Jinsi Ya Kutrace Email

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,202
218
Nimekuwa napata maombi mengi ya watu kutaka kujua vyanzo au mwanzo wa email Fulani wanazotumiwa au kutumiana , kuna matukio kadhaa ambayo yametokea na yanaendelea kutokea kwa watu haswa vijana .

Unawasiliana na mtu anasema yuko mbali sana , akipiga simu anatumia private kujua hiyo namba mpaka uende kwa mtoa huduma wako na hiyo ni hatua ndefu zaidi , lakini wengi wanajisahau linapokuja suala la barua pepe wanaamini mtu hawezi kujua chanzo cha hizi emails .

Hapo chini kuna njia kadhaa za kuweza kujua IP Address ya computer ambayo ilitumika kutuma email husika kisha unaweza kutrace na kujua hiyo IP Address ipo wapi na imesajiliwa kwa nani .

Njia hii sio ya uhakika wa asilimia moja kwa sababu kuna wengine wanatumia wireless na wanahama hama ip address hubadilika kutokana na mazingira , wengine watoa huduma zao wa Mtandao wanaficha Baadhi ya vitu na mambo kama hayo .

GMAIL NA OUTLOOK

1 – Fungua Anuani yako ya GMAIL

2- Angalia mshale chini ambao uko Kushoto mwaka Reply , Chagua Show Original



Angalia kwa makini msitari wa maneno ambao umeandikwa Received: from ni rahisi zaidi kuitafuta kwa kubonyeza Ctrl + F utagundua kuna majibu mengi ya Received From katika kichwa cha Ujumbe husika , Hii ni kwa sababu itakuwa na Ipaddress za server ambazo email husika imepitia kabla ya kufika kwako .



Kujua computer ya kwanza ambapo email yako imetokea inabidi uangalie chini kabisa , kama unavyoona hapo katika picha email ya kwanza imetoka katika computer inayoitwa Aseem yenye IP address 72.204.154.191 halafu ikapitishwa katika ISP eastrmmtao104.cox.net Nakadhalika mpaka ilipofika katika MailBox Yako .

Hiyo Aseem ni computer ya mtu na IP address yake ni kama ilivyoonyesha hapo juu , kabla ya kuelezea jinsi ya kutafuta Ilipo IP Address kwanza tujifunze katika Yahoo na OutLook .

Yahoo Mail Beta

1 – Login Katika Yahoo yako ( kama unatumia mfumo mpya wa Yahoo Beta Hakikisha una Double Click email ili ifunguke katika ukurasa mpya )

2 - Juu kulia utaona Drop Down Menue ambapo Standard Header ndio imechaguliwa

3- Click katika Standard Header kisha chagua Full Header



Utaona Taarifa zile zile kama nilivyotolea mfano katika GMAIL hapo juu lakini katika Window Mpya .



MICROSOFT OUTLOOK

1- Fungua Outlook
2- Nenda katika View katika Menu ya juu kabisa ( YA EMAIL sio ya WINDOWS ) kisha chagua Options


3- Utaona kibox kimekuja ambacho unaweza kuweka Option Mbali mbali hichi ni kidogo sana na chini yake kabisa utaona kibox cha Internet Headers ni rahisi kama ukikopy an paste hayo maandishi katika NotePad au Word Pard au WORD , ili uweze kuiona kwa urahisi zaidi


KUJUA CHANZO CHA EMAIL HUSIKA

Kutokana na maelezo hapo juu IP Address iliyotuma hiyo email ni 72.204.154.191 ,sasa tuangalie hiyo ip address ipo wapi haswa .

Kuna tovuti zinazotoa huduma hizi za kutafuta vyanzo lakini maarufu zaidi ni IP2Location na GeoBytes IP Locator , kuna baadhi ya antivirus na firewall ambazo zinauwezo wa kutrace pia vyanzo vya ip address .

Geobytes imenipa ramani kubwa ya New Orleans , LA pamoja na taarifa zingine za eneo husika .



IP2Location itakupa habari zaidi pamoja na kukuambia ISP wa aseem ni nani mfano huyu wake ni COX ambaye yuko New Orleans .

Ukitaka taarifa zaidi unaweza kutafuta katika database za WHOIS moja ya hizi database ni ARIN WHOIS Database Search. hii itakuwa taarifa nani ana host hiyo ip address na taarifa zingine za usajili , unaweza kuwasiliana nao kama unataka taarifa zaidi za IP ADDRESS HUSIKA

ENDELEA KUFURAHIA NA JITIHATA ZAKO ZA KUTRACK IPADDRESS ZA WATU , KUMBUKA HILI SOMO NI KWA AJILI YA KUJIFUNZA TU , UNAPOAMUA KUTUMIA KWA AJILI YA MAMBO YAKO UJUE WEWE NDIO UTASHIKWA KWA SHUGULI HIYO KAMA UMETUMIA SOMO HILI KINYUME CHA SHERIA

KAMA KUNYANYASA WATU KISA UMEJUA ALIPO NA MAMBO KAMA HAYO

AHSANTE
 
Nashukuru Shy kwa this useful and informative article. Sasa tupe jinsi ya kuficha IP yako.
 
Dotori,
Kwi kwi kwi!
Ili usijulikane kwamba unatuma mail kutoka wapi ama? (just kidding).
Nadhani Zone Alarm Pro. wana system ya namna hii ya kuficha IP address za wateja wao, lakini hii ni ile ya kulipia, sio free edition.
Naam Shy, tupe somo la kuficha Ip zetu.

Asante sana.
 
Nimefanya Google search ya "how to hide IP address", nimepata hits nyingi. Tatizo siku hizi uki-download vitu toka unreliable sites unaweza kupata virusi au malware.
 
Ina maana hakuna kujificha ukiwa ndani ya Internet,hamna haja ya kutumia nicks name hapa JF.Au mnaonaje hii?
 
Ina maana hakuna kujificha ukiwa ndani ya Internet,hamna haja ya kutumia nicks name hapa JF.Au mnaonaje hii?

UNAWEZA KUJIFICHA LAKINI UJUE KWAMBA INTERNET HAINA MWENYEWE , HAINA MIPAKA NA HAINA RANGI WALA DINI NI KAMA CATCH ME NOT WAKATI WOWOTE UNAWEZA KUKUTWA NA CHOCHOTE AU LOLOTE

LAKINI MADA YAKO NI NYINGINE NAOMBA UNIPE MUDA NITAANDIKA KUHUSU UNAVYOWEZA KUFUATILIWA POST ZAKO KATIKA FORUMS MBALI MBALI

AHSANTE
 
Ina maana hakuna kujificha ukiwa ndani ya Internet,hamna haja ya kutumia nicks name hapa JF.Au mnaonaje hii?

Digital/electronic technology do leave traces. From digital copier, modern typewriter, computer use to internet use etc. One has to be careful in using these electronic/digital media.
 
Dotori,
Kwi kwi kwi!
Ili usijulikane kwamba unatuma mail kutoka wapi ama? (just kidding).
Nadhani Zone Alarm Pro. wana system ya namna hii ya kuficha IP address za wateja wao, lakini hii ni ile ya kulipia, sio free edition.Naam Shy, tupe somo la kuficha Ip zetu.

Asante sana.

NI KWELI KUNA KAMPUNI ZINATOA HUDUMA HIZI LAKINI KUNA MTINDO MMOJA UNAITWA DATA MINING KWA KUTUMIA NJIA HII UNAWEZA KUJUA TAARIFA NYINGI ZAIDI ZA WATU AU MTU ILA NAOGOPA KUTOA SOMO KUHUSU UJUZI HUU KWA SABABU WATU WANAWEZA KUTUMIA NDIVYO SIVYO
 
digital copier, modern typewriter, computer use to internet use etc. One has to be careful in using these electronic/digital media.

NI KWELI HATA UNAVYOPRINT KITU UJUE KUNA MAANDISHI YANABAKI AMBAYO WEWE HUWEZI ONA NA NI MAANDISHI YA TAARIFA ZA COMPUTER ILIYOTUMIKA KATIKA SHUGULI HIYO

ILA WENGI WAMEKUWA WAJANJA SIKU HIZI WANA PRINT NA REFILL CARTRIDGE AMBAZO HAZINA FEATURES HIZI NA NI RAHISI KUFORGE NA KUCHEZEA MAMBO KAMA HAYO

UKIENDA UBALOZI WA UHOLANZI MFANO CARTDRIGE WANAZOTUMIA PALE NA VITU VINGINE NI KUTOKA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA NCHI HIYO WANAITA BOZZA
 
Shy asante sana kwa shule hii uliyotupatia.

Sasa kuna kitu nataka kuuliza. Unaweza je kujua e mail ambazo zimetumiwa e mail kama mtumaji ameweka kwenye BCC? yaani kwenye sent inaonekana jina moja lakini watu wengi wametumiwa kwa kutumia BCC hapo unaweza kujua je?
 
NI KWELI KUNA KAMPUNI ZINATOA HUDUMA HIZI LAKINI KUNA MTINDO MMOJA UNAITWA DATA MINING KWA KUTUMIA NJIA HII UNAWEZA KUJUA TAARIFA NYINGI ZAIDI ZA WATU AU MTU ILA NAOGOPA KUTOA SOMO KUHUSU UJUZI HUU KWA SABABU WATU WANAWEZA KUTUMIA NDIVYO SIVYO

Shy,
Hapa unakiuka maadili ya JF ya kuongea kila kitu kwa uwazi.
Tunaongea mambo waziwazi hapa JF, kwa hiyo wewe mwaga materials watu waendelee kujielimisha. Hilo la watu kutumia elimu yao kwa minajili haramu huna mamlaka nalo hata kidogo, na hakuna mwenye mamlaka nalo na wala usiumize sana akili yako. Ndio maana inatokea kwmba mtaalamu mmoja anatengeneza virusi na kuvisambaza na mwingine anatengeneza programu ya kuondoa virusi hivyo, na wote ni programmers!

Kwamba daktari mmoja anawapandikiza mimba watu wenye matatizo ya uzazi ili wazae na mwingine anasaidia watoaji mimba ili wasizae! Elimu ni ile ile ya udaktari.
Jimwage!
 
Habari Za Mchana Idimi

Msimamo Wangu Uko Pale Pale Nitaandika Intro Tu Vingine Mtu Ni Kazi Yake Kutafuta Na Kuongezea Siwezi Kusema Kila Kitu Na Vitu Hivi Viko Updated Kila Siku

Naamini Kuna Wataalamu Na Wajuzi Zaidi Wanaojua Zaidi Wanaoweza Kuja Kuongeza Japo Kidogo

Mie Nimeishia Hapo

Mchana Mwema
 
Kwi kwi kwi.
Hapa Bulyanhulu kwema tu mkuu.
Umeeleweka.
Tuendelee kuelimishana.
 
Back
Top Bottom