Jionee ndege ya kisasa ya Ethiopia ikiwa Nairobi

Mr Hero

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
5,542
7,450
160714104805_ethiopia_airlines_airbus_640x360_bbc.jpg

Image captionEthiopia Airlines ndiyo ya kwanza Afrika kununua ndege aina ya Airbus A350 XWB
Ethiopia imekuwa taifa la kwanza barani Afrika kununua ndege ya kisasa aina ya Airbus A350 XWB.

Ndege hiyo, Airbus A350, ndiyo ya hivi karibuni kuzinduliwa na kampuni ya ndege ya Airbus ya Ufaransa.

Ndege hiyo, iliyo na uwezo wa kubeba zaidi ya abiria 300, ilitua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi Kenya Jumatano jioni ikitokea mjini Addis Ababa, Ethiopia.

160714110235_ethiopia_airlines_airbus_640x360_bbc.jpg

"Ndege hii ya kisasa itasaidia katika utoaji wa huduma zetu, kuimarisha mtandao wetu wa usafiri, na kupunguza kwa kiasi kikubwa viwango vya hewa chafu inayotolewa wakati wa usafiri wa ndege,” Mkurugenzi mkuu wa shirika la Ethiopian Airlines Tewolde GebreMariam amesema.

Ndege hiyo ni ya kwanza kuwasilishwa kwa kampuni hiyo, huku nyingine 13 ilizoagiza kutoka kwa kampuni ya Airbus zikisubiriwa hivi karibuni.

Safari ya kwanza ya ndege hiyo ilifanyika tarehe 2 Julai iliposafiri kutoka Ufaransa hadi mjini Lagos, Nigeria.

160714105855_ethiopia_airlines_airbus_3_640x360_bbc.jpg

Viwango vya juu vya teknolojia iliyotumika kuunda ndege hiyo, vinachangia katika kuinua utendakazi wake, kupunguza matumizi ya mafuta pamoja na kupunguza kwa kiasi kikubwa utoaji wa hewa chafu.

Kampuni ya Ethiopian Airlines inaorodheshwa ya kwanza barani Afrika kwa faida na pia idadi ya maeneo inayosafirisha abiria.

160714110618_ethiopia_airlines_airbus_5_640x360_bbc.jpg

Mwaka wa 2012, shirika hilo pia lilikuwa la pili duniani na la kwanza barani afrika kununua ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner, ya kampuni ya Boeing, yenye afisi zake kuu Chicago, Marekani.

160714105335_ethiopia_airlines_airbus_2_640x360_bbc.jpg

Kampuni ya Airbus na Boeing zinaongoza duniani katika utengenezaji wa ndege za kisasa, japo Airbus ina umaarufu mkubwa na imeipiku Boeing kwa faida na uuzaji wa idadi kubwa ya ndege.

  • Dakika 41 zilizopita
Mshirikishe mwenzako

Tanzania ktk awamu ya Tano tumedhamiria kununua kama hizi 2 kabla ya September.

Hizi ni kwa kuanzia.. Kabla ya 2020 zitakuwa sio chini ya 12.
 
Subiri zitue ndani ya ardhi ya Tanzania
bombardier dash 8 q400
Kule Canada or north America ni special kwa ajili ya kuzima moto wa misituni,Ndoo jirani yetu Kagame kamshauli mkuu wetu wa nchi kununua hizo ndege,wakati yeye Kagame kanunua Airbus 3
N'jomba hizo ndege zinazonunuliwa na serikali wala hazikaribii kulingana au hata kufanana na hiyo ndege ya Ethiopian...!!
 
bombardier dash 8 q400
Kule Canada or north America ni special kwa ajili ya kuzima moto wa misituni,Ndoo jirani yetu Kagame kamshauli mkuu wetu wa nchi kununua hizo ndege,wakati yeye Kagame kanunua Airbus 3
Hahahahahaha mkuu mbavu zangu
 
  • Thanks
Reactions: MC7
Mimi kila mara nikiona au nikipanda Ethiopia Airlines huwa nalia na kumuuliza Mungu sisi Tanzania tumekosea/tunakosea wapi?
 
Hiyo ndege ni nzuri sana na hongera kwa nchi ya Ethiopia. Isipokuwa next time msitupie picha ya cockpit Ikiwa imekaliwa na mtu ambaye kwanza sio rubani , pili mvuto ni F- sijui ametabasamu au analia,.....

Kaharibu kilakitu.
 
bombardier dash 8 q400
Kule Canada or north America ni special kwa ajili ya kuzima moto wa misituni,Ndoo jirani yetu Kagame kamshauli mkuu wetu wa nchi kununua hizo ndege,wakati yeye Kagame kanunua Airbus 3
Unadhani mmiliki wa Rwandan air atamshauri nini air tz?? Biahsra babu
 
Tanzania ktk awamu ya Tano tumedhamiria kununua kama hizi 2 kabla ya September.

Hizi ni kwa kuanzia.. Kabla ya 2020 zitakuwa sio chini ya 12.
Ethiopia wamenunua hizo ndege baada ya kufanya tathmini ya matumizi na sio tu based on political gain. Ethiopian airline iko pote duniani na ABIRIA ni wengi wanaotumia hili shirika. Hivyo kabla ya kuja hapa kusema Tanzania itanunua kama hizo mbili tueleze abiria watakuwa nani? Lisije likawa Kama ile issue ya katiba mpya!
 
Something is better than nothing, hata tukinunua za kubebea maembe huko Ulaya ni bora kuliko aibu ya kuwa na mindege ya kukodi with -VE profit. Go go JPM, tuokoe na aibu ya kukalia kusifia vya wenzetu vyetu vikitufia
 
Back
Top Bottom