Jinsi ya kuutunza mwili kupunguza tumbo na kupunguza mafuta | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jinsi ya kuutunza mwili kupunguza tumbo na kupunguza mafuta

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Mar 1, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Hii sio ya kitaalamu bali ni mimi ninavyofanya na ndio inayonisaidia kupunguza tumbo.
  Kwasababu vitu vya formula mimi huwa siwezi kuvifuata na huwa naviona vigumu sana kwahiyo huwa najaribu kuishi vile ninavyoweza.

  Na kizuri zaidi ni kwamba hii sio diet ya kujinyima.
  Ila unaweza usifanikiwe pia kutokana na mwili wako kwakua tumeumbwa tofauti lakini unaweza kujaribu kama itafanya kazi

  [​IMG]Tukianza na asubuhi nikiamka mimi kama Mzizimkavu, naanza kunywa maji glass 3 ya Uvugu vugu kabla ya kupiga mswaki.
  Na nikiisha amka nakunywa maji ya uvugu vugu yaliokamuliwa ndimu au limao glass zingine tatu kabla ya kunywa Chai.
  Ukizoea maji ni matamu kuliko hata Bia
  Kuwa Teja wa Maji kuna raha yake pia

  [​IMG]Mimi napenda vitu vichachu kwahiyo maji saa zingine naya hisi kama yamepooza ila nikikamulia ndimu/limao kwenye maji ya uvuguvugu hata nisipoweka sukari yanaleta ladha fulani hivi
  Ukiweza kunywa maji ya uvugu vugu kila wakati unapohisi kiu ya maji itakuwa vizuri au hata mara tatu kwa siku angalau

  [​IMG]Si mpenzi sana wa Chai kwakuwa sipendi kabisa vitu vya sukari, lakini siku ninapo amua kunywa chai huwa nakunywa yenye tangazwizi nyingi sana na badala ya kutumia sukari huwa naweka asali...... Ila unaweza kutumia viungo vingine mbali mbali vya ki pwani (masala)


  [​IMG]Asali


  [​IMG]Kwa kifungua kinywa Sausage za kuchemsha au kama utakaanga iwe kwa mafuta yasiozidi kijiko kimoja kikubwa cha kulia (nashauri ya alizeti au olive)

  [​IMG]Mayai ya kuchemsha si mabaya pia kwa kufungua kinywa
  Kumbuka mimi huwa sifanyi diet hivi ndivyo ninavyokula na inasaidia

  [​IMG]Badala ya kutafuna Sambusa, Popcorn na cookies au chocolate kila wakati bora muda wako uelekeze kwenye matunda, kama huwezi kupitisha lisaa bila kuweka kitu mdomoni


  [​IMG]Mchana unaweza kupiga bakuli la mchemsho wa ndizi, ziwe Bukoba au za kule kwetu Moshi zote sawa kwakuwa mchemsho hauna mafuta kabisa unajilia kadri utakavyotosheka

  [​IMG]Kuku Choma ni chakula kingine ambacho kinanifaa nyakati za mchana, lakini haswa hupendelea Kuku wa kienyeji ambao hawakukuzwa kwa madawa
  Mara nyingi usiku naipotezea tu, pengine nalalia glass 2 za wine au beer kadhaa zisizozidi 3
  Au Kuku wa kienyeji wa kuchemsha aliewekwa chumvi na ndimu na ka ndizi kamoja ka kuchemsha au kukaanga kwa mafuta kidogo sana


  [​IMG]Ugali naupenda sana na huwa najiachia nao siku za kujiharibu
  Lakini kumbuka wanga sio kitu cha kukiendekeza sana hasa unapotaka kutoa kitambi
  Nikiona kinachomoza, napunguza maswala ya ugali.
  Japo kwangu ni ngumu siku ipite bila Ugali, ila kumbuka miili inatofautiana... naweza nikala ugali mwaka mzima mwingine akala wiki akafumuka
  So usinifatishe ila jaribu kupunguza au uepuke kama utaweza

  [​IMG]Tumbo liko hapa sasa!!!!!
  Hili ndio tatizo lililonikuta mpaka mkaona ile ishu imechomoka siku ya Birthday yangu


