Jinsi ya wanavyoripoti ajali za magari ya jeshi kinafiki; unaweza dhania Tanzania kuna sheria mbili huko barabarani

kuna uzi nyuzi nyingine sio za kuchangia....... unaweza kujikuta pasipojulikana
Mi napita............
 
Ni akili za kijinga sana eti polisi mmoja anapigwa na kijiji kizima, daaah kweli akili ni nywele
Hakuna polisi anaye muongopa mjeshi,ila kulikuwa na hii tabia ya wanajeshi wengi kwenye roli wanapiga trafiki 3 walio kwenye point. Sasa uoni kuwa wanajeshi ni dhaifu!! POLISI nao naona wameongeza nguvu, juzi nikitoe huko Dar nmeona kila point ya trafik ina askari 2 wenye silaha, I hope nikwaajili ya ulinzi ili mjeshi akizingua wammwage ubongo/wamtoe ngama.
 
Hapa ndipo ninapokumbuka maandishi ya George Orwell katika Kitabu chake Adhimu 'Animal Farm' Kiongozi wa Wanyama *Ngururuwe mmoja aitwaye Napoleon* alipowawekea wanyama sheria kwamba 'Wanyama wote ni sawa ila wengine ni sawa zaidi'
 
Juzi traffic alikuwa ana simamisha magari na gari zote zilisimama, hafla kushoto ikatokeza gari ya jeshi na kupita. Yule traffic alijifanya kama hakuiona nikabaki kujiuliza yule dereva wa jeshi hajui sheria za barabarani. Na huyu traffic kwanini haku msimamisha yule dereva kwa kuvunja amri yake?.


Ndukiiiii
usidhani huyo traffic ni muoga sana hapana.sheria imeruhusu gari za dharula,na vyombo vya ulinzi kujiongeza barabarani kwa umakini,maana zina haraka zaidi muda wote.huwa zinavamia njia hata gari za tanesco mpaka miguuni kwa traffic na anairuhusu.

kimsingi tusilazimishe usawa,na wao wasipae sana maana bado ni binaadamu tu akikosea mahesabu kama hivi ndio basi tena,anakufa au anaua.
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom