Jinsi ya kuwa Tajiri

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
733
rolls-royce-phantom.jpg


Kila mtu katika ulimwengu huu ukimuuliza swali hili JE UNATAKA KUWA TAJIRI? Jibu utakalo lipata hapo ni NDIO. Ndoto hii huwa katika vichwa vya watu wengi ambao bado waiona ni ndoto tu na haiwezii kuwa kweli. Baada ya kusoma makala hii fupi tunaamini kuwa utaweka jitihada na wewe za kufikia ngazi hiyo ya utajiri.

KURITHISHWA UTAJIRI: Hii ndio njia rahisi kabisaaa ya kuwa tajiri na kutengeneza pesa. Kama wewe ni mwenye bahati ya kuzaliwa katika familia ya kitajiri hauna haja ya kutumia nguvu nyingi katika mpango mzima wa kutafuta utajiri kwa sababu tayari unao katika himaya yako. Lakini kama familia yako haina utajiri basi hapo sasa ndio unatakiwa kuingia katika mpambano.

SHINDA BAHATI NASIBU: Utajiri pia unategemeana na bahati. Tumeshudia watu mbalimbali nchini wakiingia katika utajiri kwa kushinda bahati nasibu mbalimbali. Ushindi wa milioni 100 mara nyingi humfanya mtu hatakama alikuwa ameajiriwa basi kuacha kazi na kujiajiri. Hii pia ni aina mojawapo yakuwa tajiri kwa gafla.

KUZA KIPAJI CHAKO: Kila mtu anakipaji chake binafsi kazi kubwa ipo katika kukitambua kipaji hicho. Kipaji kama kipaji kinatakiwa kiweze kuonyeshwa katika soko ili kiweze kukusaidia kukupa utajiri. Watu wengi wameacha shule nakuamua kufuata vipaji vyao na sasa ni matajiri wakubwa katika ulimwengu wasasa. Mfano mkubwa ni waimbaji wanamichezo, mamodel, na waburudishaji. Kwa kulijua hilo basi jaribu kutafuta kipaji chako hata kama umekaa hapo ofisini ukiwa na laptop yako.

ANZISHA BIASHARA: Kama unamapenzi na uvumilivu unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendeleza na kuwa na maisha mazuri. Ukilisoma soko vizuri kabla hujaamua kuingia au kukopa fedha katika taasisi za fedha unaweza kuiona fursa ambayo itakupa mwanga juu ya biashara yako. Mapenzi ulionayo juu ya biashara yako itakupa utajiri usiotarajia.

KAMATA FURSA ILIYOPO: Fursa hata siku mmoja haiji mara mbili. Hiiyo inakupa umakini wakuwa macho iliuweze kuiona hiyo fursa, hata siku moja usikubali fursa ikupite tena kama ipo ndani ya uwezo wako. Je utajuaje au utaitafutaje fursa? Unachotakiwa kujua ni fursa zimekuzunguka tumia mda wako na utulivu katika kuziangalia zipo.miaka 8 iliyopita Nani alijua kuwa biashara ya utoaji huduma ya kuosha magari ingekuja kuwa fursa kubwa wakati huu, lakini wale walioona hiyo fursa sasa wanapesa nzuri tu na mpaka watu wanaanza kuiga wao labda walishafikiria kuiacha.

Haya umeshajua njia za kuweza kuwa tajiri ni juu yako kuwa tajiri au kubakia maskini..
 
jinsi ya kuwa tajiri ni opositi ya jinsi ya kuingia mbinguni. Do the opposite ya sinsi ya kuingia mbinguni na utakuwa tajiri
 
Njia nyingine ni kununua hisa katika mfumo uliyopo unaofanikiwa kujenga timu nawe uwe sehemu ya mafanikio hayo.

Kuwa TAJIRI kuwa na UHURU WA KIPATO or FINANCIAL FREEDOM ni rahisi sasa kuliko wakati mwingine wowote, soma kitabu cha Paul Zane Pilzer cha Next Millionaires, au chapisho lake la The perfect Storm of Opportunity utaona kuwa kuna aina ya biashara ambayo inazalisha mamilionea wapya kila mwaka,

Pia soma Kitabu cha Robert Kiyosaki "Rich Dad's Cashflow Quadrants", au Benson Mahenya cha "Biashara ya Mtandao" utaona fursa za watu kutajilika kwa kuanza na kiasi kidogo sana cha mtaji.

