Jipatie mbegu ya papai za kisasa (malkia F1)

Watanzania kwa ubishi ingia shambani Fanya kazi...Mapapai yapo aina tatu, jinsia ya kiume, kike na jinsia zote (Hermaphrodite papaya).

HII ANALYSISI INAONYESHA UNAFANYA KAZI YA KILIMO CHA MAPAPAI HIVYO UNAUZOEFU.JE UNAWEZA TUSAIDIA KUJUA FURSA ZA MASOKO, NA MAENEO AMBAPO UNAWEZA KULIMA..mFANO HALI YA HEWA YA NJOBE AU PWANI NI IPI INAFAA ZAIDI..JE UNAUELEWA WA MASOKO YA MAKAMPUNI KAMA JOG , MKIKITA AMABAO WANAJITANGAZA WANAMASOMO MAKUBWA YA PAPAI?
 
Watanzania kwa ubishi ingia shambani Fanya kazi...Mapapai yapo aina tatu, jinsia ya kiume, kike na jinsia zote (Hermaphrodite papaya).

Hata hivyo, aina zote tatu zinategemeana katika uzalishaji.

Mpapai wenye maua ya kiume uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata matunda, ingawa wenye maua ya jinsia zote hujirutubisha wenyewe.

Zipo za aina mbili za mbegu: mbegu za kawaida ambazo huweza kupatikana popote kwenye papai lililoliwa. Changamoto iliyopo ni ugumu wa kubaini mbegu zipi ni za aina gani ya mpapai.

Aina ya pili ya mbegu ni chotara , mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye maua ya kike na ya kiume pamoja. Hii hukua haraka na kutengeneza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile ya kienyeji.

Upandaji

Panda mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na kujazwa robo tatu. Kisha viweke chini ya kivuli umwagilie maji.

Mbegu huchukua siku nane hadi 15 kuchomoza, hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku ila yasiwe maji mengi. Hamisha mche toka kwenye kitalu baada ya wiki ya sita hadi nane.

Hakikisha kazi ya uhamishaji mimea inafanyika wakati wa asubuhi sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.

Wakati wa kuhamishi miche shambani, hakikisha nafasi kati ya mmea na mmea ni mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.

Andaa mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60, tenga udongo wa chini na wa juu kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi.

Unaporudisha udongo kwenye shimo tanguliza udongo uliochanganywa na mbolea ya samadi na juu malizia udongo ulioutoa chini wakati wa kuchimba shimo.

Kwa wale wenye mashamba makubwa, mipapai huingia kati ya miche 1000 hadi 2000 kwa hekari moja. Pia, 400 hadi 800 kwa ekari moja.

Mmea ukishahamia shambani bado kutahitajika matumizi ya mbolea, wiki moja baada ya kuhamishia shambani weka mbolea gramu 28 kila mmche lakini usitumie mbolea yenye Chlorine bali tumia yenye Phosphate, mfano; - 12:24:12. (NPK).

Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano, 20:10:10 (NPK).

Kisha tumia mbolea yenye Potassium kiasi cha gramu 114, baada ya maua na matunda kutokeza. Kisha fanya hivyo kila baada ya mwezi. Mfano wa mbolea hii ni 12:12:17 +2 (NPK).

Weka mbolea ya majani yenye virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mwezi. Boron ni mbolea ya muhimu katika kupata matunda mazuri. Ukifuata utaratibu huu baada ya wiki 37 tangu kupanda mbegu utaanza kufaidi matunda hadi mpapai utakapochoka kuzaa.

Kwa mpapai uliotunzwa vizuri kwa msimu huweza kutoa matunda 80 hadi 120. Ikiwa umepanda mipapai 1000 kwa ekari maana yake utakua na mapapai 96,000 hadi 120,000
Je! Papai ina misimu mingapi ya kuzaa kwa mwaka?
 
  • Papai hizi ni papai za mda mfupi miezi sita tu unavuna, papai hizi ni tamu na nyekundu ndani ina zaa mpaka papai 105,

  • Soko lake ni kubwa sanaa,

  • Eka moja inauwezo wakukupa mpaka milion 100.

Tufanye hesabu kidogo:
1 acre =1000/1200 miche ya papai
kila mti wa mpapai unazaa 105
kila papai ni Tsh 1000 japokua inaweza kuwa zaidi kulingana na ukubwa.

kwahiyo =1000miche X 100papai/mti X 1000Tsh =100,000,000Tsh

Mche Tsh 3500
Mbegu Tsh 30,000 kwa pakti inakuwa na mbegu 70/80


Tuwasiliane:
0752972727
mambo yangekuwa rahisi hivi hakuna mtu angekuwa maskini....
acha kutapeli watu....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom