Jipu lingine: Kodi kwa anayepokea hela kwa njia ya simu (double taxation ) sijui tuiiteje!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,874
Kweli hii sasa ni kama vile tupo gizani. Tena tumepangiwa mambo kwa juu juu sana bila hata waheshimiwa sana na watukufu wetu kutilia maanani mzigo huo wanaomtwisha mtanzania wa kawaida.

Naishukuru sana Jamii Forum kwani ndilo jukwaa pekee Tanzania tunalotumia kuijadili bajeti kwa uhuru (kwa dhati kabisa tutawaunga mkono kwa kila hali na mali)

Katika pitapita yangu kwenye bajeti nimekutana tena na hii kodi ambayo mpokeaji wa hela kwa njia ya simu (Airtel money, M-Pesa tigo pesa n.k) atakatwa kodi ambayo ni ile tozo ya kodi iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T

Sasa kinacholeta mkanganyiko ni kuwa hiyo hela aliyopokea huyo mpokeaji tayari imekatwa kodi kama hiyo yaani ile iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T wakati mtumaji akituma.Kifupi hapa tunafanya double taxation! Huu ni wizi wa makusudi kabisa. Mtumaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela na mpokeaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela! Kweli tumefikia huko?

Nimeenda mbali zaidi na kilichonichekesha zaidi ni sababu za waziri Mpango za kukata hiyo kodi namnukuu "Makampuni ya simu yanafanya ujanja kuhamisha taarifa za kutuma pesa kwa wanaopokea pesa kwa njia ya simu hivyo kuikosesha serikali mapato. Hivyo kwa kutumia njia hii ya kutoza kodi kwa mpokeaji na mtumaji tutadhibiti mianya ya ukwepaji kodi"
Very interesting!

Kama kweli serikali inatoa sababu kama hiyo, kwanini hiyo kodi ya mwanzo haikugawanywa mara mbili ili kutokumbana mlalahoi? Wangeigawanya kodi hiyo moja mara mbili (nusu kwa nusu) wahamishie kwa mtumaji na nyingine kwa mpokeaji ama lah wangetafuta soft ware inayoweza kukabiliana na tatizo hilo la kuhamisha taarifa kitu ambacho ni rahisi sana!

Na hiyo V.A.T inayotozwa kwenye miamala ya simu ni nini maana yake? Kwanini wakaiita V.A.T?
 
Wahi kwa mamvi akupe vidonge huelewi maana ya "double taxation" siyo neno kama lilivyo neno ukawa, hii ni "term" iliyobeba maana inayojulikana Kimataifa. Kwani ukituma pesa, gharama za kutuma na kutoa ni sawa? Ukienda kununua kitu dukani, unadhani huyo wa dukani huko alikonunua hakutozwa kodi? Sasa hiyo haiitwi double taxation, dt ni term nyingine kabisa.
 
Ufafanuzi wa kutosha ulishatolewa humu Jf siku nyingi tu. Kautafute au mods waiiunganishe huko hii thread yako.
 
G Sam hebu soma tena ulichoandika, maana naona ndo umeleta mkanganyiko zaidi kushinda hata uliopo. Kwa ufupi haujui kwamba haujui na hili ndio tatizo la waTZ tulio wengi. Kila kitu tunakifahamu.
Wewe unayejua ndio utoe elimu kumaliza mkakanyiko... Sio kulalamika lalamika hivi. Jibu hoja kwa hoja...sio hoja kwa kioja!
 
G Sam hebu soma tena ulichoandika, maana naona ndo umeleta mkanganyiko zaidi kushinda hata uliopo. Kwa ufupi haujui kwamba haujui na hili ndio tatizo la waTZ tulio wengi. Kila kitu tunakifahamu.
kakariri madesa ya PS ana apply kwenye Taxation!
 
Mshahara unakatwa kodi,unapelekwa benki,ukienda kuuchukua unakatwa kodi, kama umezoea kuchukua elfu hamsini hamsini au ishirini ishirini,kila ukienda unalimwa asilimia 18.

Ukituma mpesa unakatwa asilimia 18,unayemtumia akitoa anakatwa asilimia 18,kahela kale kale unakomtumia mama kijijini akanunue jembe kanapigwa huku na kule
 
Kweli hii sasa ni kama vile tupo gizani. Tena tumepangiwa mambo kwa juu juu sana bila hata waheshimiwa sana na watukufu wetu kutilia maanani mzigo huo wanaomtwisha mtanzania wa kawaida.

Naishukuru sana Jamii Forum kwani ndilo jukwaa pekee Tanzania tunalotumia kuijadili bajeti kwa uhuru (kwa dhati kabisa tutawaunga mkono kwa kila hali na mali)

Katika pitapita yangu kwenye bajeti nimekutana tena na hii kodi ambayo mpokeaji wa hela kwa njia ya simu (Airtel money, M-Pesa tigo pesa n.k) atakatwa kodi ambayo ni ile tozo ya kodi iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T

Sasa kinacholeta mkanganyiko ni kuwa hiyo hela aliyopokea huyo mpokeaji tayari imekatwa kodi kama hiyo yaani ile iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T wakati mtumaji akituma.Kifupi hapa tunafanya double taxation! Huu ni wizi wa makusudi kabisa. Mtumaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela na mpokeaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela! Kweli tumefikia huko?

Nimeenda mbali zaidi na kilichonichekesha zaidi ni sababu za waziri Mpango za kukata hiyo kodi namnukuu "Makampuni ya simu yanafanya ujanja kuhamisha taarifa za kutuma pesa kwa wanaopokea pesa kwa njia ya simu hivyo kuikosesha serikali mapato. Hivyo kwa kutumia njia hii ya kutoza kodi kwa mpokeaji na mtumaji tutadhibiti mianya ya ukwepaji kodi"
Very interesting!

Kama kweli serikali inatoa sababu kama hiyo, kwanini hiyo kodi ya mwanzo haikugawanywa mara mbili ili kutokumbana mlalahoi? Wangeigawanya kodi hiyo moja mara mbili (nusu kwa nusu) wahamishie kwa mtumaji na nyingine kwa mpokeaji ama lah wangetafuta soft ware inayoweza kukabiliana na tatizo hilo la kuhamisha taarifa kitu ambacho ni rahisi sana!

Na hiyo V.A.T inayotozwa kwenye miamala ya simu ni nini maana yake? Kwanini wakaiita V.A.T?
Ni sahihi ila mambo mengine kama ukitumia neno"unashindwa kuelewa" basi usiwe unatoa jibu la moja kwa moja kuwa double taxation. ..maana kumbe wewe binafsi ndiye hujaelewa!!!! Ungeomba au kutumia neno "kufahamishwa"kabla huja conclude hivyo

Sasa jiulize hivi"" ukituma pesa let's say m.pesa...kwa mtu fulani
(1) we mtumaji Kampuni inakukata pesa ya kutuma???? Naamini jibu ni ndiyo
(2) yule unaye mtumia akitoa hiyo pesa toka m pesa je anakatwa tena pesa???? Naamini unafaham jibu ni ndiyo
SWALI:- UNAMAANISHA KAMPUNI YA M PESA NAYO INATOZA MARA MBILI KWA PESA ILEILE???? (Double Taxation kwa maana yako????)
My take:- najua mojawapo ya makubaliano ya UKAWA baada ya Bunge kusitishwa ni KUTUMIA MITANDAO KADRI WAWEZAVYO KUONYESHA KAMA MKANGANYIKO KWA WANANCHI IONEKANE WAO NI MUHIMU SANA!!!! NA KWAMBA KUTOKUWEMO BUNGENI (Kwa sababu ya upuuzi wao tu) BAS BAJETI ILIYOPITA INA MAKOSA MEEENGI SANA!!!!
Lkn mnajidanganya sana!!!! Mnatumika sana ninyi mwishowe mtapuuzwa tu
Pamoja na kwamba hapa Bongo neno UPINZANI maana yake ni PINGA KILA KITU MBELE YAKO. .LKN MUDA MWINGINE HATA WATOTO MLIOWAZAA WANAJUTA KUPATA MZAZI AITWAYE MPINZANI MMECHOKWA SANA!!!@...

DOUBLE TAXATION Maana yake ni mtu mmoja kulipishwa mara mbili
Lkn hiyo ni transaction mbili kwa watu WAWILI TOFAUTI. ..Ni kama biashara...NDO MAANA KAMPUNI M PESA INAKATA KWA ANAYETUMA NA ANAYEPOKEA SI DOUBLE TAXATION. .The same apply kwa Serikali..ni tozo kwa anayetuma na kupokea..SIYO DOUBLE TAXATION. ..Please be informed !!!!!!!!
 
Tulia tukunyooshe,kipindi kile mlisema mwananchi hakatwi....mabenki yameanza kukata mnatuletea bhange gani tena?
 
Inavyoonekana wahusika hawakuona changamoto za haya wanayoyaanzisha. Na hii ni sehemu tu ya mkanganyiko lakini wanaoumia wanakufa kisabuni!
 
