Jinsi ya kuyaepusha maji yako kuota utandu wa kijani (Algae)

chinchilla coat

JF-Expert Member
May 16, 2016
5,107
10,968
Unaweza ukawa umehifadhi maji yako kwenye tank, bwawa au resevoir yako nyingine ya kutunza maji lakini yakawa yanakabiliwa na kutokea kwa utando wa kijani na kuyachafua
Utando huo unaitwa algae na ni kama aina ya mimea sema ni microscopic, na huzalisha sumu zinapooza
Utando huu hukua maji yakiwa yanapata mwanga na yakiwa na madini mengi ya phosphorous
Kuepusha utando huu kuota hifadhi maji yako sehemu isiyopata mwanga, kama tank lako linapitisha mwanga basi utahitaji tanki jeusi lisilopitisha mwanga
Pia unaweza ukazuia utando huu kuota kwa kutumia chlorine, chlorine inapatikana kwenye vitu kama bleach na dawa ya waterguard lakini ni lazima kuwa makini kwani chlorine ni sumu ikiwa nyingi so utawasiliana na mtaalamu atakayekuuzia akuambie ni kiasi gani utaweka kulingana na concentretration ya chlorine kwenye hiyo product
 
Back
Top Bottom