Jipatie Nakala yako: Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania by Nyerere

Mlenge

R I P
Oct 31, 2006
2,125
2,291
Natafuta kitabu kilichoandikwa na J.K. Nyerere, "Uongozi wetu na Hatima ya Tanzania" kwa Kiswahili au Kiingereza.

Jitihada za kukipata mitaa ya Dar zilishindikana baada ya kuambiwa 'udaku' kwamba kimepigwa marufuku kinamna. Madukani mwa vitabu mwote nilimopita kukiulizia waliniona juha, kana kwamba 'kila mtu anajua' kitabu kilipigwa marufuku.

Madai hayo ni ya kweli au uzushi tu wa uchaguzi?

Shida yangu ni nakala moja tu ya kitabu hicho kwa ajili ya rejea ya kitaaluma.

Natanguliza shukrani.

Amazon.com: Mlenge Fanuel Mgendi: Books, Biography, Blog, Audiobooks, Kindle

=============
UPDATE by JF Admin:


Kwa msaada wa mkuu SubiriJibu kitabu kimepatikana, nakala inaweza kupatikana chini hapa
 

Attachments

  • UONGOZI WETU NA HATMA YA TANZANIA.doc
    161.5 KB · Views: 3,999
Wasiliana na MM Mwanakijiji atakuwa hakikosi kwenye makabrasha yake.
 
Wasiliana na MM Mwanakijiji atakuwa hakikosi kwenye makabrasha yake.

Inawezekana MKJJ anacho kweli coz nakumbuka alikuwa akitoa reference mara nyingi tu wakati ule akirusha matangazo yake live,mapambano ua ufisadi yakiwa yamepamba moto na kashfa zikiibuka mfululizo wengi wetu tukidhani ni masimulizi kama ya filamu za kimagharibi.

Hata hivyo pointi nyingine hapo ni if its true kuwa kimepigwa marufuku,ama ni majungu?Coz jamaa anasema akipatikani kabisa madukani na kwamba wanamshangaa anapokiulizia.
 
MM Mwanakijiji Please kama unahizo nakala za kitabu tuuzie Mkuu, mie pia nimekitafuta sana bila mafanikio.Akhsante
 
Siwezi kushangaa kupigwa marufuku kitabu hiki ukizingatia hasa kuwa watu wenye influence waliobaki ndio hao kina Ali Mwinyi. Hiki ni kitabu kilichosusiwa na wachapishaji wote wa Tanzania wakati ule ikalazimika kukichapia Zimbabwe.
 
Mlenge,
Kama uko DSM ningekushauri umtafute Walter Bgoya. Yeye alichapisha kitabu cha Mtei. Kama walivyosema waungwana hapo awali, kitabu cha Mwalimu kilichapishwa Zimbabwe baada ya kufanyiwa mizengwe na wenye madaraka kisichapishwe DSM. Ninavyo vyote vya Kiswahili na Kiingereza lakini bahati mbaya niko mbali ya DSM.
 
Mkuu ukipata nitumie na mimi, tukiweke scribd, kila mtu aweze kukisoma
 
Jaribu ofisi za Mwalimu Nyerere Foundation bila shaka wanaweza wakawanacho maana wakati wa Kumbukumbu ya Miaka 10 ya kifo cha Mwalimu walikiuza pale Karimjee hall.
 
Mwenzenu mmeniacha kidogo. Hiki kitabu kilikuwa kinahusu nini mpaka kipigwe marufuku? Hebu nisaidieni nipate angalau ufahamu kidogo.
 
Mwenzenu mmeniacha kidogo. Hiki kitabu kilikuwa kinahusu nini mpaka kipigwe marufuku? Hebu nisaidieni nipate angalau ufahamu kidogo.

Nadhani kilitabiri haya yanayo onekana kutaka kutokea wakati huu,conclusion yake haiwafurahishi kabisa viongozi waliopo sasa kwasababu kilitabiri anguko lao.
Kama sijakosea kiligusia mambo ya tatizo la ccm kuwa kama kansa ambayo kuitibu ni lazima ukate na kuifutilia mbali infected part.
 
Mlenge,

Better go to the JK foundation, ukikosa hapo inabidi ununue online, ukipata niambi maana nakitafuta sana pamoja na History of Tanganyika. Naweza jua msingi wa udanganyika wetu
 
Si unajua tena? Nyerere na theory zake zinapigwa chini na viongozi wetu walio wengi in practice. Sawa na mchungaji au shekh kusemea sana ubaya wa kuua binadamu mwenzio na ulevi na uzinzi wakati wasikikizaji wake walio wengi ndio maisha yao ya kila siku, hatapata mashabiki wengi katika wasikilizaji hao.

Kama ingewezekana, Azimio la Arusha, maadili ya viongozi, Ujamaa ..... watawala wetu wangependa maneno hayo yaondoke hata kwenye kamusi.
 
mi naona wengi tu tunakihitaji - akikiweka hapa tu download itakuwa ametusaidia sana, MM plse! wengi wetu kununua online inakuwa tatizo kidogo.
 
Please, tunaomba mwenye nacho atusaidie akiwekea hapa in down-loadable form ili tuweze kukidownload. Please do that for us. I will appreciate very much.

Inasikitisha na inauma sana jinsi vingozi wetu wanavyojifanya vipofu kwa ukwel, wanajali masilhi binafsi bila kujali dhamana waliyopewa na jamii ya kuitumikia. Ukijaribu kusema ukweli kama wewe sio sombody unaweza ukafichwa kusikiojulikana na kama wewe unajina kubwa basi kazi yako ndo kama hivyo inafichwa.

Mungu Atusamehe.
 
Sidhani kama kwa mtindo wa kudownload,wenye kutunga vitabu watakuja fanikiwa katika mauzo,tujenge utamaduni wa kununua ili kuwasaidia kurudisha walau senti chache walizotumia.Mimi hicho kitabu ninacho na niko dar.Ukiweza tuwasiliane kwa PM nikupatie utumie halafu utanirudishia.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom