Jirani anaweza akaunda jeshi la kifamilia so soon

McDonaldJr

JF-Expert Member
Sep 25, 2013
6,392
2,000
ImageUploadedByJamiiForums1386789671.696398.jpg ImageUploadedByJamiiForums1386789741.394763.jpg
Habari kwanza waungwana umu jamvini naamini mko na afya kwa nguvu za Muumba.
Kumekua na wimbi la wa TZ kumiliki silaha kwa kasi ya kutisha na serikali na chombo husika wanajifanya hawaoni kbs mpaka naanza kuamini utoaji wa vibali katika kumiliki silaha masharti yatakua rahisi sana miaka hii.
Napata shaka na baba wa swahiba wangu ambae naona kwake ivi vya moto anaona fashion kwake maana baba anazo 2, kaka ambae ni dj kwenye kampuni yao anayo 1,swahiba wangu nae naona kavuta cha moto siku za karibuni naogopa kuuliza kuhusu bi mkubwa wasije test ivi vitu kwangu ila kwa hii trend atakua nayo sasa akinunuliwa na yule binti nna uhakika soon watakua na jeshi lao la kifamilia hata ugomvi wa kuombana chumvi na jirani utamalizwa kwa mlio wa mtutu.
Turudi kwa ndugu zangu tunaokaa Bar imekua kawaida mtu anakata masanga mezani kuna bia na bastola tena kwenye bar moja wanaringishiana watu kadhaa ndo maana nikienda hata kuangalia mpira bar nashangilia kwa mashaka nisije tokea kwenye media nikiwa mfu bure.
Serikali na jeshi la polisi wamejusahau kwny hili naona ukipimwa akili na una milioni unaruhusiwa kuvuta mkwasa km iPhone tu nna uhakika siku zijazo kesi za kawaida zitamalizwa na bunduki mfn ukifumaniwa,umemsengenya,umetukana ni bunduki tu sasa ivi ukiwa na GX100 unaomba silaha khaaaa upuuzi mtupu.
Siku tukizoea hii milio ya bastola naomba asitafutwe mchawi maana tunalifumbia macho sisi wenyewe jitu lina silaha mwizi hayupo ndo hapo unasikia shabiki wa Barcelona kampiga risasi shabiki wa Man U kisa kumtukana Messi...,ni haya kwa leo Alamsiki.
 

Misa

JF-Expert Member
Jul 5, 2013
839
195
tuombee nchi yetu iendelee kuwa na amani tu,siku ikitokea la kutokea baya nchi yetu kutawaka moto kila mtaa na hv vya moto
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom