G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,593
- 36,012
Kweli hii sasa ni kama vile tupo gizani. Tena tumepangiwa mambo kwa juu juu sana bila hata waheshimiwa sana na watukufu wetu kutilia maanani mzigo huo wanaomtwisha mtanzania wa kawaida.
Naishukuru sana Jamii Forum kwani ndilo jukwaa pekee Tanzania tunalotumia kuijadili bajeti kwa uhuru (kwa dhati kabisa tutawaunga mkono kwa kila hali na mali)
Katika pitapita yangu kwenye bajeti nimekutana tena na hii kodi ambayo mpokeaji wa hela kwa njia ya simu (Airtel money, M-Pesa tigo pesa n.k) atakatwa kodi ambayo ni ile tozo ya kodi iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T
Sasa kinacholeta mkanganyiko ni kuwa hiyo hela aliyopokea huyo mpokeaji tayari imekatwa kodi kama hiyo yaani ile iliyopendekezwa jumlisha na hiyo 18% wanayoita V.A.T wakati mtumaji akituma.Kifupi hapa tunafanya double taxation! Huu ni wizi wa makusudi kabisa. Mtumaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela na mpokeaji atakatwa kodi kwenye hiyohiyo hela! Kweli tumefikia huko?
Nimeenda mbali zaidi na kilichonichekesha zaidi ni sababu za waziri Mpango za kukata hiyo kodi namnukuu "Makampuni ya simu yanafanya ujanja kuhamisha taarifa za kutuma pesa kwa wanaopokea pesa kwa njia ya simu hivyo kuikosesha serikali mapato. Hivyo kwa kutumia njia hii ya kutoza kodi kwa mpokeaji na mtumaji tutadhibiti mianya ya ukwepaji kodi"
Very interesting!
Kama kweli serikali inatoa sababu kama hiyo, kwanini hiyo kodi ya mwanzo haikugawanywa mara mbili ili kutokumbana mlalahoi? Wangeigawanya kodi hiyo moja mara mbili (nusu kwa nusu) wahamishie kwa mtumaji na nyingine kwa mpokeaji ama lah wangetafuta soft ware inayoweza kukabiliana na tatizo hilo la kuhamisha taarifa kitu ambacho ni rahisi sana!
Na hiyo V.A.T inayotozwa kwenye miamala ya simu ni nini maana yake? Kwanini wakaiita V.A.T?