Jipatie nakala ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka 5 wa Kikwete

Mwanakijiji Thanks for the Document, FYDP.

Nimeuona kwa ufupi bado naendelea kuusoma, kwa jinsi nilivyouona ni mzuri sana nampa hongera Mh Rais kwa kuona hilo. Swali la msingi ni "wataweza kuutekeleza?" Maana system nyingi serikalini ziko very Corrupted kila mtu anachukua anavyoweza.

Watu wakuutekeleza naona kama ni wachache, inabidi serikali ifanye maamuzi magumu kuutekeleza kwani kwa watumishi hao hao nachelea kumwambia JK na serikali kuwa itakuwa ngumu.
 
Nimeupitia huu mpango and unlike wale walioupongeza; ni miongoni mwa mipango ya ajabu kabisa kubuniwa na watu wenye akili timamu!
 
Mdau mwingine katolea maoni mpango huo hivi:

mose said:
Assalaam aleykum kaka MM...

Nimeipitia hii rasimu; kama dakika chache zilizopita na nimeiona ilivyoni taarifa zaidi kuliko ile chachu halisia ihitajikayo kwa watu kuamka na kujituma ili kuleta mabadiliko ya kiuchumi na ustawi na basi maendeleo.

Matunda mengine ya siasa na utendaji wake... Imeandikwa kwa kiingereza lakini kwa kweli ni mambo lege lege ikiwa yatazungumzwa kwa kiswahili na hivi hata kwa wenye kuzungumza kiingereza wangalisema hiyo rasimu ya kuwa-- 'it is so verbose...'.

Ni tatizo lile la kule kufikirika/kudhanika kuleta mabadiliko na maendeleo kutoka nje... Na mengi yanadhaniwa humo kusema ukweli hayatawezekana ila tu kuambulia uchache wa asilimia katika ufanisi wa matekelezo; halafu watahitaji kukamisheni visomo vingine na rasimu zingine... Kama kawaida ya ofisi hizi za umma--hata hivyo si ndiyo kazi yao? Watajitetea... Tume ya Mipango ya Rais. Rasimu yenyewe ni kazi rahisi ambayo hata mwanafunzi wa kawaida wa elimu ya juu anaweza kuandika ikiwa upatikanaji wa rasilimali na vitendea kazi fulani utarahisishwa kumfikia--taarifa tu; basi ni vipande vipande toka huku na kule halafu kukata mafungu ya maneno toka huku na kule na kisha kuyaunganisha katika 'Rasimu ya Mpango wa miaka mitano wa Maendeleo Tanzania'....

Japo miye ni mtetezi wa visomo na ninasema bayana kwa zama hii Kujifunza ndiyo tendo takatifu kabisa na lenye kheri; na hii ni zama ambayo ibada ya mtu ni katika kutafuta kuelimika ilivyo ni sahihi na kuishi kwa neema ya kheri ya elimu na ufunuo wake binafsi; lakini si kimtindo huu... Watu wachache kutengenezewa mkondo wa taarifa na visomo vyenye kunasibu mipango kwa wengi waliosalia ni shughuli kimeo kwa nafasi ya kujitegemea... Maamuzi yao na utashi vyaweza kuwa ni vifungo zaidi kwa wale wasioshtukia kutoshiriki/shirikishwa katika michakato ya maendeleo thabiti--na hivi hata hichi kinachozungumzwa ni 'Uwazi' na 'Ukweli' ingalipasa kisije kwa hisani ya viongozi wa serikali ila tu kuwa ni shughuli ya moja kwa moja ya elimu sahihi inayosogezwa kwa raia wote; na wao watakuwa na utambuzi kwa mikingamo yao kwa wakati na kuwajibika na mabadiliko wayatakao... Na hivi hadi sasa, hata mipango iliyokuwemo katika rasimu hii tayari inatengeneza mazingira ya michongo kwa wajanja wengi walio ndani na hata nje ya serikali kabla hata ya yule raia aliyetengwa mbali... Shilingi yaua tena maua.

Rasimu hii itameremeteshwa kwa mafungu ya fedha na migawo yake mbalimbali katika kuratibu utekelezaji wake... Haya ni maua; na wengi watavutiwa na mbolea hii ya kiutekelezaji--Kuachia juu nguvu iliyolala ya Kukua ya Tanzania; kama kisemavyo kichwa kidogo cha rasimu hii... Je, kukua huku kutaleta msimamo upi wa sekta mbalimbali za kibiashara kama vile inavyoonesha kwa sasa-- Mawasiliano yanaongoza, halafu ujenzi , umeme na gesi, kujiingiza kwa vyombo vya kifedha na halafu kufuatiwa na mengine?

Kwa kuwa ili kuwepo kwa fanaka sawa kwa watu wote, sehemu ya limbikizo la faida la vyombo vikuu kifedha haina budi kuyeyuka... Rasimu yenyewe inatambua kuwepo kwa matatizo ya upatikaji wa mitaji katika vyombo vya fedha vya ndani kwa watu wenye uhitaji... Hili kwangu si tatizo sugu tu; bali ni tatizo la kimaadili juu ya falsafa nzima ya mitaji na faida... Wabunifu wa mipango ya kifedha wanaweza kujikakamua sana katika kujitahidi kutengeneza mikakati ya kifedha lakini kwa bahati mbaya msingi wa jitihada zao ni falsafa lemavu za biashara, hesabu na dhana za mapato, makusanyo na kodi.

Sasa rasimu inaonesha shughuli zinazochangia pato ghafi la taifa ni pamoja na zile shughuli za biashara za mizigo na ukarabati, Kilimo, Viwanda na biashara/huduma ya Nyumba na mashamba... Kwangu miye shughuli halisi zinasohesabia uchumi 'wenye afya' ni Viwanda na huduma/Afya... Kwenye afya ninamaanisha huduma zote ambazo binadamu hujikuta kuhitaji--kujumlisha starehe na faraja za kila siku... Kwenye viwanda nina maanisha uzalishaji wa bidhaa zote muhimu na za lazima ndani ya jamii ya uchumi mmoja husika. Japo hakuna nchi yeyote itayomudu kujitegemea kwa 100%; lakini vipo vitu vya msingi ni lazima kila jamii/jumuiya ya dola haina budi kujimudu yenyewe.

Aghalabu Korea ya Kaskazini waliwahi kuwa na dhana ya 'Juche'... Kim II Sung alibuni tasnifu nzuri kabisa ya Juche japo na yeye alikuwa mtu mwenye moyo mwepesi kwa kushobekea utukufu wa duniani... Ni mapinduzi ya mfano sana aliyoanza nayo rais wa zamani wa Korea kwa kusisitiza kuhifadhi mila, desturi, mawazo wa watu wa Korea na kuhimiza kuachana na fikra za kuazima kutoka nje(nchi za kisovieti, kwa wao) na kusimamisha nguzo ya Juche katika kuelekeza sera zote za nchi... Hii ilikuwa na maana ya kuunda taifa lenye kuja kujitegemea kwa mapana yote ikiwemo kiulinzi na usalama... Na kusisitiza watu watengenezewe mazingira ya kupenda taifa lao na nchi yao mama... Kukazia elimu na historia ili kuvuvia mapinduzi na fahari mpya.

Miye ningependa tuanzishe mapinduzi kama ya Kim II Sung lakini tuepuke ule ushamba kushobokea jina/umaarufu... Tunaweza kufanya hivi ikiwa ubunifu wetu utaweza kuwa katika kanuni na si itikadi tupu. Kwa kuwa hakuna mtu mwenye hati milki inapofika kwenye kanuni... Kwa kuwa Sheria ya Kweli si neno la mwanadamu, na kanuni ya kweli ni mwili wa madhahirisho kwa hiyo Kweli--basi sifa na utukufu si stahiki ya mwanadamu yoyote ila kile Chenye kujalia yote Fahari yake ya kuwa Kweli Pekee.

Tukijua kanuni tutaachana na 'fiscal and monetary policies' za leo maana zote ni fikra za kufikia tu. Ukuaji unaotengenezea hata hicho kichwa kidogo cha rasimu utapata sura mpya na si 'Ukuaji' tu usiojulikana mwanzo na mwisho wake...

Wafikirifu, watendaji na viongozi wa leo wanaweza kuhangaika kubuni mengi ya 'kuuza' kwa raia lakini kumbe wangalijua kanuni za mambo wasingalihitaji kujaribu mbinu zile zile zinazosuasua katika kutafuta suluhu za kudumaa kwa ustawi wa watu na maendeleo.

Tunalohitaji katika kufumua na kusuka taasisi mpya--na rasimu hiyo ina mengi inayochukulia kuwa poa na hali siyo poa.... Kwa mfano haioneshi dalili ya kung'amua vikomo vya kiitikadi vilivyoshindwa katika kufafanua harakati za kisiasa na uchumi kama vile kwa nini Azimio la Arusha limeshindikana na halitekelezeki... Japo rasimu hiyo inazungumza kwa muhtasari historia ya jitihada za namna hiyo kutoka siku za uhuru, Azimio la Arusha, matatizo makubwa ya kiuchumi mwanzoni mwa miaka ya 80, jitihada za marekebisho ya kiuchumi na tena hadi dira ya taifa 2025 na mwanzo wa mchakato wake mwishoni mwa miaka ya tisini. Kwa kuna dimensha ya utu na makusudio yenye kuharibika upesi katika mioyo ya watu--kuleta namna ya mashauri mengine ya 'kiroho'. Na basi rasimu hii inajitetea kuwa ni sehemu ya kuboresha dira ya Taifa ya Maendeleo ya taifa 2025; na picha ya yale yaliyotazamiwa kwa kupangwa--kwa mtingo wa mawazo uliosogea...

Kiufundi siwezi kuikosoa rasimu hii kwa kuwa mtingo wa kusimama kwa mawazo wake ni tofauti na mlengo wa mtingo wangu wa mawazo. Ufikirifu wangu ni tofauti kuanzia kwenye mipango ya fedha ya mwaka kwa mwaka na sera za fedha-- mule hutajwa kama 'fiscal and monetary policies'... Kuna mengi yanazungumziwa humo kutoka kwenye kuongeza idadi ya wataalamu na watumishi mpaka kupanua idadi ya wasomi kutoka vyuo vya elimu ya juu... kwa mfano kuna hitaji la kuzalisha/kuwapata wahitimu kwa takriban ya kasi 80,000 kwa mwaka kufikia mwaka 2015 na wakati hapa tulipo tunatoa wahitimu 40,000... Halafu suala la viwanda linazungumziwa sambamba na lile la maji, ardhi na nishati...

Nikiwa kama mtu niliye na mawazo ya kipekee juu ya muundo mzima wa kiuchumi-jamii; ninamtazamo tofauti na mikakati ya uchumi wa fedha... Miye ninashikilia picha ya uchumi wa kazi... Kwa hiyo sioni fedha na mipango kama ndiyo fimbo ya mnyonge kama ilivyo kwa taifa la watanzania na watu wake. Nina mawazo tofauti na wafikirifu wa uchumi kama Keynes na dhana zao kufafanua 'Zao Ghafi la Ndani la Taifa', GDP, katika kule kuhusiana na 'Mlinganisho wa Malipo', Balance of Payment, ambavyo ndiyo hudadavua msimamo wa uimara wa sarafu ya nchi kutokana na tathmini ya Uagiziaji na Usafirishaji Nje wa bidhaa na Huduma... Tunapotoshwa mno na dhana batili ya 'Uchumi wa bidhaa' wa Dunia... Miye nimesanifu usanisi wa Ujasiriamali wa kijamii... NI mwelekeo tofauti na Uchumi wa kileo wa kifedha... Kwa kuwa humo ndani yake ninaifafanua upya dhana ya fedha, kazi, huduma na bidhaa na kupendekeza sera mpya za fedha...

Rasimu inazungumzia kuzidia mbali namna ile ya mipango ya hatua fupi fupi ya programu zilizo za msingi-hitaji, need-based SAP zilizokuja na jitihada za marekebisho ya uchumi ya miaka ya 80 ya kati--kwa kusema programu hizi hujibana na kiasi cha rasilimali zilizopo(fedha?) na kudai fedha isiwe mwisho ila namna ya kufikia ule mwisho[1.2.1. The 15 Year Roadmap]... na basi jitihada zake zipo katika kutambua fursa na mianya ya maendeleo lakini kuangukia kwenye saga ile ile ya mikato ya kiushindani na fursa linganishi zijazo na unafasi wa kibiashara wa nchi kijiografia(kukaba penati ya fedha tena?) Ikiwa hatuna viwanda vyetu sisi wenyewe, bado hata fursa zote hizo zitakuwa vumbi linaloweza kupeperushwa na upepo... Ikiwa hatuzungumzi nafasi ya ubunifu na uvumbuzi tena hasa kutekeleza muktadha wake, uchumi wote huu unatazimiwa si kitu ila 'puto'... Ikiwa hatuoni elimu yetu inabidi kutengenezewa taasisi zenye nidhamu tofauti na leo ya 'soma umalize'--tunajiloga hata kwa visomo vyetu sisi wenyewe...

