Jipu lingine: Kodi kwa anayepokea hela kwa njia ya simu (double taxation ) sijui tuiiteje!

Kichwa panzi kama wewe unatakiwa ukafungiwe ufipa miaka yote ushinde na Mbowe humo ukimpangusa viatu.

Ukiachwa huku nje unaharibu vizazi Vya Mungu
Mbowe kaingiaje hapa?Kama mmpeta jambo la kundolea stress na hasira zenu za kutwa nzima kwa kutetea wanaovurunda na kukurupuka kila siku katika maamuzi yao,msiwahusishe na wasio husika.
 
Na hapi ndipo Rais Magufuli alipowakamata ndo maana wanatapatapa...Serikali ilikuwa inapata Kodi kwa ANAYETUMA PESA TU (Swali hapo ni Hiyo 18% alikuwa anatozwa mlaji au kampuni???? )
Lakini yule anayepokea pea iliyokuwa inakatwa na Kampuni ilikuwa haikatwi Kodi. ...Kwa sasa wamebanwa kotekote
Halafu UKAWA wanajifanya kutumia mitandao wakiwemo hawa akina G sam kupotosha!!!!! Haya yana mwisho tunaelewa vizuri sana lengo la Serikali. ..ni suala la muda tu mtajiona wajinga tena weupeeee. ..subilini tu
Kwa huu upuuzi uliouandika hapa,unakushusha hadhi mkanganyiko kati ya BOT na TRA usingekuwepo kama mbeleni tunge aibika peupe.kwa sababu hatutaaibika,nyie ndio mmeaibika badala yetu
 
Wahi kwa mamvi akupe vidonge huelewi maana ya "double taxation" siyo neno kama lilivyo neno ukawa, hii ni "term" iliyobeba maana inayojulikana Kimataifa. Kwani ukituma pesa, gharama za kutuma na kutoa ni sawa? Ukienda kununua kitu dukani, unadhani huyo wa dukani huko alikonunua hakutozwa kodi? Sasa hiyo haiitwi double taxation, dt ni term nyingine kabisa.
Sijakuelewa hapo unapofananisha hela inayokatwa pande mbili, mtumaji na mpokeaji... ukumbuke unahusisha bidhaa
 
Kweli hii sasa ni kama vile tupo gizani. Tena tumepangiwa mambo kwa juu juu sana bila hata waheshimiwa sana na watukufu wetu kutilia maanani mzigo huo wanaomtwisha mtanzania wa kawaida.

Naishukuru sana Jamii Forum kwani ndilo jukwaa pekee Tanzania tunalotumia kuijadili bajeti kwa uhuru (kwa dhati kabisa tutawaunga mkono kwa kila hali na mali)

Katika pitapita yangu kwenye bajeti nimekutana tena na hii kodi ambayo mpokeaji wa hela kwa njia ya simu (Airtel money, M-Pesa tigo pesa n.k) atakatwa kodi ambayo ni ile tozo ya kodi iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T

Sasa kinacholeta mkanganyiko ni kuwa hiyo hela aliyopokea huyo mpokeaji tayari imekatwa kodi kama hiyo yaani ile iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T wakati mtumaji akituma.Kifupi hapa tunafanya double taxation! Huu ni wizi wa makusudi kabisa. Mtumaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela na mpokeaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela! Kweli tumefikia huko?

Nimeenda mbali zaidi na kilichonichekesha zaidi ni sababu za waziri Mpango za kukata hiyo kodi namnukuu "Makampuni ya simu yanafanya ujanja kuhamisha taarifa za kutuma pesa kwa wanaopokea pesa kwa njia ya simu hivyo kuikosesha serikali mapato. Hivyo kwa kutumia njia hii ya kutoza kodi kwa mpokeaji na mtumaji tutadhibiti mianya ya ukwepaji kodi"
Very interesting!

Kama kweli serikali inatoa sababu kama hiyo, kwanini hiyo kodi ya mwanzo haikugawanywa mara mbili ili kutokumbana mlalahoi? Wangeigawanya kodi hiyo moja mara mbili (nusu kwa nusu) wahamishie kwa mtumaji na nyingine kwa mpokeaji ama lah wangetafuta soft ware inayoweza kukabiliana na tatizo hilo la kuhamisha taarifa kitu ambacho ni rahisi sana!

Na hiyo V.A.T inayotozwa kwenye miamala ya simu ni nini maana yake? Kwanini wakaiita V.A.T?
Rafiki yangu punguza mashambulizi yasio na tija kabla haujapoteza mwelekeo.
 
Na hapi ndipo Rais Magufuli alipowakamata ndo maana wanatapatapa...Serikali ilikuwa inapata Kodi kwa ANAYETUMA PESA TU (Swali hapo ni Hiyo 18% alikuwa anatozwa mlaji au kampuni???? )
Lakini yule anayepokea pea iliyokuwa inakatwa na Kampuni ilikuwa haikatwi Kodi. ...Kwa sasa wamebanwa kotekote
Halafu UKAWA wanajifanya kutumia mitandao wakiwemo hawa akina G sam kupotosha!!!!! Haya yana mwisho tunaelewa vizuri sana lengo la Serikali. ..ni suala la muda tu mtajiona wajinga tena weupeeee. ..subilini tu
We yanga kweli! anayekatwa ni Raia siyo kampuni! Kampuni haikatwi chochote hesabu zake bado ziko palepale! Huelewi unachokisema wewe utakwepa kukatwa hela kwasababu wewe siyo ukawa!!
 
Siku zote anayalipa ni mtumiaji wa mwisho. MFANO. Shati kiwandani ni 5000 kodi ni 800 mfanyabiashara biashara atauza 5000 +800+usafiri. Hapo nani atakuwa kalipa kodi?
 
Kweli upinza unawamezesha watu vibaya kuhusu hiyo VAT,ebu rejea taarifa ya habari ya saa mbili usiku channel itv
Kitu ambacho wanashangaza Upinzan ni kuwa HIVI HII KODI JUU YA MIAMALA YA FEDHA IMEANZA LEO KWNY BAJETI HII??,,, JIBU NI KUWA HATA BAJETI YA MWAKA JANA VAT ILIKUWEPO ILA ILIKUWA INAKATWA KWNY KAMPUNI UPANDE MMOJA TU KWA YULE ANAYETUMA PESA...LKN KWA SASA INAKATWA KOTE HATA UPANDE WA KUTOA...MBONA MWAKA JANA UZUSHI HUU HAUKUWEPO?????? Kwan ile VAT alikuwa anakatwa Mlaji (mtuma pesa ????) Ilikuwa inatozwa jw ile pesa ya makato ya kampuni ya kutumia pesa. ...
Yan ukweli ni kwamba Uzushi huu ulioanzia kwa Zito kabwe lengo kuu ni kuleta sintofaham kwny jamii ionekane Upinzani uliposusia bunge basi bajeti ilutopitishwa haifai ina mapungufu mengi kitu ambacho si kweli
Lkn haya yana mwisho Uzushi huu una mwisho tu
 
Hii issue imejadiliwa sana toka asubuhi. Itakuwa kurudia. Angalia uzi unaohusu gavana wa BOT watu wameongea mengi na kutoa elimu ya kutosha. Ukiwa kichwa maji hata nikirudia hapa hautaambulia chochote

Wewe unayejua ndio utoe elimu kumaliza mkakanyiko... Sio kulalamika lalamika hivi. Jibu hoja kwa hoja...sio hoja kwa kioja!
 
Kwa huu upuuzi uliouandika hapa,unakushusha hadhi mkanganyiko kati ya BOT na TRA usingekuwepo kama mbeleni tunge aibika peupe.kwa sababu hatutaaibika,nyie ndio mmeaibika badala yetu
ana hadhi gani huyu kiraza?
 
Hii issue imejadiliwa sana toka asubuhi. Itakuwa kurudia. Angalia uzi unaohusu gavana wa BOT watu wameongea mengi na kutoa elimu ya kutosha. Ukiwa kichwa maji hata nikirudia hapa hautaambulia chochote
Kama ilijadiliwa tulitizamia moderators wange merge uzi au ku delete...
 
Subiri labda wako bize,
Angalia taarifa ya habari, kamishna wa kodi za ndani pia kaelezea vizuri tofauti na mkanganyiko aliousababisha jana Kamishna Kidata.

Alichosema Gavana wa BoT na anachosema huyu kamishna wa kodi za ndani ndicho sahihi kuhusiana na miamala ya benki na simu.

Hakuna double taxation kama anavyosema G Sam. Kilichopo mlaji wa mwisho/ mtumiaji wa huduma ndo ataumia na hii kodi maana mabenki na makampuni ya simu yataoongeza gharama kwa 18% ili yakusanye kodi ya Serikali.

Take care

Hoja kama hizi ndio tunazotaka.. Sio majibu ya Calabash
 
Mkuu inachosha na kukera kurudia rudia kitu kilekile, halafu mtu anaanzisha uzi wa kupotosha.

Poa mkuu, nimeamua kuelezea kidogo baada ya kuona uko interested kujua uhalisia na si ushabiki.

Mkuu, hapa wananchi wa kawaida tutaisoma namba.
 
Subiri labda wako bize,
Angalia taarifa ya habari, kamishna wa kodi za ndani pia kaelezea vizuri tofauti na mkanganyiko aliousababisha jana Kamishna Kidata.

Alichosema Gavana wa BoT na anachosema huyu kamishna wa kodi za ndani ndicho sahihi kuhusiana na miamala ya benki na simu.

Hakuna double taxation kama anavyosema G Sam. Kilichopo mlaji wa mwisho/ mtumiaji wa huduma ndo ataumia na hii kodi maana mabenki na makampuni ya simu yataoongeza gharama kwa 18% ili yakusanye kodi ya Serikali.

Take care
Kituo gani mkuu kimetoa hii taarifa ili nifuatulie marudio ya hiyo taarifa ya habari?
 
Subiri labda wako bize,
Angalia taarifa ya habari, kamishna wa kodi za ndani pia kaelezea vizuri tofauti na mkanganyiko aliousababisha jana Kamishna Kidata.

Alichosema Gavana wa BoT na anachosema huyu kamishna wa kodi za ndani ndicho sahihi kuhusiana na miamala ya benki na simu.

Hakuna double taxation kama anavyosema G Sam. Kilichopo mlaji wa mwisho/ mtumiaji wa huduma ndo ataumia na hii kodi maana mabenki na makampuni ya simu yataoongeza gharama kwa 18% ili yakusanye kodi ya Serikali.

Take care
Alafu hivi finance bill iliyopitishwa na bunge ilikuwa na kipengele kinachoelekeza moja kwa moja kuwa hiyo VAT yatozwe mabenki na siyo mteja?

Kwa definition halisi ya VAT sheria hii itakuwa sahihi kutumika?
 
Ukweli ni kwamba kile unachoambiwa changanya na akili zako,msitake kuleta mapenzi ya vyama kweny utendaji na ufuatiliaji wa kodi,kulipa kodi ni lazima na sio hiary nenda uendako
 
Kalata ya Mwisho ya UKAWA ipo kwenye suala la VAT. Wamesahau kuwa sheria ya kodi imeshapitishwa na sasa ni utekelezaji tu. wanaumia sana kwani serikali ikikusanya fedha nyingi maana yake ni kwamba itaweza kufanya mambo mengi kwa manufaa ya taifa kitu ambacho wao hawataki
 
Kitu ambacho wanashangaza Upinzan ni kuwa HIVI HII KODI JUU YA MIAMALA YA FEDHA IMEANZA LEO KWNY BAJETI HII??,,, JIBU NI KUWA HATA BAJETI YA MWAKA JANA VAT ILIKUWEPO ILA ILIKUWA INAKATWA KWNY KAMPUNI UPANDE MMOJA TU KWA YULE ANAYETUMA PESA...LKN KWA SASA INAKATWA KOTE HATA UPANDE WA KUTOA...MBONA MWAKA JANA UZUSHI HUU HAUKUWEPO?????? Kwan ile VAT alikuwa anakatwa Mlaji (mtuma pesa ????) Ilikuwa inatozwa jw ile pesa ya makato ya kampuni ya kutumia pesa. ...
Yan ukweli ni kwamba Uzushi huu ulioanzia kwa Zito kabwe lengo kuu ni kuleta sintofaham kwny jamii ionekane Upinzani uliposusia bunge basi bajeti ilutopitishwa haifai ina mapungufu mengi kitu ambacho si kweli
Lkn haya yana mwisho Uzushi huu una mwisho tu
Inawezekana kuna sehemu pametokea mgongano wa ufafanuzi wa hii kodi kwenye miamala ya simu na bank...bank wanasema 18% itozwe kwa mtumiaji wa huduma, ambapo ndivyo inavyokuwa, tra wanasema itozwe kwa mtoa huduma kwenye zile gharama anazotozwa mteja na mtoa huduma. Nionavyo mimi mtozaji kodi, tra, aliona kuna sehemu mtoa huduma anatakiwa kulipa kodi akasahau akaiita kodi hiyo vat...hapo moja kwa moja mzigo ataubeba mteja! Kama lengo la serikali ni kumpunguzia ugumu wa maisha mtanzania masikini anayetumia sana huduma hizi za kifedha huku wakikusanya kodi kwa ufanisi, wakae tena chini na kuangalia jinsi ya kufanya, lakini kuiita vat ni kupeleka kilio kwa watanzania masikini walio wengi.
 
Back
Top Bottom