Jipatie Microsoft Excel template kwa ajili ya biashara

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
284
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
284 250
Jipatie Ms Excel template kwa ajili ya biashara yako kwa Tsh. 25,000/= tu

Ni matumaini yangu kuwa sote ni wazima wa afya, kwa wale ambao hawako sawa, Mungu awatengenezee afya zao warejee katika hali zao za kawaida.

Mimi ni mtaalamu wa Microsoft Excel, huwa natengeneza templates mbali mbali. Leo nimekuja na excel template ambayo inawahusu zaidi wafanyabiashara (wakubwa na wadogo)

Hii template inakuwezesha kurekodi/kutunza mauzo yako yote ya mwezi mzima na kukuwezesha kujua kiasi cha mauzo na faida kilichopatikana katika bidhaa fulani au bidhaa zote katika tarehe husika. (Angalia picha zote hapo chini)

Nimeweka lugha mbili (Kiswahili na English) ili kuwawezesha hata wale wasiojua Kiswahili waweze kuitumia pia. Mtumiaji ataamua mwenyewe atumie lugha gani kati ya hizo.

Mtumiaji atakuwa anajaza sehemu ambazo hazina rangi tu,sehemu zingine zilizobaki zinajazwa na template na pia zipo locked ili mtumiaji asiweze kuharibu formula zilizopo kwa kutojua.

Picha No.1 Hapa ni pale mtumiaji wa template anapotaka kujua mauzo na faida zilizopatikana katika bidhaa flani katika tarehe flani.

Picha No.2 Hapa ni pale mtumiaji anapotaka kujua mauzo na faida zilizopatikana katika bidhaa flani tokea mwezi uanze

Picha No.3 Hapa ni pale mtumiaji anapotaka kujua mauzo na faida zilizopatikana katika bidhaa zote katika tarehe flani.

Picha No 4 Hapa ni pale mtuamiaji anapotaka kujua mauzo na faida zilizopatikana katika bidhaa zote tokea mwezi uanze.

FAIDA ZA TEMPLATE


1. Ni rahisi kuitumia, haiumizi kichwa na pia inaweza kutumika ktk biashara nyingi tu kama vile maduka ya jumla, pharmacy, hardware, supermarket, na hata viwandani. Ina uwezo wa kuchukua record zaidi ya 600 kwa siku

2. Inakuwezesha kujua mapato na faida ya bidhaa husika katika tarehe flani (nimeweka sehemu mbili za ku-search, search by product na search by date ambapo utaweza kuandika bidhaa yako na tarehe unayotaka ili uone record zake)

Bei ya template ni Tsh 25,000/= tu
Malipo ni kabla, template nakutumia baada ya kufanya malipo.

Kama unaihitaji, tuwasiliane kupitia email yangu au PM

Njuka II
Expert in Microsoft Excel
Email: ebusiness.excel@gmail.com
Dar es salaam

19 November 2019, Tuesday

UPDATED


Template tayari imeshakamilika, ina jumla ya worksheet tatu.
Worksheet ya kwanza ni ya stock/purchase ambayo inakuonesha jumla ya stock ulizonunua na stock iliyobaki. Inajiupdate yenyewe, ukiongeza mzigo stock inaongezeka na ukiuza mzigo pia inapungua (angalia picha comment #26)

Worksheet ya pili ni ya mauzo ambapo itakuwezesha kujua kiasi cha mauzo ya bidhaa flani pamoja na faida iliyopatikana

Worksheet ya tatu ni ya MATUMIZI ambayo itakuwezesha kujua kiasi cha matumizi uliyofanya na pia inakuonesha Net profit(faida baada ya kutoa matumizi). Sheet inajiupdate yenyewe, kila unapoingiza matumizi utaona hiyo net profit inavyoshuka. Matumizi yakizidi gross profit,rangi nyekundu inadisplay na kuanzia hapo utakuwa unatumia pesa ya mtaji (hasara/faida unaiona mwenyewe kadri matumizi yako yanavyoongezeka/kupungua) (angalia picha comment #27)
 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
284
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
284 250
Boss hii template inatunza kumbukumbu ya inventory. Let's say nina bidhaa 40 nimeuza 10, ipunguze automatically zibaki 30. Afu nkiuongeza bidhaa let's say 15 iziongeze
Hapana mkuu,hiyo ni case nyingine ambayo naweza kuitengeneza kwa makubaliano. Naweza sheet ya stock records ambayo itakuwa inafanya hayo mahitaji unayoyataka
 

lynch

JF-Expert Member
Joined
Jul 30, 2015
Messages
218
Points
250

lynch

JF-Expert Member
Joined Jul 30, 2015
218 250
Njuka II, Good. mm natak kujua.kama ina uwezo wa ku update stock automatically.kila unapoingiza mzigo mpya.kwa kukuonyesha idad ya mzigo uliongeza na kiasi chake cha faida in return.thn unapatikan wap mkuu tukikutfta
 

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2016
Messages
515
Points
1,000

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Joined Nov 12, 2016
515 1,000
Mkuu nakukubali sana, napenda kazi za kutumia akili nyingi , nguvu kidogo, matokeo makubwa. Hongera sana, na nikutie tu moyo boss,

katika kazi yoyote unayoifanya hata kwa wakati huo huoni matokeo kama ulivyotarajia ila kuna watu wana-appreciate hiyo kazi, usije iacha boss, one day matokeo utayaona, a good example is Jack Ma na ishu yake ya Alibaba, ni suala la muda.
 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
284
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
284 250
Boss hii template inatunza kumbukumbu ya inventory. Let's say nina bidhaa 40 nimeuza 10, ipunguze automatically zibaki 30. Afu nkiuongeza bidhaa let's say 15 iziongeze
Hapana mkuu,hiyo ni case nyingine ambayo naweza kuitengeneza kwa makubaliano mengine. Naweka sheet nyingine ya stock records ambayo itakuwa inafanya hayo mahitaji yote unayoyataka
 

Njuka II

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2019
Messages
284
Points
250

Njuka II

JF-Expert Member
Joined Feb 25, 2019
284 250
Good. mm natak kujua.kama ina uwezo wa ku update stock automatically.kila unapoingiza mzigo mpya.kwa kukuonyesha idad ya mzigo uliongeza na kiasi chake cha faida in return.thn unapatikan wap mkuu tukikutfta
Hii ina sheet moja tu ya kurecord mauzo, kuhusu hayo mahitaji ya kujiupdate stock naweza kutengeneza sheet nyingine ikawa inatoa taarifa za stock, ukiuza stock inapungua na ukiongeza stock pia inaongezeka automatically. Hapa tunaingia makubaliano mengine
 

Forum statistics

Threads 1,367,038
Members 521,607
Posts 33,385,405
Top