Katika Usanisi ninazungumza haya ya fedha kuwa 'fimbo' isivyo 'mpango mzima'; pia ninaonesha mara moja ni shughuli gani inaweza kuhamasisha watu kujishughulisha na mpango wowote wa maendeleo kwa kugusia umuhimu wa kuboresha shughuli za makazi, umiliki wa mali na ardhi. Rasimu nayo inazungumzia kizungumkuti juu ya mengi--utungwaji wa sheria za ardhi, milki na mchango wake katika kujenga sura thabiti ya matumizi ya kiuchumi na ustawi... Ambacho ninaona kama wanakipa umakini haba ni mchakato mzima wa kumhamasisha mtu atambue heshima yake kwa mali/ardhi anayoweza kujipatia na kumilikishwa na mmiliki mkuu aliye ni Rais kwa dhamana kuu ya dola... Hapa kwangu ni jambo lisilo jepesi hata kidogo... Na ujinga uliokatika raia wengi wasio zinduka kutafuta haki zao na stahiki zao utaponza mikakati ya serikali kuonekana ikitekelezeka kwa kasi ndogo... Mhimili wa Sheria na Mahakama una mapungufu mengi ya kibinadamu... Mkukuta na Mkurabita ni mipango iliyodorora ama kustawi kwa kasi iliyopooza; na ishara ya wazi kuwa shughuli ya kurasimisha rasilimali za wanyonge, kubuni vyombo vinavyotambulika katika michakato ya kitaasisi siyo makisio ya kiporojo za rasimu na mipango ya kwenye makabarasha... Haki ni shauri nyeti sana; pasipo kufanyika kwa misukumo ya haki taifa lolote haliwezi kubarikika hata iwe vipi...

Kujenga taasisi katika jamii yeyote ni shughuli yenye kuhitaji 'kina' fulani katika kumea ndani ya akili na mioyo ya wahusika. Ikiwa jitihada sahihi haitaeleweka katika kubuni vyombo na mipangilio ya shughuli zake zenye kurudiwa rudiwa kivitendo na urasmi wa sura/mfumo, ilivyo ni tafsiri rahisi ya taasisi-- taasisi madhubuti ni uwezekano wa kusuasua daima! Na mimi kwa kulielewa hili ndiyo maana imenipasa kujichimba na kuchimba hata imani, dini na mapokeo mbalimbali juu ya tamaduni za watu... Sasa usitegemee hili kudadavuliwa katika rasimu ya kiserikali, serikali itazungumza tumeunda taasisi za kuzuia rushwa(utafikiri rushwa inaweza kukomeshwa kwa vyombo vya mtindo huu!) na kuimarisha demokrasia ya vyama vingi--tumeimarisha mbanano wa pamoja wa watu kisiasa na hivi kutengeneza mazingira mazuri ya serikali kutekeleza majukumu yako--haya utayakuta humo kwenye hiyo rasimu--hawawezi kusahau karata zao dume... Lakini ndiyo maana serikali hizi zinawezakubuni mipango kadhaa kuburudisha fikra za watu na kuakisi ufikirifu fulani wa wasomi wake na kumbe bado ni kule kujua na kutambua ukweli wa mambo kwa sehemu.

Hitaji kuu ni kupisha nje mtingo wa kimawazo uliompya na usivyolazima kufungamana na lugha ya mipangilio ya kizamani ya kuzungumza na kujua mambo yake... Naam yote tu, kuanzia siasa, uchumi, jamii na utamaduni wote kwa ujumla. Na hili huja kwa mchango wa mtu mmoja mmoja na halafu harambee...

Tuthubutu kufikri vinginevyo na itakuwa sawa na hata zaidi.

Tutamulika haya zaidi na kwa kina zaidi, insh'llah

 
Msaada tutani: Mwanakijiji unaweza kutusaidia kupata waraka ya "Sanifu Usanisi wa Ujasiriamali wa Kijamii" iliyofanywa au aandikwa na huyo bwana Mose. Natanguliza shukrani zangu. Naendelea kuusoma FYDP.
 
Msaada tutani: Mwanakijiji unaweza kutusaidia kupata waraka ya "Sanifu Usanisi wa Ujasiriamali wa Kijamii" iliyofanywa au aandikwa na huyo bwana Mose. Natanguliza shukrani zangu. Naendelea kuusoma FYDP.

yupo humu unaweza kumtumia PM atakujibu tu; he is a gentle soul.
 
Back
Top Bottom