Jitahidi ujue lugha mama (lugha ya kabila lako)

Gentleman P

JF-Expert Member
May 23, 2018
370
453
Habari wana JF,

Wengi wamezaliwa mjini, anachojua tu ni kwamba yeye ni wa Kabila fulani, ila ukimuongelesha kwa Lugha hiyo ya kwao anakuwa hajui chochote zaidi ya basic terms na salamu tu.

Katika maisha, Lugha ni nyenzo muhimu ya maendeleo.

Kuna lugha ya taifa (kiswahili), lugha mama (ya kabila lako), lugha ya biashara (american english), lugha ya sheria (british english), lugha ya mapenzi/mahaba/wapendanao (kihispania), lugha ya ujasiriamali (kichina), lugha ya dini (kiarabu) na lugha ya utalii (kifaransa).

Zote zina matumizi tofauti kwa nyakati tofauti (mfano kwny biashara English haikwepeki, kwenye utalii Kifaransa hakikwepeki, kwenye utambulisho wako kitaifa wewe kama mtanzania Kiswahili hakikwepeki, etc)

Leo nikazie faida moja ya kwanini Lugha mama (ya kabila lako...kijita, kisukuma, kihaya, etc) ni muhimu kwa maendeleo yako:

Kabila ni jamii, ndio maana lina mila na desturi, na hata lugha yake...ukienda ugenini, ukakutana na mtu wa kabila lako, automatically huyo ni NDUGU yako.

Angalia biashara nyingi, kuna undugu ndani yake, na ukifuatilia utaona watu hao wanatoka kabila moja.

Pia angalia nguvu ya fadhila: watu ni matajiri mjini au wengine wanahangaika lakini atajitahidi ajenge kijijini kwao...kwenye kabila lao...alikozaliwa.

Mifano ni mingi...ila ukishindwa kuwasiliana kwa lugha yako, ni ngumu kusaidika na kupata sapoti ya watu wa kabila lako walioko mjini au huko ugenini uliko.

USHAURI:
Tafuta dictionary ya lugha ya kabila lenu, zinapatikana kwny maduka mengi ya kimishenari hasa AIC, Moravian na Anglican

Pia connect na ukae na watu wa kabila lako, chukua maneno mawili au matatu kwa siku.

Asanteni.
 
Kuna waha wawili walizamia uzunguni huko!mmoja anajua kikwao mmoja ni born town. Wakapandishwa kizimbani bwana,mmoja yule akasema mie ni mnyarwanda akaongea kinyarwanda akaonekana kweli ni mkimbizi,wapili sasa!
 
Kazi kwa wazenji , hawana lugha yao dhidi ya lahaja za kiswahili, na kiswahili fasaha . Ina mantiki Sana hii kwani vizazi vinaanza kupoteza lugha mama zao !!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom