Utunzaji wa nywele za asili

Asante kwa uzi mzuri umenitia moyo kwa safari hii niliyoianza, pia kuna jeli ya bamia ambayo inatumika kama leave in conditional, unachemsha bamia, unachuja then unapaka, usioshe. Pia majani ya mpera nayo nasikia ni mazuri sana though sijatumia.
 
Weka kapicha
Huwa sina formula ila nilishaacha kutumia shampoo, naosha nywele na sabuni ya kipande haswa jamaa.

Chakula nnachokilisha nywele zangu Kila ijumaa ni tui la nazi bila kulichanganya na maji. Siku nyingine ndizi mbivu na mtindi, siku nyingine parachichi na mtindi na olive oil, siku nyingine juice ya carrot na maji ya mchele, au maji ya mchele uliolowekwa kwa siku 5 au juisi ya kitunguu maji peke yake na siku nyingine nachanganya kitunguu maji na tangawizi nachuja juisi yake.

Vyote hivi sichanganyi na maji na nikipaka usiku nalala nimefunga nywele na kofia ya plastic asubuhi naziosha na kuzipaka hair butter na hair cream (Haya mafuta ya dukani) kisha naweka protective style mwenyewe ya wiki nzima.

Nshasahau kadhia za wasusi zaidi ya mwaka sasa na nywele zangu zinarefuka kila leo.

Pamoja na kurefuka wengi tuu wameshaniambia, Kasie una asili ya kisomali au kimanga wewe, hizi nywele zote ni zako mbona zina waves kama za kisomali wakati wewe ni mmatumbi wa kinyamwezi..... Basi Mie nacheka tuu hehehehee.

Kasie Manywele.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Picha tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tumia Asali katika Urembo wa Nywele na Ngozi yako

Asali hutumika kulainisha Ngozi
Asali ina asili ya kuvuta unyevu kutoka kwenye hewa na kuipa ngozi uwezo wa kuhifadhi unyevu hivyo ni faida kwa mtu mwenye ngozi kavu.

Jinsi ya kuandaa
Chukua asali mbichi kijiko kimoja cha chai kisha paka usoni, kaa nayo kwa dakika 15 hadi 20 kisha safisha uso wako.
Asali katika kusafisha ngozi, kutibu na kuzuia chunusi

Kutokana na uwezo wa asali katika kuua bacteria na kuvuta uchafu katika matundu ya ngozi asali itakusaidia kutatua tatizo la chunusi.

Jinsi ya Kuandaa
Chukua asali mbichi Kijiko kimoja cha chakula changanya na mafuta ya nazi vijiko viwili changanya mchanganyiko uwe mlaini kisha paka usoni huku ukisugua taratibu kwa kufanya kama viduara huku ukiepuka kufikisha machoni. ukimaliza kusugua uso na mchanganyiko wako osha uso wako.

Jinsi ya kuandaa kama kisafisha ngozi, exfoliator

Changanya kijiko kimoja asali na kijiko kimoja baking soda. tumia mchanganyiko huu kusugua ngozi yako. Asali inaongeza lishe na chembe chembe kuzuia madhara yanayotokana na sumu za hewani zinazozeesha ngozi. Baking soda inasaidia kusafisha matundu ya ngozi.
Asali inasaidia ngozi iliyoungua na jua kujirudi na kung'aa.

Jinsi ya kutumia asali katika nywele
Asali inatibu nywele kavu zilizopauka, na kulainisha ngozi kavu ya kichwa na kutibu muwasho kichwani.

Jinsi ya kufanya
Changanya kijiko kikubwa cha asali na maji ya uvuguvugu kisha paka kichwani Acha kwa muda wa saa 1 iwe kama conditioner kisha safisha nywele zako.

Unaweza kuchanganya asali kiasi cha kijiko kimoja mpk viwili katika maji vikombe vitano kisha safishia nywele zako taratibu, yaani yapitishe tu hayo maji kwenye nywele zako ambazo ni safi.

Tahadhari: Asali kwa kiasi kikubwa hupausha weusi wa nywele kutokana na Hydrogen Peroxide inayopatikana ndani ya asali.

Ni vema ukatumia asali mbichi kujihakikishia faida za asali katika mwili wako.

Iwapo unavutiwa na matumizi ya kitu cha asili katika urembo wako unaweza kuongeza kitu hicho katika kitu kingine unachotumia mfano katika steaming yako au scrub unayotumia.
 
IMG_2664.JPG

Jinsi ya kuandaa

* Chukua kitunguu kimoja au viwili kutegemea na ukubwa wa kitunguu, kimenye

* Kata kitunguu au vitunguu vipande vidogo vidogo ili iwe rahisi kusaga au kutwanga

* Visage au vitwange mpaka vilainike kabisa ili uweze kutoa maji kwa urahisi na uvichuje bila kuongeza maji.

Jinsi ya kupaka

Paka kichwa kizima na kisha uvae kofia ya plastic ambayo itasaidia kukupa joto zaidi. Kaa na kofia ndani ya saa 4-5 kisha utoe na kuziosha nywele. Kwa matokeo mazuri zaidi fanya hivo mara 2 au 3 kwa mwezi.
 
Watu wanashukuru na hawajaambiwa kazi ya vitunguu kwenye "nywere" ni nini.
Kutunza, kutunza kivipi yani, kutunza ziweje,
 
iyo labda uwe housegirl au muuza genge watu hawatanotice an odd smell, ila ukiwa unafanya kazi maofisini au dukani aisee utakimbiwa na watu sio unapaka mavitunguu af unaenda banana kwenye daladala mi nitakushusha kama mi ndo konda
 
Back
Top Bottom