Ni sahihi ila mambo mengine kama ukitumia neno"unashindwa kuelewa" basi usiwe unatoa jibu la moja kwa moja kuwa double taxation. ..maana kumbe wewe binafsi ndiye hujaelewa!!!! Ungeomba au kutumia neno "kufahamishwa"kabla huja conclude hivyo

Sasa jiulize hivi"" ukituma pesa let's say m.pesa...kwa mtu fulani
(1) we mtumaji Kampuni inakukata pesa ya kutuma???? Naamini jibu ni ndiyo
(2) yule unaye mtumia akitoa hiyo pesa toka m pesa je anakatwa tena pesa???? Naamini unafaham jibu ni ndiyo
SWALI:- UNAMAANISHA KAMPUNI YA M PESA NAYO INATOZA MARA MBILI KWA PESA ILEILE???? (Double Taxation kwa maana yako????)
My take:- najua mojawapo ya makubaliano ya UKAWA baada ya Bunge kusitishwa ni KUTUMIA MITANDAO KADRI WAWEZAVYO KUONYESHA KAMA MKANGANYIKO KWA WANANCHI IONEKANE WAO NI MUHIMU SANA!!!! NA KWAMBA KUTOKUWEMO BUNGENI (Kwa sababu ya upuuzi wao tu) BAS BAJETI ILIYOPITA INA MAKOSA MEEENGI SANA!!!!
Lkn mnajidanganya sana!!!! Mnatumika sana ninyi mwishowe mtapuuzwa tu
Pamoja na kwamba hapa Bongo neno UPINZANI maana yake ni PINGA KILA KITU MBELE YAKO. .LKN MUDA MWINGINE HATA WATOTO MLIOWAZAA WANAJUTA KUPATA MZAZI AITWAYE MPINZANI MMECHOKWA SANA!!!@...

DOUBLE TAXATION Maana yake ni mtu mmoja kulipishwa mara mbili
Lkn hiyo ni transaction mbili kwa watu WAWILI TOFAUTI. ..Ni kama biashara...NDO MAANA KAMPUNI M PESA INAKATA KWA ANAYETUMA NA ANAYEPOKEA SI DOUBLE TAXATION. .The same apply kwa Serikali..ni tozo kwa anayetuma na kupokea..SIYO DOUBLE TAXATION. ..Please be informed !!!!!!!!
ufafanuzi mzuri. Pia ajibu kwamba yeye anapoenda kutuma mpesa mjini iende kule kijijini, hapo mjini anapotuma kuna wakala, si analipwa na voda? Je kule kijijini ambako pesa zinatolewa, si kuna wakala pia? Nae si analipwa na voda? Sasa kwani isikatwe kote kote? Yaani unataka upande basi kwenda ulipe halafu urudi na basi hilo hilo then usilipe useme ulilipa wakati wa kwenda?
 
Mshahara unakatwa kodi,unapelekwa benki,ukienda kuuchukua unakatwa kodi, kama umezoea kuchukua elfu hamsini hamsini au ishirini ishirini,kila ukienda unalimwa asilimia 18.

Ukituma mpesa unakatwa asilimia 18,unayemtumia akitoa anakatwa asilimia 18,kahela kale kale unakomtumia mama kijijini akanunue jembe kanapigwa huku na kule
wewe hujui afadhali ujinyamazie
 
Wahi kwa mamvi akupe vidonge huelewi maana ya "double taxation" siyo neno kama lilivyo neno ukawa, hii ni "term" iliyobeba maana inayojulikana Kimataifa. Kwani ukituma pesa, gharama za kutuma na kutoa ni sawa? Ukienda kununua kitu dukani, unadhani huyo wa dukani huko alikonunua hakutozwa kodi? Sasa hiyo haiitwi double taxation, dt ni term nyingine kabisa.
 
ufafanuzi mzuri. Pia ajibu kwamba yeye anapoenda kutuma mpesa mjini iende kule kijijini, hapo mjini anapotuma kuna wakala, si analipwa na voda? Je kule kijijini ambako pesa zinatolewa, si kuna wakala pia? Nae si analipwa na voda? Sasa kwani isikatwe kote kote? Yaani unataka upande basi kwenda ulipe halafu urudi na basi hilo hilo then usilipe useme ulilipa wakati wa kwenda?
Na hapi ndipo Rais Magufuli alipowakamata ndo maana wanatapatapa...Serikali ilikuwa inapata Kodi kwa ANAYETUMA PESA TU (Swali hapo ni Hiyo 18% alikuwa anatozwa mlaji au kampuni???? )
Lakini yule anayepokea pea iliyokuwa inakatwa na Kampuni ilikuwa haikatwi Kodi. ...Kwa sasa wamebanwa kotekote
Halafu UKAWA wanajifanya kutumia mitandao wakiwemo hawa akina G sam kupotosha!!!!! Haya yana mwisho tunaelewa vizuri sana lengo la Serikali. ..ni suala la muda tu mtajiona wajinga tena weupeeee. ..subilini tu
 
Kichwa panzi kama wewe unatakiwa ukafungiwe ufipa miaka yote ushinde na Mbowe humo ukimpangusa viatu.

Ukiachwa huku nje unaharibu vizazi Vya Mungu
 
Da!!!! Yani anajuuuta sana kupost hii thread....tatizo lao wanatumika sana kijingajinga
Lengo lao ionekane eti kwa kuwa walizila bungeni basi eti bajet iliyopitishwa haifai????? Ni upuuzi kweli yani...waache kutumika kama toilet paper ona sasa anavyoonekana Mburula!!!!! What a shame! !!!!!
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom