INAUZWA Jipatie Excel Template ya kuchakata matokeo ya wanafunzi (O-level) kwa sh 35,000/=

Njuka II

JF-Expert Member
Feb 25, 2019
400
693
Natumaini kuwa sote ni wazima wa afya

Bila kupoteza muda, niende moja kwa moja kwenye mada. Mimi ni mtaalamu wa Microsoft Excel, Leo nimekuja na template ambayo kazi yake ni kuchakata matokeo ya wanafunzi wa O-Level.

Hii template ina uwezo wa kuchukua wanafunzi 400 na ina worksheets tano, kila worksheet ina kazi yake, nitazielezea moja moja.

1. Worksheet 1 (setting)

Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anafanya setting za grades, divisions n.k
Mfumo wa penalty nimeuweka kama optional, mwalimu atachagua YES/NO kulingana na mahitaji yake.

Wanafunzi ambao watapigwa penalty ni wale ambao watakuwa wamepata division one na division two lakini wamefeli somo la Basic Mathematics au Kiswahili.

Pia katika hii worksheet kuna sehemu mwalimu ataset alama ya ufaulu (pass mark) ambayo itakuwa inalinganishwa na wastani alioupata mwanafunzi kwa masomo saba aliyofaulu zaidi, nitaielezea vizuri dhumuni la kuweka hii passmark katika worksheet inayofuata.

2. Worksheet 2 ( Score sheet )

Hii ni worksheet ambayo mwalimu atakuwa anajaza majina pamoja na alama (marks) za wanafunzi wake. Mwalimu atajaza alama tu, grades zitajijaza zenyewe kulingana na setting ulizofanya kwenye worksheet 1.

Pia mwalimu atajaza jina la shule yake , tarehe, na kidato (Haya maelezo yatatumika katika worksheet zingine).
Worksheet hii itamsaidia mwalimu kuwajua wanafunzi waliofaulu (Pass), wanafunzi waliofeli (Fail), wanafunzi ambayo wamefanya mitihani nusu (chini ya masomo saba, Incomplete) na wanafunzi ambao hawajafanya kabisa mitihani (Absentees).

Wanafunzi wote ambao watakuwa wamevuka alama ya ufaulu (pass mark) ambayo uliijaza kwenye setting watakuwa na highlight nyeupe, wanafunzi ambao watakuwa hawajafikisha alama ya ufaulu watakuwa na highlight ya kijivu(grey), wanafunzi ambao watakuwa wamefanya mitihani ambayo idadi yake haifiki saba watakuwa na highlight ya kijani mpauko, na wale ambao hawajafanya kabisa mitihani watakuwa na highlight ya orange mpauko.
NB: Nimeweka key za highlights zote hapo juu

3. Worksheet 3 (Student's Report)

Hii ni worksheet ambayo kazi yake ni kutengeneza report za wanafunzi wote ambao mwalimu aliwaandika kwenye sheet ya kurekodi marks (score sheet).

Inaonesha nafasi (position) kwa kila mwanafunzi utakayemchagua kwenye list (drop down list, ambayo itadisplay pale utakaposelect cell yenye jina la mwanafunzi)
Worksheet hii mwalimu haruhusiwi kuandika chochote zaidi ya kuchagua jina la mwanafunzi tu, cells zote zilizopo kwenye hii worksheet zinajijaza zenyewe na pia nimezilock ili kulinda formula nilizoziandika.

4. Worksheet 4 (Overall results)

Hii ni worksheet ambayo inaonyesha matokeo ya jumla kwa wanafunzi wote.
Kurasa moja inachukua idadi ya wanafunzi 40, kama idadi ya wanafunzi wako itakuwa ni zaidi ya 40 utachagua page inayofata ili kupata orodha ya wanafunzi wengine (41 mpaka 80) na kuendelea.

5. Worksheet 5 (Results summary)

Hii worksheet inafanya kazi zifuatazo

(i) Inaonesha idadi ya wanafunzi wote waliofanya mtihani (total candidates), na wale ambao hawakufanya (absentees)

(ii) Inaonesha idadi ya madaraja (Divisions)

(iii) Inaonesha asilimia ya wanafunzi waliofaulu na waliofeli

(iv) Inaonesha idadi ya wanafunzi waliofaulu na waliofeli kwa jinsia zote mbili

(v) Inaonesha idadi ya grades kwa masomo yote 11

(vi) Inaonesha idadi ya wanafunzi ambao hawajafanya mtihani wa somo husika kwa masomo yote.

(vii) Inaonesha majina ya wanafunzi bora (top ten) bila kujali nafasi ya mwanafunzi katika orodha. Hata kama mwanafunzi bora jina lake lipo kwenye s/n ya 400, template itamtafuta alipo na kumuweka kwenye nafasi anayostahili.

Worksheet hii mwalimu haruhusiwi kuandika kitu chochote zaidi ya kuprint tu. Cells zote zina formula na zinajijaza zenyewe.

Nimeshindwa kuweka picha kati kati ya maneno,hivyo picha zote nitaziweka kwenye comment ya pili.

TEMPLATE REQUIREMENT

>> Microsoft Office 2010 na kuendelea, Ms 2007 kuna baadhi ya function hazipo

Bei ya hii template ni Tsh 35,000/=

Kama utakuwa ni muhitaji, tuwasiliane PM au kupitia email yangu hapo chini.

>Template zingine ambazo nimeshaziandaa ni

  • Template ya wahasibu (PAYE payroll) Tsh 25,000/=
  • Template ya matokeo (primary) Tsh 20,000/=
  • Template ya matokeo (A-level) Tsh 35,000/=
  • Template ya michango/ada (A-level& O-level) Tsh 20,000/=
  • Template ya biashara Tsh 25,000/=
  • Automated School time table generator Tsh. 15,000/=

Ukihitaji kutengenezewa template ambayo haipo kwenye orodha hapo juu tuwasiliane pia

Njuka II
Expert in Microsoft Excel
Email: ebusiness.excel@gmail.com
Dar es salaam,
Sunday 08-09-2019

UPDATED

Template imeboreshwa na sasa inachukua mitihani miwili miwili (midterm &terminal) kwa kila somo tofauti na hapo awali. Angalia picha kwenye comment #87
 
Student's report ( Upande wa chini)
report.JPG
 
Katika sheets zote 5, mwalimu anajaza sheet moja tu (score sheet), sheet nne zilizobaki zinajijaza zenyewe. Unaweza ukaprint report za wanafunzi wote 400 ndani ya siku moja, template inakupangia mpaka nafasi (position) kwa kila mwanafunzi.

Unaweza kuprocess matokeo ya shule nzima ndani ya siku mbili hata kama una wanafunzi 2000, page setup zote pia nimeshaziset.

Utakuwa unachagua jina la mwanafunzi na kuprint bila kufanya setting za page kama vile margin, paper size n.k
 
Very good... Nataman saan kuwa mkali wa excel ila naishia kucheza na sum.. Countif n.k

Nisaidie hata pdf document niwe expert walahu kidogo mkuu.

Hata zile site nipige pindi niwe mkali mkuu
 
Very good... Nataman saan kuwa mkali wa excel ila naishia kucheza na sum.. Countif n.k

Nisaidie hata pdf document niwe expert walahu kidogo mkuu.

Hata zile site nipige pindi niwe mkali mkuu
Kwa level ya beginner utatumia nguvu nyingi kuelewa kama utatumia njia ya kusoma vitabu. Kwa sasa tumia njia ya video (YouTube) au mtu akufundishe ana kwa ana mpaka pale utakapokuwa na basics za kutosha
 
Basic unayozungumzia kama hipi man maana nagusa gusa vipi ila kwenye kutengeneza full project ndio tatizo..

Alafu hata kam youtube sometime nashndwa elewa naandika nin ili kije ninachokitaka..

Inatakiwa uanze kujifunza function moja moja na ujue kazi ya kila function, mfano hiyo template ina function tofauti tofauti zaidi ya 70. Ukishazijua functions (sio lazima zote kwa level yako, hata baadhi)ndipo utajua ni function ipi itumike ili ifanye kazi unayotaka. Kuna muda pia inafika kunakuwa hakuna function yoyote inayoweza kufanya kazi unayotaka hivyo inakulazimu kuunganisha function zaidi ya moja kwenye formula moja. Uwe mvumilivu wakati wa kujifunza, ktk excel unapokuwa ktk hii level unaweza ukaandika function 10 na zote zikakugomea zisilete kitu unachokitaka, usikate tamaa endelea kujifunza zaidi. Website zipo nyingi kuna Mr Excel, computer gaga, Prietra Kumar,PK(huyu ni muhindi, anaongea English lakini matamshi yake magumu kuyaelewa mpaka umzoee), Leila Ghalani (huyu ni mdada wa kizungu, ana channel yake YouTube), Sele training n.k
 
Shukran mkuu ngoja nianze nazo..
Ila ni zipi function zinatumika saana katika project kama hii ya kwako...

Yaani uwezo wa kuliko data ya sheet moja na sheet nyingine...

!?
 
Back
Top Bottom