Jiokoe na ajali ya moto;chukua hatua hizi kujilinda na kuilinda familia yako

David M Mrope

Member
Jul 13, 2021
48
95
Sasa yapata siku chache toka soko kuu la kariakoo lipatwe na janga la moto. Lakini baada ya janga hilo kuna mengine ambayo yanaendelea kutokea kama mzaa mzaa hivi na wengi wanaumia tu bila ya kujua wajikinge vipi.

Kwanza naomba serikali ichukue hatua katika kupambana na swala hili. Serikali ijikite katika kutoa elimu juu ya mapambano ya ajali za moto katika makazi,vituo vya kazi,sehemu za mikusanyiko,shule n.k

Basi makala hii inakuletea moja kwa moja njia ambazo unaweza chukua ukiwa nyumbani ili kuepuka na ajali ya moto.

(i) HIFADHI MAHALI TULIVU & SALAMA VIFAA VYOTE VYA MAFUTA NA MLIPUKO.
Kama upo katika nyumba yako,basi hakikisha vifaa vyote vya mlipuko kama jenereta na jiko la gesi unavihifadhi sehemu moja tulivu.

Hakikisha katika nyumba yako,hakuna ukaribu kati ya watoto wako na jenereta au watoto na jiko la gesi. Hii itakusaidia kuzuia hizi ajali za moto.

(ii) HIFADHI MCHANGA NDANI YA NYUMBA YAKO.
Mchanga husaidia kuzima moto kwa kiasi kikubwa sana. Unaweza kuwa moto wa mafuta au umeme. Ni vizuri ukaacha kutegemea maji kwa sababu sio kila moto unazimwa na maji mfano wa umeme.

Hivyo ni vizuri kuhifadhi mchanga kwenye ndoo na uweke sehemu ya wazi,kama jikoni au karibu na mlango ndani na nje.

(iii) HAKIKISHA UNAZIMA VIFAA VYA UMEME KABLA YA KULALA.
Hii itakusaidia sana kwani ajali nyingi hutokea usiku wa manane. Basi unashauriwa kuzima vifaa vyote vya umeme kabla ya kulala.

Kumbuka usiku wote unakuwa umelala sasa anaweza pita hata panya akadondosha kikombe chenye maji yakamwagikia vifaa vya umeme na kuanzisha tatizo.

(iv) KIMBILIA KUZIMA KIRUHUSU UMEME (SWITCH) HARAKA UONAPO DALILI MBAYA.
Dalili mbaya ni kama radi nyingi,au maji yamemwangika kwenye kifaa cha umeme. Hizi ni dalili za kutokea kwa hatari ya moto katika nyumba.

Kumbuka njia hizi ni za kujiokoa mwenyewe na kuiokoa familia yako.

(v) PENDA KUKARABATI MFUMO WA UMEME WA NYUMBA YAKO BAADA YA MUDA FLANI.
Hili jambo ni muhimu sana japo wengi hupuuza,hasa kikwetu. Wengi wakishaingiza umeme na ikawaka taa basi wanaacha hata miaka kumi.

Unaweza kuta shule flani mfumo wake wa umeme unamiaka hata 20 na hata hawaiti mafundi kuja kukagua. Kumbuka hizi waya pamoja na vifaa vingine vya umeme vinakikomo chake,sasa ni vizuri kuvibadilisha baada ya muda flani.

Mwisho,naomba tuendelee kuchukua tahadhari juu ya janga hili la moto.

DAVID M MROPE.
SUA.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom