Jinsi ya kuzuia tatizo la kuharisha safarini

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,198
12,691
Tatizo la kuharisha safarini linatatiza sana na pia huabisha. Shida hii husababishwa na sumu zilizotengenezwa na bakteria au virusi uliowameza kwenye msosi. Ni jinsi gani ya kujizuia.

1. Usile vyakula vichafu hasa usiku kabla ya safari. Wengi wanaopata shida ya kuharisha safarini si sababu ya vyakula wanavyokula safarini, ni sababu ya vyakula walivyokula jana usiku. Kawaida sumu hizi huchukua kuanzia masaa nane kuanza kusababisha kuharisha toka mtu ale sumu hizo. Sasa unaamka vizuri, unashanga umekula tu kidogo tumbo linachafuka. Sumu ile ya jana inakuwa imeanza kufanya kazi. Vyakula hatari kwa kusababisha mambo haya ni chachandu, kachumbari na jamii ya nyama isiyoandaliwa vizuri. Unakuta mtu amsechamba, na bila hata kujisafisha vya kutosha anaenda kuandaa kachumbari au chachandu. Ni rahisi sana kupata wadudu na hizo toxins.

2. Flajili haifungi kuharisha. Ukianza kuharisha usitegemee flajili itafunga. Dawa za kufunga kuharisha zipo, moja wapo inaitwa Loperamide. Na ni vema sana hii dawa ikawekwa kwenye mabox ya huduma ya kwanza kwenye mabasi. Hii inatuliza misuli ya tumbo haraka sana hivyo inakata kuharisha fasta. Fajili ni dawa ya kuua bakteria, inachukua muda mrefu kufanya kazi. Siyo dawa ya emergency.

3. Epuka vyakula vya vinavyoweza sababisha uharishe. Kama unajijua mbovu wa vyakula fulani, basi usitumie wakati wa safari au masaa kadhaa kabla ya safari kama usiku wa safari. Kuna vyakula kama Juisi ya ukwaju. Ukwaju huwa unatabia ya kulainisha choo na kuongeza msukumo. Epuka juisi hiyo safarini.
 
Dah kuna siku naenda Moshi, nimefika ubungo asubuh tumbo likavuruga.. choo cha geti la kutokea pale kikaniokoa.. tumefika kibaha ngoma bado mbichi, gari imeingia kujaza mafuta ndo pona yangu.. sema konda alikuwa na dawa akanipa ndo tumbo likatulia...

Kuna siku natoka mwanza, nimefika dodoma nikafakamia zabibu.. dah kilichonikuta siji kusahau.. kuna sehem ya mizan ndo pona yangu tena kulikuwa na choo kibovu kweli kweli

Kwa sasa huwa naogopa sana kula kula njiani.
 
Ukiona tatizo limejirudia ujue tatizo ni wewe.Afu wanaume hawakulikuli njian
 
Safarini tembea na kamba kavu ya magome ya mgomba. Funga kidole cha mwisho cha mguu wa kushoto.

Huwezi kujisaidia haja kubwa NG'OO hadi ufungue kamba hiyo.

TEST IT
Hii experiment tuifanye wakati mtu keshakula na kunywa vya kutosha tuone kama itafanya kazi
 
Dah hatar hyo nimetoka zangu simu 2000 Happo ubungo naendanzangu bunju then bagamoyo aise nilifika mitaa ya stanska then kwend ndevu pale nikaona Hali ya tumbo haliko sawa nasikia mzigo umekaribia kbsa kushuka kukata lock kbsa ebwaaa eeeh acha kbsa nikashuka faster Hapo kwa ndefu nikaona nifupishe safari. Na ilikuwa nimeashalipa nauli ya mpk mwisho wa safari dalalda imesimama tu hv mm huyo nikashuka pale faster nikaingia kuuliza Kama Kuna huduma ya choo karibu jama aknimbia zungunguaka hapo nyuma ipo ebwana nikazama nikakuta jamaa anataka hela ndipo uingie ndani kwa bahat nzur ndio mtu anatoka ndani

Aisee asalalee nilishusha shehena kubwa kas ya ajabu mno jamaa anaeyetoza hela naisi alisikia ule mlio niliouachia kwa kas ya 4 g dahaa ilikuwa imebakiza sekonde kumi na tano ngoma ikate loki yenyewee na kudhalilika vibaya mungu akaniokoa na aibu hyo kwa kupat sehem ya karibu faster duh acha kbsa

Siku nyingine niligoma kusafir kutoka mbeya had Arusha baada ya kuona tumbo haliko sawasawa niliahrisha kwenda safari ile had nione hali itakuaje aise nilkah wik mbili kumbe ndio nilikuwa nimeanzakuugua typhoid na homa ya tumbo mnk siku hyo nilidrive mno nikaja bas ningesafiri hat nisinge fika igurusi kwa loki kukata

Sasa HV msaad awangu Ni loperimide
 
Mimi nakushukuru sana mkuu kwa kunijuza hiyo dawa maana mara kadhaa nimepatwa na shida hiyo ya kuchafukwa na tumbo nikiwa safarini ila frajili amekuwa mkombozi wangu mara zote hivyo nikianza safari tu lazima pacti iwemo kwenye mfuko wa shati.
 
Back
Top Bottom