Jinsi ya kuwasaidia Watoto Viziwi ambao ni wahanga wa ukatili kwenye jamii

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,010
9,875
Jinsi ya kuwasaidia Watoto Viziwi ambao ni wahanga wa ukatili kwenye jamii:

Wanajamii wanapaswa kushirikiana na viongozi wa maeneo yao kuwatambua na kufuatilia maendeleo ya Watoto viziwi wanapokuwa nyumbani, kwenye Jamii na shuleni.

FUWAVITA inaihimiza serikali na mashirika binafsi kuweka watoa huduma wenye ujuzi wa alama ya lugha katika huduma za umma ili waweze kuhudumia kundi la viziwi na hasa Watoto viziwi.

Wanajamii kukemea familia ambazo huwatenga Watoto viziwi badala ya kuwapeleka shule.

Serikali kuwekea mkazo katika sheria na sera zilizopo zinazolazimu wazazi kuwapeleka Watoto shule na zinapokiukwa kuwepo na uwajibishaji.
 
Watoto wenye changamoto mbali mbali wamekua Wahanga wa matukio ya kikatili hasa wenye uziwi kwa kuwa wanashindwa kujitetea hata kwa kupiga kelele.

Ni umefanya jambo bora kuwakumbusha wazazi namna bora ya kuwalinda watoto hawa dhidi ya matukio ya kikatili.

Serikali pia ikumbuke kuboresha huduma katika shule maalumu ili watoto wajifunze kwa uhuru kama watoto wengine.
 
Back
Top Bottom