  Kwakweli chips ni tamu hasa kwa sisi tunaofanya kazi za usiku ukirudi umejichokea unavamia tu  Unakuta unafululiza hata mwezi unazila kisha unaenda kulala
  Japo tunapenda chips vumbi ila tuwe na kipimo isizidi, isiwe kila siku
  Ukijumlisha na bia, daaah!! dah!!!!!! dah!!!!! shughuli imeisha  No. 1 enemy kwa vitambi vya wanawake ni hii kitu
  Kula angalau mara moja kwa wiki tafadhali kama huwezi kuacha kabisa
  Wenye kuweza kufanya sit ups pia fanyeni japo najua mazoezi ni magumu sana na yanatia uvivu hasa unapokuwa na kazi nyingi  Maji ni kitu cha lazima na cha kila siku
  Ukiweza kunywa maji ya uvuguvugu Asubuhi, Mchana na Usiku utafanikiwa japo kidogo  Narudia hii sio Diet ya kitaalam ni jinsi ninavyo ishi mimi, jaribu kama utaweza kufanikiwa kwa wale walioniomba ushauri.
  Ila kama mwili wako ni mkubwa sana pia jaribu kupunguza kipimo cha chakula unachokula kila siku, ila usijinyime sana.

  Mboga mboga kibao kila siku ukiamua mchana na jioni. Ni muhimu sana

  Lady Jay Dee: JINSI YA KUUTUNZA MWILI KUPUNGUZA TUMBO NA KUPUNGUZA MAFUTA.........KUNAHITAJI VITU VINGI TOFAUTI NA VYA ZIADA ILI KUPATA SHAPE UNAYOIPENDA

   
 2. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #2
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,713
  Trophy Points: 280
  Asante mzizimkavu ngoja nijaribu maana daah
   
 3. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #3
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Mkuu hii shule nameipenda sana , asante sana
   
 4. Preta

  Preta JF-Expert Member

  #4
  Mar 1, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 24,113
  Likes Received: 3,036
  Trophy Points: 280
  Tatizo langu lipo hapa.....hata nifanyaje kuacha hii kitu inaniwia ngumu.....kitambi karibu kinanifika magotini....sijui nimelogwa....?

  [​IMG]
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Mar 1, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,633
  Trophy Points: 280
  Mzizimkavu,

  Asante kwa darsa,vipi mbona mnyama wa taifa haujamzungumzia kabisa ?.
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Mkuu umekusudia Mnyama yupi wa Taifa? Ng'ombe? Nyama ya Ng'ombe ina madhara bora ule nyama ya kuku kuliko kula nyama ya ng'ombe au Kitomoto nyama zote zina madhara ila nyama ya kuku ndio bora inafaa kuliwa wakati wote mkuu.
   
 7. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #7
  Mar 1, 2012
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Mkuu Mzizimkavu, nakupa big-up sana!! Kuna siku uliweka uzi sikumbuki ulikuwa unahusu nini ila nilibeba contents mhimu zilizokuwa zinanihusu! ambazo ni kunywa maji ya uvugu uvugu asubuhi kabla ya kuamka. Nimefanya hivyo kwa muda wa mwezi sasa na nimezoea. Siwezi kuamka asubuhi tena bila kupata maji ya uvugu uvugu, yananisaidia sana, nilikuwa nadalili za kufumka kitambi huko nyuma, sasa kinapotea ghafla, huwezi kuamini nimeloose weight 2 ~ 2.5kg ndani ya huu muda bila kufanya mazoezi.
  Vitu vitamu vitamu haswa vyenye sukari nimepunguza, nikitaka juice nakamata ya chungwa au limao! hapa nilipo zinapatikana kwa urahisi kwa hiyo siyo shida. Mwisho, ni vizuri kwa kila mtu kujifanyia uchunguzi mwenyewe na kujua ni misosi ipi inamfanya awe hivi au vile ili kuimarisha afya zetu. Once more, thanks for your useful posts on the forum.
   
 8. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #8
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280

  Ha ha ha ha haaa mkuu kweli jamaa hajaongelea hiyo kitu bana
   
 9. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #9
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  mi maji nikinywa asubuhi natapika mzizi why?
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Nyama ya Nguruwe  BWANA Yesu hakula kabisa nyama ya nguruwe. Alifuata barabara sheria za Musa na hivyo hakula nyama ya nguruwe. Katika Walawi 11: 7 – 8, inasema: "Nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hacheuwi; kwenu huyo ni najisi. Kwa

  Sababu wanyama hao ni najisi msile nyama yao wala msiguse mizoga yao
  "[1]. Mahusiano ya Yesu na nguruwe ni kule kutoa kwake ruhusa kwa majini walio najisi waliokuwa wamemuingia mtu kuwaingia wao (yaani nguruwe). Walipowaigia

  kundi la nguruwe, walikimbilia majini na kuzama humo. Hata hivyo, watu wengi wanaojiita Wakristo leo sio tu wanakula nyama ya nguruwe, bali wanaipenda sana nyama hiyo mpaka wamewafanya nguruwe kuwa ndio somo la nyimbo za

  mahadhi kwa shule za chekechea. Kwa mfano, (This little piggy went to the market …Nguruwe huyu mdogo amekwenda sokoni) na hadithi za watoto (kwa mfano, The Three Little Pigs … Nguruwe Watatu Wadogo). Nguruwe wa

  Nyama ni katuni mashuhuri, na hivi karibuni sinema kamili ilifanywa kuhusu nguruwe aliyeitwa "Babe – msichana mdogo". Hivyo, inaweza kusemwa kuwa wale wanaojiita wafuasi wa Yesu kwa hakika hafuati njia na mwenendo wa Yesu.
   
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Pole sana jaribu kunywa maji ya Uvuguvugu yaliyochanganywa na kijiko kimoja cha asali inshallah huta tapika.
   
 12. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #12
  Mar 1, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Jamaa hajaongelea juu ya SAMAKI vipi?
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Samahani nilisahau Samaki nawapenda sana faida zake ni hizi hapa chini


  SAMAKI (FISH)

  • Huyayusha damu, huifanya kuwa nyepesi
  • Huilinda mishipa ya damu isiharibike
  • Huzuia damu kuganda
  • Hushusha shinikizo la damu
  • Hupunguza hatari ya kupatwa na mshituko wa moyo na kiharusi
  • Hutuoa ahueni kwa wenye ugonjwa wa kipandauso
  • Husaidia kuzuia uvumbe mwilini
  • Huendesha mfumo wa kinga ya mwili
  • Huzuia saratani
  • Hutoa ahueni kwa wenye pumu
  • Hupambana na dalili za awali za ugonjwa wa figo
  • Huongeza nishati ya ubongo
   
 14. Smile

  Smile JF-Expert Member

  #14
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 15,427
  Likes Received: 194
  Trophy Points: 160
  sawa mkuu nitajaribu.maana naona unene unanianDAMA MWENZENU NINA KG 73
   
 15. salito

  salito JF-Expert Member

  #15
  Mar 1, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 1,365
  Likes Received: 352
  Trophy Points: 180
  Asante kwa somo zuri mkuu
   
 16. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #16
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280

  Tukizama kwa makini tutaona ya kwamba Dini zote zimeharamisha nguruwe. Mfano tazama katika Biblia (Agano la Kale), Kitabu cha Walawi: "Na nguruwe msimle; ana kwato zilizogawanyika lakini hachuei; kwenu

  huyo ni najisi. Kwa sababu wanyama hao ni najisi msile nyama zao wala msiguse mizoga yao" (11: 7 - 8). Na katika Kitabu cha Isaya: "Mwenyezi Mungu asema hivi: 'Wapo watu waaojitakasa na kutawadha wapate

  kuingia katika bustani za ibada za sanamu; wanafanya maandamano na kuhani akiwa kati yao. Watu hao hula nguruwe, panya na vyakula vingine haramu'"(66: 17).


  Na katika agano jipya, Yesu anasema: "Msidhani kuwa nimekuja kutangua sheria na mafundisho ya manabii. Sikuja kutangua bali kukamilisha" (Mathayo 5: 17).  Na Qur-aan ipo wazi kabisa kuwa nyama ya nguruwe haifai kuliwa. Allaah Anasema:
  "Yeye Amekuharimishieni mzoga tu na damu na nyama ya nguruwe na kilichotajiwa, katika kuchinjwa kwake, jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu" (2: 173).
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Ukishindwa kunywa Maji ya Uvuguvugu na Asali kijiko kimoja na limau moja kubwa wakati wa asubuhi unapo amka kunywa Glasi moja ya Mtindi kila asubuhi mchana na usiku kwa muda wa miezi 6 utapunguwa huo unene.
   
 18. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #18
  Mar 1, 2012
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,640
  Likes Received: 1,429
  Trophy Points: 280
  Mkuu maji ya uvugu vugu unamaanisha yaliyochemshwa yakapoa kidogo au unamaanisha maji ambayo hayajawekwa kwenye jokofu?
   
 19. Ndokeji

  Ndokeji JF-Expert Member

  #19
  Mar 1, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 525
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  hapo mkuu ni kweli kabisa nafikiri lazima watu wa kawaida tumekuelewa mtu asipokuelewa hapo atakuwa abnormal kwa maana anafikira nyingi kupita kiasi au ndogo kupita kiasi
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Mar 1, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,615
  Trophy Points: 280
  Maji ya Uvuguvu ni yale yaliyochemshwa yakapoa kama dakika moja toka yatoke jikoni kwa kizungu wanayaita (Warm Water) kama sijakosea.
   
Loading...