JIPU lingine TRA : Tumekamata simu 2,744 za StarTimes

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
TRA : TUMEKAMATA SIMU 2,744 ZA STARTIMES

Mkurugenzi wa Huduma ya Elimu kwa Mlipa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo amethibitisha kukamatwa maboksi 294 yenye simu 2,744, na vifaa mbalimbali vya simu katika ghala la Kampuni ya StarTimes.

Kayombo amesema mamlaka hiyo ilikamata maboksi hayo ambayo thamani yake haijajulikana baada ya kutilia shaka nyaraka za mizigo hiyo iliyoingizwa nchini ikiwa haionyeshi ni ya nani, ilikotoka pamoja na kuwepo kwa taarifa zenye utata kuhusu idadi ya mizigo hiyo.

"Tulipokea taarifa za utata wa mizigo iliyodaiwa kuingizwa na kampuni hiyo jambo lililotulazimu kwenda kuikamata kwa ajili ya uchunguzi.

“Tulikamata maboksi yaliyokuwa na simu na vifaa mbalimbali kama vile betri, chaji za simu, powerbank na kava za simu. Baada ya kuikamata tuligundua kulikuwa na udanganyifu wa idadi ya maboksi yaliyokuwa kwenye nyaraka, kwani zilisomeka kuwa kuna maboksi 211, lakini katika uchunguzi tulikuta 294,” alisema Richard Kayombo.


 
294-211=83

Hongereni-Japo Kuna vitu vikubwa vinapita bila kodi wafuatilie sio kudaka box 83 na Kujifanya wamefanya Kazi!
 
294-211=83

Hongereni-Japo Kuna vitu vikubwa vinapita bila kodi wafuatilie sio kudaka box 83 na Kujifanya wamefanya Kazi!
atleast inatia moyo,itafika itafikia kipind tutapunguza kias fulan,
 
Simu ni vipele sio majipu kaka....Kuna Majipu yanahitaji kutumbuliwa sio hivyo vipele hao TRA wanatafuta Kiki tu.
 
Inaonekana toka wameanza wamepitisha box ngapi mpaka sasa sema TRA waje na ishu hapa bwana sio vibox vya tecno ivyo bwana..madini wale kaburu chunya pale na kiwanja cha ndege kipo pale pale kodi wanalipa stahiki kweli au..
 
Huyu anaesema sio jipu ana lake, wewe simu zote hizo kama siku zote zinapitishwa bure hebu niambie toka startimes imeanzishwa wameiingizia serikali hasara kiasi gani kwa mwendo huo?? Jipu ni jipu tu halina maana ingine so tuwapongeze wanaopasua
 
Huyu anaesema sio jipu ana lake, wewe simu zote hizo kama siku zote zinapitishwa bure hebu niambie toka startimes imeanzishwa wameiingizia serikali hasara kiasi gani kwa mwendo huo?? Jipu ni jipu tu halina maana ingine so tuwapongeze wanaopasua
hizo masimu za kichina zina nn bhanaa 50 mara sijui ngapi khaaaaaaaaaaaaaaaaa kwanza wachina wenyewe wanakarakana za simu feki kk,kwahiyo sio ishu haifiki hata hela ya vits 1
 
magari ya examption fake yamejaa mabarabarani /
waanze kuyakamata sasa!
n.b
****
kama wewe ni mwl.umepatiwa examption ni shurti uliendeshe gari hilo / sio kufanya ujanja ujanja wa kuiuza examption hiyo
kwa mikataba ya kitaa!/
 
Kwani huyo kayombo si ndio kazi yake? Kuna haja gani ya kulitangaza hili as if ni issue kuuubwa wakati ndio zao miaka nenda rudi. Hizo box 83 zina kodi ya shiling ngapi ? Acheni kufanya kazi na magazeti kujipaitia ujiko wakati ni wajibu wenu.
 
wachina na baba riz na tuzo na vyeo.....Yaaani mchina ana nguvu bongo kama vile sijui nini...
 
Back
Top Bottom