Utunzaji wa nywele za asili

Labda ukiosha uweke shampoo zaidi ya mara moja.

Me ata sina mda wa kushuhulikia nywele naosha nachana nabana au siku nyengine sichani kabisaaa 🤣
The same. Naona ukianza kuzitia midawa ya kuosha au kukuza ndio zinaenda kuharibika..zinakua zinahitaji utumie kila siku
 
Njia ni nzuri na inasaidia sana ktk kukuza nywele...ila ili neno "nywere" litafanya watu wasifatilie mada kwa usahihi , wakakimbilia kuona ilo neno, si unatujua wabongo tena
 
View attachment 1231221
Jinsi ya kuandaa

* Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemea na na ukubwa wa kitunguu kimenye

* Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga

* Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi na uvichuje bila kuongeza maji.


Jinsi ya kupaka

Paka kichwa kizima na kisha uvae kofia ya plastic ambayo itasaidia kukupa joto zaidi.Kaa na kofia ndani ya saa 4-5 kisha utoe na kuziosha Nywere. Kwa matokeo mazuri zaidi fanya hivo mara 2au3 kwa mwezi
Four hours vitungu kichwani-hauna kazi nyingine. Kutunza nywele ili ziweje kwanza
 
Ulipokosea ni kusema tumia kofia ya plastic na unajua kabisa hakuna kofia ya hivyo otherwise utumie kondomu
 
Ukuzaji wa nywele za asili

Kwa wale ambao tuna nywele asilia a.k.a natural hair, tayari tunafahamu changamoto kadhaa tunazokumbana nazo.

Kwa wale mnaofikiria kuanza kuwa na nywele asilia,karibuni sana tuendelee kujuzana namna ya kutunza nywele zetu kama tulivyopewa na Mungu.

Katika mada ya leo,nitakwenda kuzungumzia vitu vya kuzingatia ili kuikuza nywele yako asilia kwa haraka zaidi.

Je,unazifahamu nywele zako vizuri? Una nywele za aina gani? Zina tabia gani?Zinataka nini?

1. Kuzikubali kama zilivyo na kuzipenda.

Utasikia ..hiki kipilipili changu ni steelwire ya kimataifa, ..hakitikisiki hata upepo wa dunia yote ungevumia pande hizi.

Mwingine oh..nywele zangu kama miti ya mibuyu kichwani…hazishikiki.Tatizo ni kwamba hamjafahamiana vizuri yani wewe na nywele zako.

Hata mimi niligombana nazo sana huko nyuma kabla ya kuzielewa vizuri. Jenga mahusiano mazuri tu na nywele zako, zielewe, ukifikia hapo utaanza kuzipatia hata hazitakusumbua.

2. Usafi wa ngozi ya nywele na nywele zenyewe.

Nywele zenye afya huanzia kwenye ngozi safi ya nywele.Nafahamu unataka nywele zako zisidumae kwa hiyo zioshe vizuri.

Wakati uliopita nilizungumzia kuziosha kwa product zilizo rafiki( ‘friendly’) .Ngozi safi ya nywele itasababisha nywele kupata njia ya kujitokeza nje kwa urahisi.

Unapoziacha chafu,ule uchafu unaziba matundu ya nywele zako na kuzuia njia,kama ambavyo matundu ya uso yakiziba unapata machunusi maana uchafu unajaa basi kwa nywele hazitakua vizuri.

3. Linda unyevu wa nywele zako

Kila mtu akisikia kiu hunywa maji.Nywele zako zinahitaji kulindwa zisisikie kiu.Unapoziosha,yale mafuta asilia ya kuzilinda huondoka na uchafu.

Nywele inabaki ikiwa na udhaifu fulani maana haiwezi hata kushikilia hayo maji yaliyopo vizuri,na zikikauka zinakua kavu sana.Ni vizuri kabla hazijakauka vizuri,ukazi-’condition’.

Kwa nywele ambazo ni nyepesi na chache, pia kuna product za kuzisaidia ziweze kutunza vizuri unyevu na hivyo kuwa na afya nzuri.

4. Zifahamu nywele zako

Yaani hapa ndo shule ilipolalia kabisaa maana ukizijua tu basi utazihudumia kwa usahihi.

Unatakiwa kuangalia namna gani nywele zako zinanyonya unyevu. Unajuaje?
Chukua kikombe, kijaze maji safi. Ukipata glass itakuwa vizuri zaidi.

Chomoa unywele mmoja kichwani, hakikisha unatoka na kale kamzizi kake keupe keupe hivi.

Tumbukiza unywele wako kwenye glass yako ya maji hakikisha imeingia yote.Kama ikizama hapo hapo na hainyanyuki tena, basi nywele zako zinanyonya unyevu kwa haraka kabisa.

Kama inachukua muda kuzama,au haizami kabisa,nywele zako zinanyonya unyevu taratibu au zinanyonya kwa shida. (Wala usihofu, zipo namna ya kuzifanya zinyonye unyevu kwa haraka, tutajuzana.)

Ni kwamba ‘cuticle’ zake zimefunga haswa, ndio maana unyevu au maji haviingii kwa haraka.

Kwa hiyo ukifanya ‘deep conditioner’ kwa kutumia joto kama la drier lakini uwe moto mdogo sana au ufanye ‘hot oil treatment’ itakusaidia ‘cuticle’kufunguka na unyevu kupita.

Mbadala, unaweza baada ya kuosha suuza na maji ya uvuguvugu halafu weka mafuta ya kimiminika.

Inasaidia sana. Mimi nina aina gani?..Nina nywele zinazonyonya unyevu haraka.

5. Mafuta ya Kupaka kichwani.

Ni ya muhimu mnoo!.Nimefanya utafiti wa kina nimeona mafuta ya nazi yanaweka afya nzuri kwa nywele aina nyingi hivyo na mimi nikaanza kuyatumia.

Kwangu mimi, mafuta ya nazi ya kutengeneza mwenyewe yamenikubali sana.

Japo huwa nanunua pia mafuta kama ya Zaituni Olive(extra virgin) na ya Tea tree.

6. Kuzichambua vizuri kabla ya kuchana.

Uwe mkarimu na mwenye subira kwa nywele zako.Mimi zikijifunga huwa nazichambua kwa mikono taratibu wakati mwingine nazilowesha na maji kwa mbali halafu nachana kwa chanuo lenye mapana sio ambalo reli zake zimebanana. sio kitana. Chanuo kubwa(wide toothed comb).

7. Usizisumbue mara kwa mara na usuke mitindo ya kuzitunza zikue.

Kama unataka zikue haraka,usizisumbue sana.Unaweza ukasuka mitindo mizuri tu ukakaa nazo wiki nzima au kadri zitakavyodumu.

Au upunguze kuzichana mara kwa mara lakini utafute siku kama wikiendi ukae uzichambue taratibu na vidole kuondoa mafundo.

Kuchana mara kwa mara zinapukutika, zinaanguka. Zitakua lakini sio kwa kasi ya kama ukizisuka ukaziacha kwa muda.

8. Punguza matumizi ya vitu vya moto kwenye nywele zako kama pasi ya nywele na vingine vya hivyo.

Mimi dryer la nywele situmii zaidi ya mara mbili kwa mwezi. Mara nyingi naziacha zikauke na hewa hata kama nimezifunga rollers natoa kesho baada ya masaa 24.
Kwa leo naishia hapa.

Tukutane tena wakati ujao kwenye kujuzana zaidi.

Unakaribishwa kwa maoni, ushauri na kupendekeza mada yoyote izungumziwe kuhusu nywele asilia.

Nakutakia mapenzi mema ya nywele zako.
 
Habari wana jamii, heri ya mwaka mpya.

Nahitaji nywele zangu ziwe na mawimbi kama curl mawimbi ya muda mrefu bila kuhangaika kuweka marolazi kila wiki. Sasa nikiweka curl inakata nywele zangu mpaka inanilazimu kunyoa kipara, na sababu ya kukata ni kwamba nawekaga dawa nyeusi ya kubadili nywele rangi na wanasema curl na dawa za kubadili rangi nywele hazipatani.

Nikiziacha bila kuweka piko zinakuwa nyekundu na mbaya. Nimeshajaribu kuweka curl kama mara mbili hivi lakini tatizo lipo palepale. Sasa nataka kuweka dawa nyingine ya wave nzuri ambayo nitapaka halafu niweke rolazi ya curl nywele ziwe na mawimbi ya muda mrefu.

Naomba kutajiwa dawa nzuri ya wave itakayaonisaidia. Nimeshatumia Movit mild for short hair, na Easy wave zote hazijanisaidia. Nikiweka baada ya muda mfupi nywele zinakuwa kavu kama hazina dawa. Na mafuta natumia ya Softnfree gel activator na ECO styling gel. Pia mirija sipendelei nywele zinakakamaa na ile lota body inakata nywele zangu.

Msaada wadau, asanteni.
 
Dawa ndio inakata nywele na kuzifanya ziwe mbaya endapo hautazifatilia kwa makini Au kutumia dawa ambayo haiendani na nywele zako
Sio kila dawa za nywele unaweza kutumia it depends na aina ya nywele na aina ya dawa
Kuna nywele nyepesi na nzito

Kwa ushauri tu
Weka mirija ni nzuri sana ukipata saluni inayojua kutengeneza mirija maana inakaa muda mrefu, kisha uwe unapaka mafuta ya kulainisha nywele

Zaidi ya hapo nywele zako labda hazina shukrani tu Au kwann usiwe unavaa mawigi ya curls more that kuhangaika kupoteza hela, muda kuhangaisha kichwa unasuka zako minyoosho ukitoka unavaa wigi lako la curl yapo mengi tu kila aina utakayopenda
 
Pisi kali,
asante my dear, kwa ushauri mzuri. nitajaribu na mawigi pia ingawa duuh! naonaga km nimebeba mzigo kichwani ila nitajitahidi. thanks again.
 
Ukiweka curl usiweke kuperblack yoyote, tu, weka super black ya movit na mafuta ya Kali ya MIKI, hapo utamalizana
 
MTU na hasa mwanamke anayetambua umuhimu wa mwonekano mzuri hutamani kuwa na nywele nzuri za kutosha na zenye afya yake ya asili. Tatizo la kupotea kwa nywele au upara (wengine hupenda hali hii) limekuwepo tangu awali. Kipara kinaweza kuja kwa sababu za kimaumbile za kawaida.

Kuna sababu nyingi zinazoweza kusababisha kupotea kwa nywele kama vile:

Sababu za kimazingira
Kuzeeka
Msongo wa mawazo (stress)
Kuvuta sigara kupita kiasi
Lishe duni
Homoni kutokuwa sawa
Kurithi vinasaba
Maambukizi kwenye ngozi ya kichwa
Matumizi yasiyo sahihi ya vipodozi vya nywele
Baadhi ya dawa za hospitali
Matatizo katika kinga ya mwili
Upungufu wa madini chuma, na
Magonjwa mengine sugu
Kitunguu maji kina kazi nyingi katika mwili wa binadamu kwani hutibu magonjwa mengi kama kikohozi, vidonda vya tumbo na mifupa, ngozi, koo, figo, na pia kina virutubisho vingi vya vitamini C.

Kitunguu hiki huwa na salfa (sulphur) ambayo husaidia kutengeneza tishu za ‘collagen’ katika mwili ambapo huipa nywele na ngozi nuru ya aina yake.

Hivyo naweza kusema kuwa juisi ya kitunguu maji husaidia kukuza nywele na kwa wale wenye nywele za kukatika, kupaka kitunguu maji mara kwa mara kunaweza kusaidia kupambana na tatizo hilo.

JINSI YA KUANDAA

kutegemea na ukubwa wa kitunguu chenyewe
•Osha vizuri kitunguu au vitunguu na kisha ukimenye au uvimenye
•Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga
•Saga kwenye blenda au uvitwange kwenye kinu.
•Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi.
•Vichuje vizuri ili upate majimaji. Hakikisha kwamba huongezi maji kwa hivi vitunguu.

JINSI YA KUPAKA

Nywele sio lazima ziwe safi maana unapaswa kuziosha baada ya kupaka maji ya vitunguu.

Chukua pamba ambayo utatumia kupaka hayo maji ya vitunguu kwenye nywele zako. Paka zile sehemu ambazo nywele zimekatika. Unaweza pia paka kichwa kizima.
Baada ya kupaka unapaswa kuvaa kofia ya plastiki na kitambaa kichwani ili uweze kupata joto.
Ukae hivyo kwa muda wa saa 4 – 5
Baada ya hapo unaweza kuosha na kukausha nywele zako.

HITIMISHO

Ni vyema kufanya shughuli hii ya kupaka vitunguu angalau mara mbili kwa mwezi.

Ikiwa harufu ya kitunguu ni kali, unaweza kuongezea asali kidogo kwenye maji ya vitunguu.

Kwa matokeo mazuri ya kukuza na kutunza nywele zako, fanya kama jinsi nilivyoeleza apo juu.......
fbb11917b84b9dcf5909cbd41542b3af.jpeg
af5b24709606fb710414de1717d108b0.jpeg
703b09e599ea759bb36eb806828117c2.jpeg


@military_Genius
 
Back
Top Bottom