Yawezekana fursa hii wapo waliokutana nayo, hawaikuilewa wakaicha na kueneza habari isiyo nzuri ya kitu wasichokijua vizuri (ndo hulka ya waTZ), ama wapo waliojaribu, hawakuwa na uvumilivu ama muda kuisoma vyema wakaacha wakazidi kusambaza habari mbovu.

Tembelea HAPA, ujionee Bill Clinton anasemaje, Tajiri namba 2 duniani Warren Buffet na anazungumziaje, Maprofesa Charles King na Paul Zane Plizer wanashauri nini katika Biashara inayokuja juu Duniani ya NETWORK MARKETING ama Biashara ya Mtandao.

Pia WEBSITE HII utajulishwa kwa kampuni iliyofanikiwa sana Duniani kwa biashara hii.

Bila shaka kila mtu anaweza kuwa TAJIRI akiamua, ndio ni suala la UAMUZI ama KUCHAGUA kuwa au kutokuwa TAJIRI.
 
Mbona hujataja hii njia ya kupata utajiri?

"Jifunze ku-save pesa benki kidogo kidogo kama 25% ya mshahara wako kila mwezi, hii ni pamoja na kuwa na nidhamu katika matumizi ya pesa zako"

Imeekaaje hiyo???
 
Write a Book on How to Become Rich........

Seriously fata following points:-
Spend less Than What you earn, then save and invest
repeat the above
 
Jamani kama kichwa kinavyojieleza, nauchukia sana umaskini. Siupendi umaskini, nimefanya kazi sana za kuajiriwa na huu ni mwaka wa kumi, lakini sitajiriki. Nifanyeje?
 
kuwa yafuatayo.
-askofu au nabii au jiitee mtume kabisa
-anzaaa kuimbaa taarabu coz mzee yusuph hana mpinzani
-kuwa mwizii ikiwezekana jambazi kabisa
- tafuta mwanamke wa kichagaa
-jiunge team lowassa.
-anzaa udalali wa papuchi za watoto classic wazuri sio kina watoto wanuka mbu.nye
-anzaaa kwa babaa askofuu gwajima au matransfomaa
 
MBINU ZA BIASHARA

SIRI YA UTAJIRI

JIBU LA KWA NINI WATU WENGINE NI MASIKINI NA WENGINE NI MATAJIRI

Watu wengi wanajiuliza, "Siri ya utajiri ni nini?" Jee ni mbinu gani zinaweza kumsaidia mtu kupata utajiri? Siri kubwa ya utajiri ni kujifunza elimu ya namna ya kutafuta mtaji, kuwekeza kwa busara kwa namna ambayo daima panakuwa na ziada na faida. Kwa bahati mbaya sana, elimu hii haifundishwi darasani ila wanayo wafanyabiashara wachache na kila anayefanikiwa kujifunza siri hii huwa tajiri na huendelea kuificha. Kwa bahati nzuri, katika utafiti wagu nimeweza kuigundua siri ya utajiri. Kwa kuwa ninapenda wasomaji wangu waweze kufanikiwa na wapate manufaa kwa kununua kitabu hiki nimeamua kuiweka siri hii wazi:-

- Siri ya kwanza ya kuelekea ukwasi ni kubuni mradi unaojipa, yaani unaoweza kuitoa ziada na faida.
- Siri ya pili ya kuelekea kwenye utajiri ni kujifunza na kujenga tabia ya kuweka akiba
- Siri ya tatu ni kuwekeza fedha hizo za akiba katika vitega uchumi ambavyo vinazalisha faida endelevu.
- Siri ya nne ni kujifunza namna ya kufanya biashara na kuanzisha biashara yako ili iwe indelevu.

Kuna njia mbili za namna ya kupata utajiri zenye uhakika. Njia ya kwanza ni njia ndefu ambapo wataalamu na watafiti wa masuala ya fedha wameigundua njia hii ni rahisi kuifuata kwa sababu haihitaji uwe na kipato kikubwa, wanashauri kwamba ujenge tabia ya kuweka akiba, anza kuweka akiba ya T.shs 1,000 kila siku sawasawa na TShs 30,000 kwa mwezi, matokeo yake ni kwamba kama utaweka akiba yako kwa kipindi cha miaka 65 bila riba yoyote utakuwa na akiba TSshs 23,725,000 (Milioni Ishirini na Tatu Mia Saba Ishirini na Tano Elfu). Kama utawekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa kila mwaka itazaa na kukuletea TShs 2,750,000,000 (Bilioni Mbili na Milioni Mia Saba Hamsini).

