Jirani Mganga

Khantwe

JF-Expert Member
Dec 20, 2012
59,409
119,014
Habari za asubuhi,
Niende moja kwa moja kwenye mada, dada yenu siku za karibuni nimehamia mtaa wa saba sasa hii nyumba ina pande mbili...upande wa mbele wanakaa wawili na upande wa nyuma tunakaa wawili.
Sasa huyu jirani yangu tunayekaa nae upande wa nyuma majirani wengine wanadai ni mganga wa kienyeji, mkaka yupo nadhifu tu sasa kinachoniogopesha huyu mkewe ni mkarimu sana, huwa ananipa sana chakula na juzi kanipa nyama ya kuku nikasema isijekuwa ndio zile wateja wanaleta haha... Kiukweli mimi najipa moyo kuwa ndio wale wa tiba mbadala, najishawishi kuwa huko ndani hakuweza kuwa na tunguli au nyie wadau mnaonaje.
 
Sisi hatuoni kitu..hujaweka mapichapicha

Sema nini,kama huwez ama apo jiweke karibu na Mungu
 
Alafu bora wewe..
Nimepanga nyumba moja masharti kibao
Nikaambiwa humu unakaa na mkeo wakati huo nataka nikae na dogo
Tukabembeleza akasema ndan ya mwezi mmoja aondoke nikasema sawa.
Baada ya kuamia ilivyopita wiki tuu..mzee nikawa silali usiku kama nakabwa ivi alafu nikasikia mtu ananiambia"Mganga atakasitika"
Nikawasimulia watu hawakuamini basi ikapita kama mwezi niko ndani na dogo akaja mganga mlangoni sijui ndo alikuwa anafukia dawa dogo kashtuka kaniaamsha kucheki kweli.
Ndo wakaamini na muda huo sasa wananiambia nimwage maji ya baraka.
Hatati sana hizi nyumba za kupanga.
Now nimesepa zangu nimemuacha dogo pale aendelee kuliwa kiboga taratibu na majini ya yule mzee nasikia anafuga majini.
 
Alafu bora wewe..
Nimepanga nyumba moja masharti kibao
Nikaambiwa humu unakaa na mkeo wakati huo nataka nikae na dogo
Tukabembeleza akasema ndan ya mwezi mmoja aondoke nikasema sawa.
Baada ya kuamia ilivyopita wiki tuu..mzee nikawa silali usiku kama nakabwa ivi alafu nikasikia mtu ananiambia"Mganga atakasitika"
Nikawasimulia watu hawakuamini basi ikapita kama mwezi niko ndani na dogo akaja mganga mlangoni sijui ndo alikuwa anafukia dawa dogo kashtuka kaniaamsha kucheki kweli.
Ndo wakaamini na muda huo sasa wananiambia nimwage maji ya baraka.
Hatati sana hizi nyumba za kupanga.
Now nimesepa zangu nimemuacha dogo pale aendelee kuliwa kiboga taratibi na majini ya yule mzee nasikia anafuga majini.
Haha eti aendelee kuliwa kiboga humpendi mdogo wako wewe
 
Habari za asubuhi,
Niende moja kwa moja kwenye mada, dada yenu siku za karibuni nimehamia mtaa wa saba sasa hii nyumba ina pande mbili...upande wa mbele wanakaa wawili na upande wa nyuma tunakaa wawili.
Sasa huyu jirani yangu tunayekaa nae upande wa nyuma majirani wengine wanadai ni mganga wa kienyeji, mkaka yupo nadhifu tu sasa kinachoniogopesha huyu mkewe ni mkarimu sana, huwa ananipa sana chakula na juzi kanipa nyama ya kuku nikasema isijekuwa ndio zile wateja wanaleta haha... Kiukweli mimi najipa moyo kuwa ndio wale wa tiba mbadala, najishawishi kuwa huko ndani hakuweza kuwa na tunguli au nyie wadau mnaonaje.
You're the next msukule
 
Duh umesoma uzi kweli?
Nimesoma,
Zaidi ya kuambiwa na majirani zako, wewe hujaonesha kwa utashi wako kuwa unahisi ni mganga.
Tuambie zaidi umejuaje zaidi ya kuambiwa na jirani zako,
Vinginevyo hutakuwa hujachanganya na zako.
 
Nimesoma,
Zaidi ya kuambiwa na majirani zako, wewe hujaonesha kwa utashi wako kuwa unahisi ni mganga.
Tuamhie zaidi umejuaje zaidi ya kuambiwa na jirani zako,
Vinginevyo hutakuwa hujachanganya na zako.
Mimi sijaona dalili za uganga ila hainifanyi nipuuze maneno ya majirani wengine halafu kwani ni mangapi huwa tunayaamini kwa kusikia tu si lazima kila kitu uthibitishe kwa macho yako...hao walioniambia wangeanza kutunga ili iweje
 
Binafsi nakushauri usile, just don't eat. Binadamu wa siku hizi tumekuwa wanyama, hata kama sio mganga/mlozi/mchawi. Anaweza kukufanya kitu kibaya. Sema asante nashukuru, nimeshakula...
 
Sijasema uthibitishe kwa macho, si kila kitu kina hitaji kithibitishwe na macho ndio kiwe kweli.
Anyway, mi habari za uganga na uchawi ni habari nilizo zipuuza tangu zamani.

Ni habari zilizojaa hisia zaidi ya uhalisia.
Kama utakuwa una amini habari za kuambiwa bila kujipa muda kujidhihirisha itakupa shida mbeleni.

Jifunze kuhimili hisia, weka kifuani, jipe muda kubaini.

Pamoja na kwamba tunatofautiana ktk kuamini masuala ya kiganga, nakushauri usihukumu kabla ujajidhihirisha mwenyewe.

Ni mtazamo tu.
 
Ooh asante rafiki kwa ushauri

Ahsante
 
Haha eti aendelee kuliwa kiboga humpendi mdogo wako wewe
Ata ungekuwa wewe usingeekaa apo..kifupi nyumba ina masharti kama yote.Siku namwambia mwenye nyumba nimepata sehemu bado kumalizia kodi kidogo ndani ya wiki moja..sikulala usiku wake(nilisumbuliwa kama nakabwa) na nilivyoamka nikasepa zangu.Yaan ni kma nilitoa taarifa kuwa wakikaza tuu kidogo naamsha na ndo wakafanya kweli.
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom