Jinsi ya kuunga maharage yenye ladha nzuri

leaht

New Member
Jun 5, 2013
1
1
Habari wanaJF,

Naomba kwa yeyote anafahamu jinsi ya kuunga maharage matamu yenye radha nzuriiii anisaidie kwani ujuzi unatofautiana.

Asante..
 
Yachemshe yaive ,kaanga kitunguu kikiiva tia nyanya ikiaanza kurojeka weka karoti kidogo na chumvi kaanga kisha weka hoho kaanga kisha yachuje maji yatie humo kaanga hiyo supu ya maharage korogea royco mchuzi mix kisha malizia acha yachemke kwa moto mdogo ili supu ipungue ipua tayari kwa mlo,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,
 
NIpikavyo mimi Rubi!

Mharage makavu kilo moja!

nikijua kesho napika maharage. nayachambua jioni kuondoa taka kisha nayaosha nayaroweka usiku wote kesho yake muda wowote nitakaoona unafaa nitayasuuza kisha kuweka kwenye sufuria na kubandika jikoni ndani ya saa moja yatakuwa yameiva. kama ni maharage mabichi hayaitaji kurowekwa.

Wakati yakikaribia kuiva naweka chunvi na pia nahakikisha supu yake haikaukii maana ndio mchuzi wenyewe.

yakishaiva chukua sufuria safi kwa ajili ya kuunga.

Njia mbalimbali za kuunga maharage nizipendazo mimi maana najua kila mtu ana njia yake. hiyo hapo juu mimi siiwezi.

1. njia rahisi kama maharage yameiva bila kubadilisha chombo waweza katia kitunguu, weka na mafuta kidogo kisha funika vichemke vichanganyane vizuri. Vitunguu vikianza iva koroga ule mchangayiko wako kisha tia hoho na pilipili mbuzi nzima ambayo haijapasuka vichemkie pamoja kama dk 4-5 kwa ajili ya kuogeza radha, ipua tayari kwa kuliwa.

N.B. ukipenda wakati vitunguu vinachemka waweza tia nazi kama wapenda.

2. kaanga kitunguu chako (napendelea vitunguu vingi kidogo) hakisha hakiungui wala hakibadiliki rangi kisha weka maharage bila supu, geuzageuza mchanganyiko wako uchanganyike vizuri kisha weka supu vikianza kuchemka na mchanganyiko ukiwa umechanganyika vizuri weka hoho, na karoti kiasi na pipipili mbuzi nzima, acha vichemke kidogo kisha ipua tayari kwa kuliwa. waweza pia weka nazi ukipenda.

3. kaanga kitunguu chako pamoja na nyanya moja isiwe kubwa sana baada ya hapo weka maharagwe yako fanya kama No. (2)

4. Kaanga kitunguu chako pamoja na nyanya vikishalainika weka karanga koroga hilo rosto la karanga mpaka uhakikishe limeiva na bila kushika chini kwenye sufuria, weka maharage yako geuzageuza vichanganyike vizuri kama dk3 kisha weka supu yake ambayo utakuwa umeihifadhi pembeni vikichemka vizuri weka hoho acha kama dk 3. kisha ipua tayari kwa kuliwa.

FAIDA ZA KUROWEKA MAHARAGE MAKAVU KABLA YA KUPIKA.

1. Hupunguza sumu iliyoko kwenye ganda ambayo husababisha uoni hafifu.
2. hufanya maharage yanaiva vizuri na kwa muda mfupi bila kupasukapasuka
3. huongeza radha, maharage yaliyorowekwa huwa na radha nzuri zaidi kushinda ambayo hayajarowekwa.
4. hupunguza gharama ziwe za mkaa, kuni, gesi au umeme, tena kwa wale ambao wana pressure cooker muda huwa mfupi zaidi.

-VILEVILE MIMI SIPENDELEI KUWEKA NYANYA NYINGI KWENYE MAHARAGE KWA SABABU YANAKUWA NA LADHA YA UCHACHU NA NI RAHISI KUCHACHA.

- NAPENDELEA PIA KUWEKA HOHO NA KAROTI MWISHO WA MAPISHI YANGU YOYOTE ILI ZISIIVE SANA NIPATE ILE FAIDA NA LADHA ILIYOMO KWENYE HOHO NA KAROTI.

KARIBU TULE:

 
Me napendelea kupika maharage ya nazi ni mazuri tu
Kwa kipimo cha kg 1 utahitaji vegetable vifuatavyo
1)kitunguu maji kikubwa 1
2)nyanya 3 kubwa
3)pilipili hoho 1 ukubwa kiasi
4)karoti 1
5)vitunguu thomu chembe 10-15
6)tangawizi kiasi(husaidia kuondoa gesi)

Chemsha maharage mpaka yawe laini then katakata vegetable zako then weka kwenye sufuria yako

Add tui lako na subiria kwa dakika 15 yatakua tayar kwa kuliwa.
 
Kwangu maharage huwa siweki mbwembwe.....

Nachemsha maharage hadi yaive.... Yasikauke plz

Then naweka kitunguu maji na tangawizi unaacha yachemke kidogo ( mara moja moja ili kubadili ladha natia manjano mabichi)

Kisha natia tui bubu/zito na chumvi

Yachemke tui likiiva tayari kwa kuliwa....

Wali maharage mtamuuuuuuu
 
habari wana JF ,Naomba kwa yeyote anafahamu jinsi ya kuunga maharage matamu yenye radha nzuriiii anisaidie kwani ujuzi unatofautiana.asante

nyanya inachachua maharage shoga na kama mtu ana vidonda vya tumbo ndo unamuumiza zaidi. hakikisha harage lako umelichemsha likaiva vizuri na kulainika,kicha chukua sufuria weka mafuta kidogo kwani mafuta mengi nayo ni ugonjwa,yakichemka weka vitunguu kaanga viwe brown kisha weka karot then hoho ukipenda , vikiiva weka maharage yako yaache yachemke hadi maji yake yakaukie kidogo bila kusahau chumvi kiasi then tayari kwa kuliwa ukitaka kunogesha zaidi waweza weka tui moja tu zito la nazi hakikisha linachemka na usifunike litakatika.
ila asikudanganye mtu kupika maujanja yako waweza jaribu spice yeyote as long as kitakuwa kitamu na si kichungu kuliwa
 
Me napendelea kupika maharage ya nazi ni mazuri tu
Kwa kipimo cha kg 1 utahitaji vegetable vifuatavyo
1)kitunguu maji kikubwa 1
2)nyanya 3 kubwa
3)pilipili hoho 1 ukubwa kiasi
4)karoti 1
5)vitunguu thomu chembe 10-15
6)tangawizi kiasi(husaidia kuondoa gesi)

Chemsha maharage mpaka yawe laini then katakata vegetable zako then weka kwenye sufuria yako

Add tui lako na subiria kwa dakika 15 yatakua tayar kwa kuliwa.
Tangawizi sio kuondoa gesi tu pia inafanya maharage yawe na lsdha nzuri sana.
 
Me napendelea kupika maharage ya nazi ni mazuri tu
Kwa kipimo cha kg 1 utahitaji vegetable vifuatavyo
1)kitunguu maji kikubwa 1
2)nyanya 3 kubwa
3)pilipili hoho 1 ukubwa kiasi
4)karoti 1
5)vitunguu thomu chembe 10-15
6)tangawizi kiasi(husaidia kuondoa gesi)

Chemsha maharage mpaka yawe laini then katakata vegetable zako then weka kwenye sufuria yako

Add tui lako na subiria kwa dakika 15 yatakua tayar kwa kuliwa.
Tangawizi sio kuondoa gesi tu pia inafanya maharage yawe na ladha nzuri sana.
 
yechemshe na chumvi yakiiva kati viungo vyote i mean kitumguu karot na hoho wakati viungo vinaanza kuivia humo tia tui lanzani lichemkie humo hadi lianz kua zito hapo tayari maharagwe yatakua yameiva
 
Mimi huwa sikaangi maharage, nashkuru kwani kuna wengine hufanya kama mimi, Chemsha maharage yako na chumvi kiasi then yakianza kulainika katakata kitunguu maji, hoho,karoti(unaweza kukata mtindo wa box au kuzisaga), na iliki au tangawizi au vyote kwa pamoja hizo iliki usizitwangwe ziweke nzima kama punje nne kwa maharagwe nusu then baadae utaziondoa, tangawizi ukishasaga au kutwangwa ichuje,weka viungo vyote hivyo kwa pamoja,. kama hutumii nazi kama mimi unaweza kuweka maziwa fresh, funika bila kuyakoroga then baada ya dk 15/20 unaweza kuyacheck kama viungo vimeiva vizuri koroga na hapo yanakua tayari,NB mimi sipendi kuweka mafuta kwenye maharage thats why sijayataja.Enjoy!:)
 
Yachemshe yaive ,kaanga kitunguu kikiiva tia nyanya ikiaanza kurojeka weka karoti kidogo na chumvi kaanga kisha weka hoho kaanga kisha yachuje maji yatie humo kaanga hiyo supu ya maharage korogea royco mchuzi mix kisha malizia acha yachemke kwa moto mdogo ili supu ipungue ipua tayari kwa mlo,,,,,,,,,,,,,,, ,,,,,,,,,,,,,,
mashallah nimekuelewa
 
Kuna aina nyingi za kuunga maharage kulingana na endow husika na upatikanaji wa viungio
 
Back
Top Bottom