Jirani yetu anaumwa sana lakini hawa ndugu zake hawampeleki hospatal

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,973
27,209
Hapa mtaani kwetu kuna jirani yetu amemleta mzee wake kutoka huko kijijini ni mzee sana kati ya miaka 83 / 86 kwa kumkadiria aliletwa kuwasalimia baada ya mda akaanza kuvimba miguu mara mkojo unatoka wenyewe bila yeye kujua na akienda chooni (haja kubwa) anakaa sana huko na wakati anajisaidia anagumia sana mlio kama haja ni ngumu hivi!

Na usiku wakati amelala anapumua huku anatoa mlio kama analia vile sasa mimi nimewauliza babu amefanya nini mbona yuko hivyo wanadai eti ni mzima hana tabu kwa sababu amebadilisha mazingira ndo maana iyo hali imemtokea lakini kimwonekano huyu mzee ni mgonjwa sana hawa ndugu zake siwaelewi wana mpango gani na huyu babu!

Ushauri wenu tumsaidieje huyu babu!
 
Acha mambo ya watu wanasiri zao mkuu wakati mwingine ukijifanya unahuruma huruma yako itakuponza wewe unazani hadi wamemtoa kijijini hawajui kama anaumwa wao ndo wanajua siri ya ugonjwa wako shauri yako we endelea kufatilia mambo ya watu
 
Huyo siku zake za kukaa hapa Duniani zimeshakwisha. Kumpeleka hospitali ni kupoteza hela. Mwache, afie kwa amani hapo hapo home...
 
Mkuu roho inaniuma sana
 
Duu!!inaonyesha huna huruma hata kidogo
Huruma ya nini hapo? Kila nafsi itaonja mauti... Kama umeshawahi kufiwa na watu wa dizaini hiyo utakuwa unaelewa. Kuna mama mmoja mume wake aliugua sana na mama alitimia zaidi ya milioni ishirini kumtibu na bado alikufa. Baadaye yule mama huwa anajilaumu na kusema kama angejua kuwa siku za mumewe zilikuwa zimeshakwisha wala asingepoteza fedha zile zote...
 
Mkuu nenda kwa mwenyekiti waserikali ya mtaa wako ebu fanya kitu kwa ajili ya maisha ya huyo mzee. Barikiwa.
 
acha kujishughulisha na mambo ya watu!! mtu wa miaka miaka hyo maradhi Ni kawaida SNA. hata akipelekwa hospi still atarud kuhudumiwa home!! yawexkana kabla ya kuja hapo alikuwa anatibiwa somewhere!!
 
Huruma ya nini hapo? Kila nafsi itaonja mauti... Kama umeshawahi kufiwa na watu wa dizaini hiyo utakuwa unaelewa. Kuna mama mmoja mume wake aliugua sana na mama alitimia zaidi ya milioni ishirini kumtibu na bado alikufa. Baadaye yule mama huwa anajilaumu na kusema kama angejua kuwa siku za mumewe zilikuwa zimeshakwisha wala asingepoteza fedha zile zote...
kma asingemtibia na Pesa zipo angebak na guilty maisha yake yote. Ni muhimu kuonyesha jitihada
 
Huyo siku zake za kukaa hapa Duniani zimeshakwisha. Kumpeleka hospitali ni kupoteza hela. Mwache, afie kwa amani hapo hapo home...
matibabu kwa wazee ni bure hakuna gharama kubwa..inawezekana umri umeenda lkn anaweza akawa na hekima na ushauri tutakaohitaji hivyo kuishi ni haki yake..mbona mzee mwinyi ana miaka 90+ na bado tunamwitaji mkuu??
 
Wewe utafanya hayo kwa babu yako?
Ilishatokea kwa baba angu... Mpaka dakika za mwisho namuuliza daktari kwamba huyu mtu atapona au tuanze kuandaa jeneza? Daktari alikataa kuniambia ukweli, lakini mimi mwenyewe hali nilishaiona kwamba huyu mtu siku zake zimeshakwisha hapa Duniani, na kweli siku moja baadaye akaaga Dunia. Basi tukampumzisha kwa heshima zote kama baba mzazi...
 
Watoto ni wengi humu.........ushauri wao ni wakitoto tu nawapongeza wale wote walioshauri kuwa mtoa mada akaripoti Polisi, mwenyekiti wa S/mtaa, taasisi za Dini na kadhalika.........

UNDUGU SIO KUFANANA BALI KUSAIDIANA NA KUMBUKA KUNA SIKU NAWE UTAKUWA MZEE.........
 
Waswahili wanasema mgonjwa hufa kiacha dawa,hivyo si sawa mgonjwa kukaa bila dawa hata kama wa kufaleo au kesho ..
 
Watoto ni wengi humu.........ushauri wao ni wakitoto tu nawapongeza wale wote walioshauri kuwa mtoa mada akaripoti Polisi, mwenyekiti wa S/mtaa, taasisi za Dini na kadhalika.........

UNDUGU SIO KUFANANA BALI KUSAIDIANA NA KUMBUKA KUNA SIKU NAWE UTAKUWA MZEE.........
Kweli mkuu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom