Joseph Tunu
Member
- Apr 8, 2016
- 55
- 14
Hivi ndivyo inavyoweza kusemwa maana habari za ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka kuhusu Chuo cha Ufundi Arusha zimeripotiwa Serikalini mara kwa mara.
Ni dhahiri kwamba licha ya kashifa nyingi za ufisadi uliofanywa na kuendelea kufanywa na Menejimenti ya Chuo cha Ufundi Arusha hakuna hatua zozote zilizochukuliwa au zinazopangwa kuchukuliwa ili kutatua kero hiyo. Hii ni kero kubwa kwani licha ya kuliingizia Taifa hasara, Ustawi wa chuo unazidi kudorora siku hadi siku.
Menejimenti inayolaumiwa na kulalamikiwa kwa kujichotea fedha za umma bila kujali imekataa kuwajibika walao kupisha uchunguzi. Pia mamlaka za juu zimeshindwa kuchukua hatua zozote baada ya tetesi kusambaa kwamba majipu hayo yamejiimarisha sana na mfumo wa Serikali ya JPM.
Moja ya walalamikiwa hao alisikika akijitapa kwamba “ukiwa mtu wa mfumo hupati shida hata siku moja. Tumepiga mahela ya nguvu hapa lakini TAKUKURU wanatuamkia Shikamoo, hao bwana wadogo watapiga kelele tu”. Mkuu wa Chuo pale, ukienda ofisini kwake ana picha alizopiga na mheshimiwa Rais, unafanya mchezo, alisikika akijigamba mlalamikiwa huyo.
Mlalamikiwa huyo aliendelea kusema kwamba “ukiona watu wakitangaza kwenye vyombo vya habari wametumbua majipu elewa wana chuki bifafsi bradha, hakuna cha majipu wala nini” Unategemea mtu mwenye mtandao kama Masika atumbuliwe? Aliuliza bosi huyo anayependa sana kuitwa bosi.