Jinsi ya kuweza kumiliki Shamba kihalali mkoa wa Dodoma

uduzungwa

JF-Expert Member
Oct 12, 2016
552
541
Wana ndugu Salama.
Jinsi kichwa cha habari kinavyojieleza hapo juu. Mie ni mtumishi wa serikali nimehamiahuwa hapa mkoani dodoma kama miezi nane iliyopita. Sasa kale kasenti kangu ka uhamisho kilivyotoka nikajipatia Shamba lenye ukubwa kama hekta 5 Maeneo ya huku msalato.
Nimeuziwa na mwanakijiji wa hapahapa.
Nimeshamlipa hela yake yote.
Sasa ombi langu kwa wadau wenzangu ni kuwa nataka nijue zile process za kuweza kufuatilia ili niweze kupata hati ya hili Shamba mana nataka nijenge kibanda changu hapahapa.
Kwa wale wazoefu wa dodoma na maeneo mengine naomba nisaidie hapo nikamilishe huu umiliki wa hili shamba.

Naomba kuwasilisha.
 
Bei gani hekari moja?na mimi nahitaji hekari tano mkuu maana naa mimi ni MtuMISHI km wewe
 
Siku zote mnatangaziwa msinunue viwanja kwa kipindi hiki mpaka mtakapotangaziwa! Kwa kuwa wanapima viwanja vitakavyokidhi mahitaji ! Kumbuka kuwa unaweza ukauziwa eneo ambalo limepangwa kuwa barabara au uwanja wa Mpira, Ulikuwa na haraka gani?
 
Back
Top Bottom