Jipange mzazi mwanao asipokee boom na asitegemee ajira

mandokwa

JF-Expert Member
Jun 5, 2013
620
865
Moja ya jukumu la mzazi ni kumjengea future mtoto wake.
Kulingana na hali ilivyo ni dhahiri kutegemea mkopo wa elimu ya juu ni kukwepa majukumu na kumsababishia mtoto wako maisha magumu sana hapo baadae. Yaani makato plus interest ukilinganisha na mshahara anaopata kwa degree ya kwanza ni lazima hana nafasi ya kupanda kwa miaka 10 ya mwanzo.

Pia hali ya ajira munaona imekuwa mbaya sana. mashirika na taasisi binafsi zinapunguza watu kila siku. Serikali haitamudu kuajiri kila siku hasa ukilinganisha kwamba technologia inakua kila siku. Ofisi ikiingia kwenye e-hrm/hris na mifumo ya aina hiyo inaweza kutekeleza malengo yake kwa kutumia wafanyakazi wachache sana, hakuna tena haja ya messengers, HRs, nakadhalika.

Nashauri kama mzazi kuanzia kijana wako akiwa form four anza kumpa mbinu mbadala. Nawe anza kujipanga kwamba akimaliza tu hakikisha unampatia mtaji hata ikiwa umekopa wewe ajisogeze mwenyewe. Nimesema anza mapema kwani najua biashara na ujasiliamari sio lelemama. Lazima umjengee msingi wa kumudu majukumu yake. Yaani hata ikiwezekana badala ya kumpa zawadi ya kufaulu, mnunulie shamba msaidie kupanda miti au miche ya matunda aanze kuwaza ....

Nawakumbusha ukikosea sasa, utalia ukiwa mzee kwani hutakuwa na wakukupa msaada.

Nangu Mandokwa,
 
Kwa sisi watoto wa maskini unatunyima haki ya kusoma mkuu.....MTU uchaguliwe chuo cha jiji LA makonda,huna boom na ada tu ya secondary 35000 ilipatikana kwa kuuza mashamba....HV utasoma kweli??? .acheni jmn...boom n muhimu kwa watoto wa maskini
 
===
Rejea kusoma hutakuta mahala nimekuongelea wewe!! Nimeongea na wazazi wenye kuweza kujibana wakagharamia haya mambo...
 
Kwa sisi watoto wa maskini unatunyima haki ya kusoma mkuu.....MTU uchaguliwe chuo cha jiji LA makonda,huna boom na ada tu ya secondary 35000 ilipatikana kwa kuuza mashamba....HV utasoma kweli??? .acheni jmn...boom n muhimu kwa watoto wa maskini
Acha ubishi wewe pia ni mzazi mtarajiwa, jipange.
 
Back
Top Bottom