Jinsi ya Kuwa Balozi wa Tanzania: Siasa, Ujasusi na Ujuzi wa Kiufundi

JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
7,204
15,278
Wakati Bongo, kuchaguliwa kuwa balozi, wanaangalia uchawi wako, ukada wa chama tawala, au uswaiba tu, kwa wenzetu ni strategies zinatumika, wanajua kabisa Bongo ni super power kwa Afrika Mashariki, na ina maslahi mapana wanayoyahitaji, wanajua Rais ni mwanamke, tena Islam, wanakuletea mwanamke mwenzio, tena Islam Swala Tano kama wewe, akija kuongea na wewe, kwanza hapo ni Asalam Aleikum Nyingi, she has something in common with the president, hapo Raisi anaweza akafunguka vizuri tu, na ujasusi utafanyika vizuri.

Kawaida mabalozi huwa ni majasusi, au wenye uwezo wa kufanya ujasusi, kama Balozi wa USA Bongo, alikuwa mchungaji, tena ni afisa wa jeshi mstaafu, sio Bongo unampeleka Hoyce Temu Ulaya kuwa balozi, kikubwa alicho nacho ni taji la umis na ujasiliamali wa kiwango cha chini.

Balozi pereka mtu aliyebobea kwenye siasa (pole pole), kwenye sayansi, usalama.
 
Hapo umechukua mfano mmoja mdogo ila ukweli ni kuwa haya unayoyasema nasi tunayafanya sana
Mabalozi wengi wamekuwa ni watu bright na wenye ushawishi,Rwanda waliwahi kumkataa Balozi wa Tanzania na kusema ni Jasusi na hao wamarekani au Waingereza wanaokuja huwa tunajua sana profile zao na namna ya kudeal nao
 
Hatuwezi kufahamu yote, unajua mtu ni miss kumbe ana jukumu jingine kitambo, lazima tufikiri tofauti Sasa
wengine ni warembo, wanamuziki, wachezaki mara paap mtua anachaguliwa kwenye nafasi nyeti ya kisiasa, maswali tele tunajiuliza kwa uwezo upi alio nao? Kumbe wale tayari walikuwa undercover
 
Mnamkumbuka balozi wa marekani aliyeitwa Calucci enzi za kuundwa muungano wa tanganyika na zanzibar. Halafu rejeeni na huyu balozi wa sasa wa marekani nchini kenya na sakata la ushoga kenya. Marekani ina mabalozi very bright nchi za nje waliobobea kisiasa na kijasusi kiasi cha kufanya manuever kwenye nchi walikopelekwa kuiwakilisha nchi yao, sisi tunapeleka warembo na watu wengine wasiojulikana weledi wao
 
Unamjua vizuri Hoyce Temu au unaongea Kwa usilo lijua idara ya usalama ya Tz yaani TISS usifananishe na ya Uganda Rwanda au Kenya. Wakati DIWANI ATHUMANI anateuliwa kuwa DG wa TISS hata boss wake Simon siro alishangaaa hiii imekuwaje????
 
Back
Top Bottom