Jinsi ya kutumia mafuta kidogo kwenye gari

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,185
18,513
Vitu vinavyo fanya Gari litumie mafuta mengi ni pale mzigo unapo kuwa mkubwa (Load).

Mzigo huu unaweza kupunguzwa kwa kupunguza baadhi ya visababishi ambavyo si vya lazima.

1. AC: Unapo tumia AC engine lazima itatumia nguvu zaidi hivyo itaunguza mafuta mengi.

2. Unatembea zaidi ya km 45 kwa saa na madirisha umeyafungua , hii utasababisha gari kupambana na upepo hivyo kuongeza mzigo wa gari. Ina semekana kama unatembea kwa speed kubwa na madirisha yapo wazi gari litatumia mafuta zaidi hata kuliko ukiwasha AC.

Mengine watalaam watayaleta.
 
Kuweka tair pana ambazo sio recomended. Kula gar ina lebo ya aina ya tair na rim zake ubavun
 
Hapo umenifunza kitu mkuu,lkn la AC km bado sijaamini kuwa inasababisha unywaji wa mafuta,kwa sababu mahesabu ya mafuta ktk kila gari hupigiwa hesabu na uwashaji wa AC,km unatembea kilometer 50 kwa saa utatumia liter ,5 ujue mahesabu hayo ni pamoja na uwashwaji wa AC
 
Pia epuka unnecessary braking and acceleration, hasa kwenye foleni unaweza ukawa unatembea kwa silence tu
 
Ila hapo kwenye mwendo sio sahihi. Ninaelekea shambani nikirudi nitachangia vema.
 
Mimi naona kama sababu zako zinakinzana, yaani lazima upambane na moja wapo.

Mfano;

Natembea 60km/hr inabidi nifunge madirisha ili kupunguza ulaji wa mafuta - hapo itabidi uwashe AC na tunarudi kwenye ishu hiyo hiyo.
 
Hapo umenifunza kitu mkuu,lkn la AC km bado sijaamini kuwa inasababisha unywaji wa mafuta,kwa sababu mahesabu ya mafuta ktk kila gari hupigiwa hesabu na uwashaji wa AC,km unatembea kilometer 50 kwa saa utatumia liter ,5 ujue mahesabu hayo ni pamoja na uwashwaji wa AC

Kweli kabisa
 
Ukitembea na 60km/hr inakula mafuta kidogo sana ukilinganisha na ukitembea na 30km/hr ama 80km/hr...Huu ni uzoefu nilioupata mimi bainafsi.
 
Back
Top Bottom