Hesabu hii inaweza ikakutisha na usiamini macho yako lakini hiyo ni siri ya nguvu ya hesabu na riba kama alivyozielezea mwanafizikia Enstein kwamba katika dunia hii hakuna kitu chenye nguvu kama hesabu za riba. Pengine njia hii inaweza kuwa ni ndefu sana na ya kukatisha tamaa. Wengi wetu hatuwezi kusubiri muda mrefu. Hivyo tungependa kuwa na mafanikio ya kiuchumi kwa haraka. Lakini nasisitiza kama kipato chako ni kidogo anza leo kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku.

Dundulizo la akiba hii hukutiririshia utajiri bila wewe kukusudia kwani utaweza kukidhi hitajiko la ghafla kama kuugua safari ya dharura gharama za likizo na hata kutumia mbinu hii kama mpango wa elimu kwa watoto wako iwapo utawaanzishia hivi mara tu kila mmojawapo anapozaliwa au unaweza kuutumia kama upanga wa siku zijazo kwa mirathi ukianza hivyo leo kwa kupangilia namna hiyo kwa kila kusudio lako la baadaye.

Hebu tuangalie njia ya pili.
- Njia ya pili ya mkato ni kuongeza kiwango cha kuweka akiba kama wewe ni mtu mwenye shughuli za kuzalisha ziada. Kipato chako kinaweza kuwa kinaongezeka kila mara. Badala ya kuweka akiba ya TShs 1,000 kwa siku jiwekee malengo ya kuweka akiba ya TShs 10,000. Anza kwa kutenga asilimia 10% ya mapato yako hadi utakapofikia lengo la TShs 10,000 au zaidi kwa siku. Badala ya lengo lako kutimia kwa miaka sitini na tano (65) litatimia haraka zaidi. Kwa mfano ukiweka akiba ya TShs 10,000 kwa siku kwa muda wa miaka sita na miezi sita bila riba yoyote utapata TShs. 23,725,000. Ukiwekeza fedha hiyo na kupata riba ya asilimia 10% kwa miaka sita na miezi sita utapata TShs. 33,917,505.78. Kama fedha hiyo utaendelea kuweka akiba kwa riba hiyohiyo hadi kufikia muda wa miaka kumi utapata TShs. 63,112,201.43.

Kwa kuwa kitu cha muhimu hapa ni kuweka akiba na kuwekeza akiba hiyo katika kitegauchumi chenye kutoa faida kubwa, utajiuliza jee uwekeze kwenye kitega uchumi chenye kutoa faida kiasi gani? Wataalamu wa mambo ya fedha wanashauri kuwa uwekeze fedha yako kwenye kitegauchumi chenye kutoa faida ya angalau asilimia 10% Kwa mfano unaweza kuwekeza kwenye Akaunti ya TAJIRIKA ya Standard Chatered Bank" inatoa riba ya asilimia kumi 10% pia unaweza kuwekeza kwa kununua hisa katika soko la hisa na mitaji.
Kwa wastani wa watafiti wa masuala ya fedha viwango vya mapato yatokanayo na hisa kwa gawio pamoja na kukua kwa mtaji ni zaidi ya asilimia 11% ambayo ni makubwa kwa kiwango cha kawaida cha asilimia kumi (10%).

Baada ya kueleza siri ya namna ya kupata utajiri nitazitaja njia zingine ambazo zinaweza kukuwezesha kuwa tajiri.
1. Unaweza kurithi mali na fedha kutoka kwa wazazi wako. Hii ni njia ya kubahatisha kwani watu matajiri siyo wengi na hivyo watoto wenye bahati kama hii ni wachache pia.
2. Unaweza kusomea ujuzi au utaalamu katika fani yenye malipo mazuri na kujiajiri mwenyewe. Kwa mfano, unaweza kusomea fani kama ya Uanasheria, Uhasibu na Udaktari au ufundi / sanaa na kadhalika.
3. Unaweza kuanzisha biashara yako na kuiendesha ili kupata ziada kubwa.
4. Unaweza kuendeleza vipaji vyako na kuwa mwanamichezo au msanii wa kulipwa.
5. Unaweza kutunga vitabu juu ya suala lolote unalolijua. Kwa mfano, kama wewe ni mtu uliyebobea katika masuala ya muziki unaweza kutunga kitabu kinachofundisha watu namna ya kuwa mwanamuziki. Watunzi wengi wa vitabu ni matajiri wakubwa. Hii ni kazi unayoweza kuifanya mara moja lakini ukavuna matunda yake kwa muda mrefu sana.
6. Unaweza kuwa mbunifu na kuanza kuuza mawazo yako au kutumia chombo ulichokibuni kukuingizia fedha.
7. Unaweza kucheza bahati nasibu na kushinda.

Tatizo hapa soko na wateja wa aina hii ya huduma ni haba. Hiki ni kitu cha kubahatisha na nimekitaja makusudi ili kuwapa onyo wasomaji kwani watu wengi wanapenda sana kucheza michezo ya kubahatisha.
Uwezekano wa kutajirika kwa njia hii ni mdogo sana. Hivyo, nawashauri wasomaji kuachana na njia hii ya kutafuta utajiri. Nawashauri wachague njia yoyote inayofaa na inawezekana kwa kufuatana na mazingira yanayomzunguka mtu husika. Mkulima au mfugaji anaweza kuzingatia fani hii na kutajirika sana. Kwa kweli hakuna mipaka, hasa hapa kwetu Tanzania kwa sababu ya wingi wa fursa za kuweza kujishughulisha na kuwa tajiri.

Maelezo ya kina juu ya aina ya biashara au mbinu unaweza kuzitumia kutafuta na kupata faida utayapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Inawezekana kuwa tofauti kati ya mtu tajiri na mtu maskini inatokana na kile tulichojifunza kutoka kwa wazazi wetu. Wazazi maskini huwaambia watoto wao wajitahidi kusoma sana ili wapate maksi nzuri darasani na ili baadaye waweze kupata kazi nzuri. Wakati wazazi matajiri huwapa watoto wao elimu ya namna ya kutafuta fedha.

Kwa kawaida tukiwa shuleni tunapewa ripoti ya masomo. Katika maisha tunatakiwa kuwa na ripoti yetu ya maisha nayo ni orodha ya mali tulizonazo ikiwa ni pamoja na elimu ya kuzaliwa na ya kusomea na fedha taslimu zile zilizo katika hifadhi mbalimbali.
Kwa kufuata tafsiri ya Umoja wa mataifa mtu masikini ni yule ambaye kipato chake hakizidi TShs 1,000 kwa siku.
Inawezekana kuwa mfumo wa kifedha wa mtu maskini ni mfumo ambao humfanya kutumia kipato chake chote kulipia matumizi huwa hana ziada wala uwezo wa kuweka akiba hana madeni na hana mali.

Mfumo wa fedha wa mtu mwenye kipato cha kati ni mfumo ambao humfanya kuwa na mali kama magari, nyumba na kadhalika. Mara nyingi mali hizo huwa zinapatikana kwa mikopo na hutumia mshahara kulipia matumizi na madeni, hasa kama madeni ni makubwa, mtu mwenye kipato cha kati anapaswa kumuona mshauri wa maswala ya biashara.

Hatua anazoweza kuchukua ili kujikwamua na tatizo la madeni anaweza kulazimika kuuza baadhi ya mali zake ambazo amezinunua kwa kutaka kuonyesha ufahari tu na ambazo hazina umuhimu. Kwa mfano kama mtu ana magari matatu ya kutembelea, anaweza kuuza magari mawili kubaki na gari limoja na fedha atakayoiokoa kuiwekeza au kutumia kama mataji na kuanzisha biashara ili kujiongezea kipato.

Mfumo wa mtu tajiri ni mfumo ambao unamwezesha kuwa na biashara yake, kumiliki mali nyingi, kuwa na fedha nyingi katika akiba na awe ameziwekeza kwenye vitega uchumi vinavyolipa faida kubwa zaidi ya asiliamia kumi, kama vile nyumba za kupangisha na hisa. Mtu huyu hana wasiwasi na maisha. Anaweza kusafiri au kuugua lakini vitegauchumi vyake vinaendelea kumwingizia fedha. Siri kubwa ya matajiri ni uwezo wa kutumia fedha na kuziwekeza kupata faida kubwa.

Hiki ni kitabu cha vitendo. Yote unayoyasoma humu inabidi uyafanyie kazi ili yakusaidie. Tofauti kati ya maskini na tajiri iko katika kuchukua hatua. Tajiri hujifunza mambo ya kumwendeleza na kuchukua hatua kwa kutekeleza kwa vitendo yale anayojifunza na anayoyaona yanaweza kumuinua kiuchumi. Maskini huwa anajifunza mambo na kuyaacha kichwani bila kuchukua hatua au kuyafanyia kazi aliyojifunza na hivyo fursa ya kupata utajiri inampita hivihivi. Kwa hiyo, kama unataka kuwa tajiri anza mara moja kufanya yafuatayo:-

1. Anza kuweka akiba ya T.Shs 1,000 kila siku. Tengeneza kisanduku na tumbukiza TShs. 1,000 kila siku. Zikifika TShs. 50,000 kafungue akaunti ya TAJIRIKA, kwenye Benki ya "Standard Chatered". Kisha endelea kuweka TShs. 30,000 kila mwezi. Jinsi mapato yako yatakavyokuwa yanaongezeka tenga asilimia kumi (10%) ya mapato yako uweke akiba kila mwezi. Lengo lako liwe ni kuweka TShs 10,000 au zaidi kila mwezi. Fedha unayoweka ni kama unapanda mbegu. Kumbuka hii ndiyo hatua ya kwanza kuelekea kwenye utajiri. Faida katika benki hii ni kubwa. Inaanzia asilimia 6.5% kwa kianzio cha TShs. 50,000 hadi TShs. 5,000,000 na asilimia 10% kwa kiwango kinachozidi TShs. 10,000,000. Fedha utakazoziweka huko usiziguse mpaka ukiona zimekuwa nyingi ndipo utaamua na kupanga ukaziwekeze sehemu gani.

2. Jifunze pia mbinu za kutafuta fedha. Njia rahisi ni ya uhakika ya kukuwezesha kufanikiwa kiuchumi katika maisha ni kutafuta mshauri au mtaalamu anayejua mbinu za uongozi wa biashara ili akushauri vizuri juu ya yale unayonuia kutekeleza.

3. Inawezekana pia bado hujawa na biashara ya aina yoyote. Kama ndivyo anza kufanya utafiti kuona utafanya biashara gani. Mawazo ya biashara gani ufanye unaweza kuyapata katika sehemu ya pili ya kitabu hiki. Kila mara hakikisha unatenga asilimia 10% ya mapato yako na kuweka kwenye akaunti yako ya TAJIRIKA. Kumbuka kwamba kuwa na biashara yako ni siri ya pili ya kuelekea kwenye kupata utajiri. Kama unayo biashara yako unaweza kumtafuta mtaalamu wa biashara kuangalia jinsi unavyoweza kuiboresha au kuipanua.

4. Panga malengo ya muda wa mwaka mmoja miaka mitano na miaka ishirini ili kuhakikisha kwamba unajikomboa kiuchumi. Malengo yako makuu yawe ni:- kuwa na akiba ya fedha za kutosha katika akaunti yako , kuwa na biashara yako, na vitega uchumi vya aina tofauti ambavyo unaweza kuvisimamia vizuri.

5. Kama wewe ni mwajiriwa, kipimo chako cha mafanikio kiwe ni kujiuliza swali, kama utaacha kazi yako ya mshahara utaweza kuishi kwa kutumia kipato chako cha pembeni kwenye biashara yako kwa muda gani? Mafanikio yako yatakuja pale utakapoweza kutumia kipato chako cha ziada bila kutegemea mshahara, na hapo ndipo unaweza kuacha kazi na kwenda kuimarisha biashara zako au kuendelea na kazi huku pia ukijiimarisha kibiashara.

6. Kama utafuata mpango wa namna hii na kujituma kwa juhudi na maarifa kwa muda wa miaka mitano (5) unaweza kuwa tajiri na maisha yako yanaweza kuwa mazuri.



Haya kazi kwako!!

 
Siri ya utajiri ni ubahiri(li).
Hakikisha kidogo ukipatacho kinakuwa saved, punguza matumizi yasiyo ya ulazima kama kunywa pombe, kuchangia sana mambo yasiyo ya msingi yanayopelekea kupoteza pesa kama vikao vya harusi mbalimbali, party nyingi za marafiki kama birthdays.
Tafuta biashara ndogo ya ziada ya kuanzia kukuza pesa yako, fanya utafiti wa mahali unakoishi kuna opportunity gani ya biashara.
Well, utajiri kama wasemavyo wengi kama Warren Buffet ni kwamba,
''save more than you can spend'' ama
''spend what is left after saving''.
 
Jamani kama kichwa kinavyojieleza. Nauchukia sana umaskini, siupendi umaskini,nimefanya kazi sana za kuajiriwa na huu ni mwaka wa kumi lakini sitajiriki. Nifanyeje?

Tafuta wazo zuri la biashara then kachukue mkopo!...
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom