufanya kwa sababu mazingira yamewalazimisha kuwa kama robots ambazo zinasubiri kuwa switched siwatukani nawaamsha hisia na fikra na kuwakumbusha nyie ni kina nani msijisahau sana na kushindwa kufanya mnayoyataka na kukamilisha mipango yenu.

ewe msomaji wangu ni kama sleeping giant who is waiting to be awakening and do what he/she has to do.

Akujaalie yule unayehisi au unayemjua kuwa ndio chanzo cha wewe kuwa existed kufikiria kwa kina na kuelewa vizuri zaidi na zaidi hiki ninachokiandika hapa:

Nimekuwa nikiandika threads mbalimbali za kiroho ambazo wengi huzichukulia kiimani zaidi lakini na hii ukiichukulia hivyo you need to wake up.

Busara na hekima zina level tofauti tofauti na level moja ya hekima hupelekea hekima nyingine nimeandika haya kwa hekima ya kupenda wewe uamke na kujikumbuka kisha utuambie pia katika mitizamo yako kwa nini wewe ndiyo mtawala wa dunia hii since the beginning of time.

Mwenye elimu pana sana watu hupokea matunda ya elimu yake na si elimu ya kusoma darasani isipokuwa elimu ya ubongo ambayo kila mtu anayo hujifunza na kuipenda elimu yake na kuifanyia uchunguzi kisha kuisambaza katika mgongo wa dunia na watu wengi wakanufaika nayo.

Na yule ambaye yupo chini kiakili huonekana kama sio mwanadamu wa kawaida,
Ingawaje anaweza kuwa binadamu lakini ndio hawa ambao leo hujiona wamezaliwa kwa bahati mbaya maana hawatambui uwepo wao kama wanadamu. ambayo hii sasa ni sehemu kubwa sana katika jamii zetu tulizomo, mwenye akili huonekana mpumbavu na mpumbavu huonekana mwenye akili!

Ukweli ni kwamba mwanadamu anakamilika kulingana na tabia kuu tatu akili,mnyama na mmea:

Ingawa mwanadamu maumbile yake kwa haraka haraka ni akili na mnyama.

Akili nikimaanisha (fikra) ambapo huunda jambo ambalo halionekani katika macho ya kawaida hulitengeneza kichwani kwake na kuunda kwa mikono yake na kukipa jina kwa kauli yake.

Pia kiumbe hai huyu(wewe) huleta katika fikra(akili) yake nchi na viumbe vingine na kuvichanganya pamoja katika ubongo wake ambavyo hutokea mchana kutwa na kuvikusanya katika usiku wake (Giza) na huweza kuubeba karibu ulimwengu mzima katika kichwa chake kwa mchana mmoja na kuanza kuuchambua usiku nae ni mwenye tabia zote za wanyama lakini katofautiana nao katika uelewa na nguvu(binadamu)

binadamu ana miondoko sita ambayo inatembea au kukimbia pamoja na mfupa wake wa nyuma kupitia mapaja yake katika mstari uliyonyooka.

Yeye alijikuta duniani kwa bahati mbaya nae ataondoka kwa bahati mbaya kwa sababu ya sheria ya kiumbe hai kuzaliwa na kufa?.
Vidole vyake na mikono yake vimegawanyika na kichwa chake ni cha duara ana kucha na anamuondoko mmoja wa kutembea; anauwezo wa kujifunza na kuandika na mvumbuzi wa sanaa nzuri; anauwezo wa kuwaiga wanyama nao hawawezi kumuiga yeye; anacheka na kububujikwa na machozi yenye huzuni na ana uwezo wa kufanya miujiza ya ujenzi na uvumbuzi wa sanaa mbalimbali ana uwezo wa kusimamia uraia.

Anatiiwa na viumbe mfano wa muumbaji kwa nje na ana nuru ndani yake; mwili wake ni mfano wa chombo ambacho ndani yake kumebebwa uumbe hai wake; kapangiliwa vizuri; anatambua kipi kitamuumiza na kipi kitamfaa; anapangilia jambo akitaka kufanya anafanya na akitaka anaacha ikiwa atataka au hatataka.

Anaweza akafanya miujiza mingi ikiwemo uchawi n.k; anafahamu mategemeo ya lile analolitaka na kuelewa kila analotaka kulifanya.

CHANZO CHAKO:

Aliyemuumba kamfanya kuwa hazina na kampendelea kuwa mbora katika alivyoviumba na baadhi ya wajinga wanadhani eti hayo yote hajayafanya aliyemuumba mwanadamu kuwa katokea tokea tu kutoka kwa sokwe na cell isiojulikana na uongo uongo mwingine;
Ameemfanya kukubali na kupokea ufunuo wake na kuuelewa vyema matawi yake mbali mbali anamuongoza na kumpa akili katika ulimwengu mpana na afanye nini na anaelekea wapi na nini majaliwa yake.

Aliyekuumba anajua kila kitu na majibu ya kila swali usiloweza kulijibu, vile alivyoviumba amekuwezesha kuvijua kila muundo wake, na amepewa uwezo mwanadamu wa kuvisanya vyote viumbe vilivyotawanyika katika dunia navyo haviwezi kumkusanya yeye,anaweza akawafanya wamtii, lakini wao hawawezi kumfanya awatii, anauwezo wa kuwaigiza sauti zao; kuchora picha zao kwa mikono yake; kuwatambua kwa ulimi wake; na anaweza kuzichambua tabia zao, hakuna mnyama anaweza kujibadili katika maumbile yake aliyoumbwa nayo na hawezi kuigiza sauti za wanyama wengine; jogoo hawezi kubadili kuwika kwake; mbwa hawezi kubadili kubweka kwake; au simba kubadili muungurumo wake; lakini mwanadamu anaweza kujibadili na kuigiza sauti yoyote na pia kuigiza kama yoyote katika wanyama yeye kaumbwa kwa mwili uliopangiliwa na roho ya kupendeza.

Upande mmoja ni mzuri na mwingine ni mbaya; upande mmoja upo hai na mwingine umekufa; upande mmoja unafanya kazi na mwingine umekaa; nusu moja imepangiliwa na nusu moja haijapangiliwa; nusu moja ni wa usiku na nusu nyingine ni mchana; nusu moja ni giza na nusu moja ni mwanga; nusu moja imefichwa nusu moja ipo wazi; nusu moja unagundulika kwa kugusa nusu moja kwa hekima; upande mmoja ni wa muda upande mmoja ni endelevu; kuona haya kwa mambo ya aibu na yenye kudhalilisha kufanya unachopenda kujuta.

Upande mmoja ni mwenye busara na upande mwingine ni usio na busara,
mwanadamu anaonekana kuwa na tabia ya utulivu wa udongo, upole wa upepo, urafiki wa moto na utulivu wa maji.

Hivyo, yeye ni wastani kwa mwenendo au mienendo yake ambayo ndio roho ya maisha hapo yaani elewa anatabia zote za maada zote nne na ndio roho ya maisha.

Kwa mwenendo wake anatambua joto la moto kupitia asili yake ya moto(nguvu yake ya moto) aliyonayo na ubaridi wa maji kupitia asili yake ya ubaridi na kuendelea katika maada mbili zilizobaki.

Tofauti na hilo pia, kichwa chake kinawakilisha umbile lake la duara mbinguni mwanga; kama vile kuona, kunusa, kuonja, kuongea. Macho yake ni sawa na jua na mwezi, matundu ya pua zake ni kama aina mbili za upepo, mbele yake ni kama mchana na nyuma yake ni kama usiku,anavyotembea ni kama nyota na ukaaji wake ni kama amepangiliwa, na kufa kwake ni kama kuungua kwao.

Ndani yake ogani zipo saba sawa na sayari zinazotembea, ana mifupa saba kichwani kwake ambayo ni sawa na siku za wiki,
ana vetebras 24 mgongoni kwake ambazo ni sawa na saa 24 za siku moja usiku na mchana anajoint 28 ambazo ni sawa na nyumba za mwezi na idadi ya alphabet, idadi ya utumbo wake ni sawasawa na mwandamo wa mwezi,idadi ya arteries zake ni sawa na 365 pamoja na veins zake ambazo ni sawa sawa na siku za mwaka mzima. idadi ya characteristics zake ni sawa sawa na mabadiriko ya muda kwa mwaka.

Macho yake ndio wapelelezi wake, nguvu ya uzungumzaji wake inafananisha na mfalme(khalifa wa dunia) masikio yake ndio wataarifu wake, ulimi wake ndio mkalimani wake,moyo wake ndio sofa la elimu yake, tumbo lake ndio hazina yake, kibofu chake ndio chanzo cha uvumilivu wake hivyo nyama yake haiwezi kupasuka, ni kifungo na matibabu ya mwili, mapafu yake ndio feni zake, mikono yake ndio walinzi wake na miguu yake ndio usafiri(gari) yake. nyama zake ni sawa na ardhi,mifupa yake ni kama milima,nywele zake ni kama mimea, arteries zake ni kama madawa na ogani za tumboni mwake ni kama madini.

Mwili wake umejumuisha johari tisa zilizojengwa juu ya mizunguko tisa kila moja ndani ya nyingine, mzunguko wa nje umezungukwa na nyama, mifupa, misuli, neva, ubongo, ngozi na kucha
Ubongo umejazwa kwenye kijishimo cha mifupa. Kazi yake ni kumaintain nguvu na mzunguko wa mifupa. kazzi ya mifupa ni kushikilia na kuweka sawa nyama zinazouzunguka. Kazi ya misuli ni kufunga jointi na ogani zifanyazo kazi. kazi ya nyama ni kuzuia kasoro ndani ya mwili na kukinga mifupa isipasuke au kuhama pahala pake kazi ya arteries ni kufikisha damu katika sehemu mbalimbali za mwili.

Kazi ya damu ni kusawazisha joto la mwili na kumaintain uhai kurekebisha joto na kuzalisha mwendo, kazi ya ngozi ni kukinga nyama na vya ndani kutokudondoka kuzuia kugawanyika au kutawanyika, mwili una matundu 12 ambayo ni sawasawa na vigawanyiko vya nyota kwa kuwa kuna vigawanyiko sita kaskazini na sita kusini,
kuna matundu sita kushotoni kwa mwanadamu na sita kuliani kwa mwanadamu.

Pia mwenendo wa sayari saba mbinguni ambazo huaminika zinaaffect mwenendo wa maisha ya mwanadamu, (soma kwenye thread yangu ya nyota: Ijue nyota yako: Fahamu mengi kuhusu nyota yako)
sayari hizi ambazo kiroho huaminika zina uhai ambao zinaweza kumsaidia mwanadamu katika kuarchieve mambo mbali mbali ikiwemo mafanikio kupitia madini,wanyama,mimea ni vingi vinazungumziwa humo katika kuongeza ujuzi na usalama wa kiumbe hai (hii imekaa kiimani pia)

Kwa muda huu nitaishia hapa ila panapo majaaliwa pakikucha nitaendelea

Rakims
 
Rakims

JF-Expert Member
Jun 4, 2014
4,038
2,000
Mtiririko wa mawazo yako ni mazuri kwa fikra nyumbulifu nikupongeze kwa hilo ila sikubaliani na fikra za mwanadamu kujikweza juu ya viumbe wenzake kuwa ni mungu wao(mtawala) eti kisa kwa akili zako wajiisi umeumbwa special kuliko wao,

Umeelezea kuusiana na maumbile ya mwanadamu ukioanisha na nyakati,maumbile ya ulimwengu na vilivyomo,upande mzuri na mbaya n.k ambavyo vyote vimepangwa/kugunduliwa au ku-originate kutokana na fikra za mwanadamu hili vitumike na mwanadamu kuweza kuyamudu mazingira yake(hili aweze kuishi yampasa kusaka maarifa)

Pointi yangu ni kuwa kama walivyo viumbe wengine(wasivyojua uwepo wao duniani na purpose) hata mwanadamu ni mjinga kwenye hilo pia
Kama wewe utamzidi bundi au paka kwa maarifa yakibinahadamu kwa kufanya/kuunda vitu kwaajili ya matumizi yako na ukahisi kuwa paka au kuku ataelewa/ku-appreciate ulichofanya ni ujinga

kwa maana kila kiumbe anaishi katika mipaka ya ufahamu wake mwenyewe na kile afanyacho nikulingana na mazingira ya uwepo wake katika ulimwengu huu hivyo wewe na mwewe mnaishi dunia mbili tofauti ndani ya dunia moja kila mmoja wenu akimjaji mwenzake juu ya uelewa wake.
Mwanadamu ni bora kwa lipi ikiwa anakufa kama viumbe wengine?
Ni kiumbe gani mwenye mwili mkubwa(umbo) aliyeumbwa dhaifu kuhimili hostility ya mazingira yake tu ikawa mtihani kama siyo binadamu?

