Jipatie huduma za kilimo kwa gharama nafuu

rommy shabby

JF-Expert Member
Jun 26, 2017
1,121
1,294
DRIP IRRIGATION SYSTEM &GREENHOUSE (KWA GHARAMA NDOGO )
Hii ni njia ya kumwagilia mmea kwa kutumia tone(matone) la maji kwa muda husika, ambapo bomba dogo huundwa kwa kuwekewa matundu madogo madogo kwa kuzingatia mmea ulipo kwaajili ya kuupa maji mmea muda wote.
Umwagiliaji huu unaweza kuendeshwa kwa mashine au kwa mkono. Umwagiliaji huu pia unaweza fanyika kwa mazao yaliyo mengi ikiwemo ya mboga mboga, matunda na hata nafaka. Katika maeneo yaliyo mengi umwagiliaji huu wakulima hupendelea kuufanya kwa mazao ya matunda na mboga mboga.

FAIDA ZA UMWAGILIAJI WA MATONE
1. Matumizi ya maji ni yenye mafanikio.
2. Mavuno ni ya uhakika.
3. Mgawanyo wa maji katika mimea ni sawa.
4. Mmonyoko wa udongo ni mdogo sana.
5. Hupunguza gharama za wasaidizi shambani.
6. Huokoa muda.
VITU VYA KUZINGATIA KABLA YA KUANZA UMWAGILIAJI WA MATONE


1. Topografia Huu ni umwagiliaji wenye mafanikio hakikikisha eneo lako lipo tambarare, hata kama mteremko utawepo uwe mteremko wa wastani, kufanya mgawanyo wa maji kuwa sawa. Pia zingatia sehemu ya kuweka chanzo cha maji inaweza kuwa ni pipa liliwekewa miundo mbinu mizuri miundombinu hiyo kama bomba zilizo sanifiwa vyema kufikia kwenye mmea, pipa au chanzo chochote cha maji hicho kiwekwe sehemu iliyo inuka ili kufanya maji yateremke vizuri kwenye bomba mpaka kwenye mmea.

2. Aina ya udongo ni muhimu sana kujua aina kama ni tifutifu, kichanga au mfinyanzi,hii itakusaidia mkulima kujua uwezo wa aina husika ya udongo wa kuhifadhi maji ardhini.

3. Mgawanyo wa maji.
Maji ni lazima yawe yenye ubora na maji yawe ya uhakika, kwa kuzingatia hilo pia topografia ya eneo husika ni iwe tambarare au mteremko kiasi Kuruhusu maji kugawanyika vyema kwenye mmea kwa kiwango kile kile na spidi ile ile kwa kila mmea.


3. Kila zao lina nafasi zake katika upandaji hivyo unavyoweka mfumo wa umwagiliaji hakikisha nafasi unazo weka ziendane na nafasi ya zao husika.
Uendeshaji wa mfumo huu wa umwagiliaji
1. Mfumo huu uendeshwe kwa kuzingatia maji yanafika katika mmea husika kwa kiwango kile kile kwa mimea yote
2. Hakikisha hakuna upotevu wa maji kama bomba zinavuja hakikisha hazivuji. •Mfumo huu kuwa wenye mafanikio yapaswa ukaguzi wa mara kwa mara ili kuangalia unavyo fanya kazi.
3. Hakikisha maji yanafika katika mmea kama inavyotakiwa. Kabla hauja upeleka katika utekelezaji mfumo huu shambani chora kwanza ramani katika katika karatasi halafu nenda ukauweke shambani.
Karibuni wadau wote wa kilimo katika mapinduzi haya ya kilimo ya kisasa, tutaona eneo lako lipoje tutakushauri bure kabla ya kuanza kazi yenyewe, pia tunatengeneza greenhouse kwa bei rahisi tu. Usiogope kuuliza, piga number 0786518551.napatikana mbagala dsm, asanteni sana
images%20(44).jpeg
inline-drip-irrigation-system-500x500.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom