TTCL Corporation: Support thread (Maswali, ushauri na malalamiko)

Huu mtandao ni shida nimenunua laini juzi kwenye taarifa za usajili kunatokea jina langu kwenye TPesa linatokea jina la mtu mwengine.Nawaambia hawana jibu nazungushwa tu.Nasubiria wiki hii ikiisha tu sijapatiwa ufumbuzi jambo langu najitoa kutumia laini yenu narudi halo.

Njoo inbox mkuu
 
Asante kwa kuwasiliana nasi.
Ndugu mbongopopo, inategemea unahitaji WiFi ya aina ipi?
Maana tuna
1. Dongle hii moden ya kawaida Tsh 50,000/= inatumia mtu mmoja tu.

2. Wingle Tsh 75,000/= inatoa wifi kwa watu 10.

3. Mifi Tsh 110,000/= inatoa wifi kwa watu 10.

4. Router Tsh 150,000/= inatoa wifi kwa watu 32.

Karibu sana.

#RudiNyumbaniKumenoga.
nn tofaiti ya Wingle na Mifi naona zote zinatoa 10 user ?
 
1. Mageuzi tunayoyaona hivi sasa kwenye matumizi ya mifumo ya kidigitali na kielektronik nchini yanatokana na uwepo wa miundombinu bora ya mawasiliano kutoka TTCL Corporation. Tunajivunia mafanikio haya.

2. TTCL Corporation imetoa mchango mkubwa katika kuchangia ukuaji wa sekta mbalimbali za maendeleo nchini. Hivi sasa tumefanikiwa kutoa huduma za mawasiliano kwa Vyuo Vikuu vya Elimu ya juu, Ofisi za Mabalozi, Taasisi za dini, Makampuni, Wateja wa Nje ya Tanzania, Mabenki, Taasisi za fedha, Taasisi za Serikali nk.

3. Ni lazima tujivunie mafanikio haya, tumeimarisha huduma zetu za simu za mkononi kwa kutumia teknolojia ya 2G, 3G na 4G nchi nzima ili kuhakikisha ubora wa huduma ya Intaneti na Sauti zinapatikana muda wote. Na tunaendelea kuboresha zaidi ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu. Mageuzi yanaendelea

4. Hii ni hatua kubwa zaidi katika kuongeza mvuto kwa wateja wetu, tumefanya mageuzi makubwa katika kuongeza mvuto wa Maduka yetu ya Huduma kwa Wateja ili kutoa wigo kwa wateja wetu kufurahia huduma zetu kwenye mandhari mazuri. Tembelea maduka yetu upate huduma bora na nzuri kutoka kwa wahudumu wenye weledi na bashasha wakati wote.

5. Tunawashukuru sana wateja wote mliojiunga na mtandao wetu wa TTCL Corporation, tunajivunia sana kuwa nanyi. Tunawahakikishia tutaendelea kutoa huduma bora na zenye kiwango ili kuongeza chachu katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa letu.

Asanteni kwa kutuunga Mkono.
6. Tumeongeza mawakala wa kuuza Vocha za Muda wa maongezi kupitia mawakala wakubwa na wadogo. Pia tumeimarisha upatikanaji wa Vocha kupitia njia za kielektroniki ili kukidhi mahitaji ya wateja wetu, hivi sasa unaweza nunua muda wa maongezi kupitia T-PESA, Mawakala wa Selcom, Mawakala wa Mobistock, Mawakala CRDB na NMB, kupitia mitandao mingine ya Simu, Wakala wa TPB, Cellulant nk

7. TTCL Corporation tuna haki ya kujivunia, tumeimarisha biashara, tumeboresha njia za mawasiliano na tumeongeza uwajibikaji ndani ya Shirika ambapo juhudi zimeleta mafanikio makubwa kwa kutoa GAWIO kiasi cha Shilingi Bilion 3.6/- (TZS) kwa serikali kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019.

8. TTCL Corporation tumeshirikina kikamilifu katika kuhakikisha tunapeleka mawasiliano katika maeneo yote ambayo miradi ya ujenzi wa viwanda unaendelea nchini, tumepeleka mifumo ya mawasiliano yenye ubora ili kutoa fursa kwa wawekezaji katika sekta ya Viwanda kuwa na mazingira Rafiki ya mawasiliano. Kwa kushirikiana na Wizara ya Viwanda na Biashara tumepeleka mawasiliano ya Data na Sauti kupitia miundombinu ya TTCL Corporation kwenye Ukanda maalumu wa uwekezaji {Export Processing Zone (EPZ) na Special Economic Zone(SEZ) nchini ili kuchochea maendeleo ya sekta hiyo.

9. Tumegusa kila Miradi mikubwa kwa kuwapa Mawasiliano bora ya Data na Sauti, tunatambua umuhimu wa miradi hii katika ukuaji wa maendeleo ya Taifa letu. Tumeshiriki kikamilifu katika kupeleka mawasiliano ya Data na Sauti katika Bwawa la Kufua Umeme wa Maji la Mwalimu Julius Nyerere.

10. Tumehakikisha Sekta ya Afya inakuwa na miundombinu bora ya mawasiliano, tumeshirikiana na Wizara ya Afya na Taasisi zake katika kuimarisha TIBA MTANDAO ambapo Hospitali kubwa na ndogo nchini zimeungwa kwenye miundombinu ya mawasiliano ya TTCL Corporation ambayo imefanikisha utoaji wa TIBA kupitia mtandao.

Kwanini nyie ndio worse mobile network provider hapa Tanzania?
 
Back
Top Bottom