-Kwa maana hiyo akawa na/akatumia uwezo wa kufikiri zaidi hili kuweza kusurvive kama wenzake na siyo kuwa ni bora kuliko wengine wanaoweza kuhisi zaidi,kunusa zaidi,kuona usiku, kukimbia zaidi,kulala kwenye mvua na barafu,kujitafutia au kujitengenezea chakula chao wenyewe kama miti n.k

Ni binadamu tu ndo mwenye hizo 4 Elements na viumbe wengine hawana hizo sifa,Je ni kitu gani mwanadamu anacho cha ziada kuliko hao wanyama?

Itoshe kusema tu kwamba mimi naamini kuwa kila kiumbe yupo tofauti kimaumbile na kiakili katika hali ya msawazo(balanced) inayomfanya aendane na mazingira ambayo ndo chanzo chake na uwepo wake na hiyo akili uliyonayo/au anayokuwa nayo mnyama inawatosheleza wote

na hakuna aliyezaidi ya mwingine mkivaa uhusika wa kila mmoja wenu mtajishangaa kuwa hakuna penye kasoro bali ni kipimo cha kusurvive na kila kiumbe anatafakari usiku na mchana atasurvive vipi na kile kinachotekea kama matokeo ya struggle hii ndo kinachomtofautisha binadamu na miti,wadudu au wanyama kimtizamo,

Wakati ukweli hapo ni kuwa licha ya akili tofauti(mitizamo) kulingana na uwezo waliopewa kimazingira viumbe wote hapo hakuna anayeweza kung'amua fumbo lakuishi pasipo mwenzake/dunia au kuacha kuangaikia kusurvive nakuchange/kushepu ulimwengu kuwa wanachotaka na wasife n.k hivyo wote bado wanaukomo wa maarifa na hawajapiga hatua kubwa katika ufahamu.
Habari mkuu, Asante kwa sifa uliyonipa vile vile asante kwa kujaribu kunikosoa maana napenda zaidi wanaonikosoa kwa maana wananipa nafasi either kama sio kuwaelimisha zaidi basi ni kuingia nao mjadala katika kuexpand mind yangu na wao pia,
Nikueleweshe jambo moja baada ya jingine kulingana na hoja zako.

  • Unaposema akili ya mwanadamu ina ukomo kwanza hapo unakuwa umekosea kwa maana ukomo wa akili ya mwanadamu ni pale anaposema kwamba "hili naishia hapa sitaki zaidi", au "wacha mengine niachie wenye kutaka kuendelea nayo" maana yake ni kwamba mwanadamu hana mpaka maalumu wa fikra yake ama akili yake ni hadi pale ambapo alipokadiriwa na muumba wake in case una amini uwepo wa Mungu maana tangu tu umesema tuko balanced unaonekana kurefer kwenye balance of nature(life cicle & dealth) ambayo ni ya watu ambao wapo brain washed kwamba(zaliwa=soma=ajira=oa=zaa=lea=wekeza=kula pension=kufa) hadithi imeisha. tuna sababu ya kuumbwa kwa maumbile haya na tuna purpose ya kuwa hapa duniani.

  • Pili elewa ya kwamba kikubwa alichokadiriwa mwanadamu bora kuliko viumbe wengine ni uwezo wa akili yake(UBONGO) usije kuaminishwa kuna kiumbe duniani ana uwezo wa kukuzidi akili ikiwa unaamini hivyo basi kwenye cicle yenyewe ya neno IMANI haupo.

  • Kuhusu fumbo unalozungumzia elewa ya kuwa binadamu teyari alishafumbuliwa yote yanayohusu dunia mwanzo na mwisho wake na anaakili hiyo ambayo inaweza kumuonyesha mwanzo wake ni upi na mwisho wake ni upi ikiwa wewe bado unatafuta kujua njia yako basi usiifunge akili yako mkuu kuishia hapo uliposema kuwa nanukuu "Mimi naamini (kuamini ni asili ya kiumbe binaadamu akiwa na maana ya kukubali kitu au jambo lipo au ni kweli hasa yale ambayo hana uthibitisho nayo hadi pale yanapotokea. hivyo kwa kusema kila mtu afuate imani ya kila mtu tutajikuta leo tunasali uchi msikitini na kesho kanisani na siku inayofuata tutajikuta tunaabudu chakula kwa maana kinatupa uhai na vilevile tutaamini hata bange ni Mungu. Hivyo usiamini kitu chochote bila uthibitisho kila kitu kinachoaminika basi kimethibitika uwepo wake.
Rakims
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom