SoC01 Jinsi ya kutibu tatizo la upungufu wa nguvu kwa wanaume kwa kutumia nguvu za kiroho

Stories of Change - 2021 Competition

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,432
105,851
Utangulizi
Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume/vijana ni tatizo ambalo limekua likizidi kukua hasa kwa watu walizaliwa miaka ya 80, 90 na 2000. Wahenga wanasema kwamba vita vingi tunavyovipigana ndani ya vichwa vyetu hua sio halisi, Kwamba mambo tunayoyafikiria na kuyahofu kwenye maisha halisi hua sio halisi ila ni sisi tunayafanya yawe halisi kutokana na vile tunavyofikiria katika mlengo hasi na kujenga hofu ndani ya maisha yetu.

Hofu ikishakuingia basi unaweza kua vyovyote vile unavyohofu mfano kama unahofu kwamba kitu fulani huwezi kukifanya basi unaweza kujikuta kweli usiweze au kama unahofu kwamba una ugonjwa mwilini mwako basi unaweza kuanza kuona dalili za ugonjwa huo mwilini mwako. Binafsi naamini kila mtu anazo nguvu za kiume ila tunashindwa tu jinsi ya kuiimarisha nguvu hizo kutokana na hofu tunayojiwekea vichwani mwetu

Hofu ndio chanzo kikuu cha tatizo hili kwa wanaume wengi, vichwa vya watu vimejaa hofu ya kushindwa kufanya tendo kwa ufanisi. Zifuatazo hapa chini ni sababu zisizo rasmi ambazo nimegundua zinaweza kupelekea mtu kujawa na hofu na kushindwa kufanya tendo kwa ufanisi sababu hizo nimezigawa katika makundi mawili ambayo ni…

Sababu za ndani ya mtu binafsi
Hizi ni sababu ambazo zipo ndani ya mwanaume ambazo zinaweza kuchangia kujenga hofu na kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi.

Mitandao ya kijamii; Utandawazi umefanya dunia kuwa kama kijiji kwa kuwaweka karibu, hii inawafanya watu kuelezeana mambo mbalimbali yanayohusuahusuyo mapenzi kupitia mitandao ya kijamii kama vile FB,YouTube,JF,Instagram nk. Mtu anaweza kuelezea jinsi anavyoweza kufanya tendo la ndoa kwa muda wa saa nzima bila kupumzika, mtu mwingine akiona maelezo hayo anayaweka kichwani na kuanza kuwaza kama ataweza naye kufanya tendo muda mrefu na kuunganisha mzunguko utakaofuta bila kupumzika.

Utazamaji wa video za ngono; kama ni mtazamaji wa video za ngono utaona mtu anafanya tendo kwa saa nzima, kama huna uelewa jambo hili linaweza kukutia hofu kama nawe utaweza kufanya kwa muda mrefu kiasi hicho lakini kumbe watu hao wao wapo kwenye biashara watafanya kila liwezekanalo biashara yao iwe yenye ubora ikiwemo kutumia madawa ya kuongeza nguvu.

Mwanaume kutokujitambua ujinsia wake; Kila mtu ana ujinsia (sexuality) wake, wengi hawatambui jambo hili wanaona kwakua mtu ni mwanaume basi atakua hivo kumbe sio kweli kila mtu ana jinsi anavyojisikia kuhusiana na jinsia yake . Mtu unaweza kua hupendi kufanya tendo la ndoa , au huwezi kufanya tendo la ndoa ipaswavyo kwakua wewe ujinsia wako ni Demisexual ambapo hisia za kufanya tendo zinakuja kwa watu ambao una mapenzi ya dhati juu yao.

Sababu zinazotoka nje ya mtu
Yafuatayo ni mambo baadhi ambayo yakiwepo kwa mwanamke iyanaweza kufanya mwanaume asifanye tendo kwa ufanisi.

Usafi wa mwanamke; Usafi ukiwa hafifu kwa mwanamke inaweza kumfanya mwanaume ashindwe kufanya tendo ipasavyo maana atakwenda mzunguko mmoja asirudie tena maana mazingira ya mwanamke sio rafiki kufanya tendo.

Upendo wa mwanamke; Mwanamke kama hana upendo kwako anaweza kufanya usifanye tendo ipasavyo maana mwanamke anayekupenda atakuvumilia na kukuhamasisha ili uendelee kufanya tendo.

Adui wa upungufu wa nguvu kiume kwa wanaume ni “Mindset” yaani hofu, ukishajaza hofu mwilini basi huwezi kutenda tendo la ndoa kama inavyotakiwa. Hivyo basi tukiweza kuiziwia hofu wakati wa tendo basi tunaweza kudhibiti tatizo hili.

Hofu (Mindset) inavyosababisha upungufu wa nguvu
Thalamus
ni kisehemu ndani ya ubongo wa mwanandamu ambacho kila upande kimezungukwa na kitu kiitwacho Paleomammalian Cortex kwa lugha rahisi hufahamika kama Limbic System, Limbic System ni mfumo ambao kazi yake ni kuratibu mfumo wa Tezi na mfumo wa Autonomic Nervous System, Autonomic Nervous System (ANS) ni mfumo ambao huratibu mambo mbalimbali ila moja ya jambo ambalo huratibiwa na mfumo huu ni Emotions yaani vile mtu anavyojisikia. Emotions ni kama vile hasira,upendo,ujivuni, wasiwasi, uogo, huruma, kuchanganyikiwa nk . ANS ndio inaratibu hisia moja ya hisia hizo ni upendo na na mfumo wa ANS unaratibiwa na Paleomammalian Cortex/Limbic System hivyo basi maswala yote yanayohusu mapenzi yanaratibiwa katika mfumowa Limbic System.

Mapenzi ni kama spika iliyounganishwa na Computer, spika hua inatoa sauti tu ila haijui inatoa sauiti gani bali CPU ndio hufahamu hicho kinachotoka ni kitu gani au kama macho yenyewe yanachukua picha ya kile kilicho mbele yake ila macho hayajui hicho ni kitu gani bali ubongo ndio hutambua hicho kilicho mbele ni kitu gani. Wengi hua tunasema kwamba moyo ndio humpenda mtu la hasha! moyo hauhusiki katika kupendai bali Ubongo, unapomuona mtu akakuvutia Limbic System inatoa homoni mbazo zinapelekea moyo kwenda mbio, halafu unasikia moyo unampenda sana huyo mtu lakini ukweli huo upendo upo kwenye ubongo.

Hisia unazisikia kwenye moyo sababu kuna Neva mbalimbali ndani ya moyo ambazo huhisi maumivu au hali yoyote kutokana na jinsi ubongo ulivyoamuru moyo uhisi juu ya mtu huyo alivyekuvutia. Kwa ujumla swala la kupenda au kupendwa halihusiani kabisa na moyo bali ni ubongo ndio huhusika ila moyo ni kwa ajili ya kuzitoa zile hisia zilizopo kwenye ubongo, kwa lugha ya kitaalamu tunaweza kusema kwamba kazi ya moyo katika mapenzi unatumika kama Output device.

Kwakua mapenzi yanaratibiwa na ubongo basi swala la nguvu za kiume tunaweza kulitatua kwa kutumia Akili (Mind) kumbuka kwamba Mind ipo ndani ya ubongo. Conscious mind ni sehemu ya Akili (mind) ambayo inahusika na kushughulikia mambo yote ambayo tunayafahamu kwa kuona,kusikia au kuhisia. Kiufupi Conscious mind inashughulikia yale ambayo yapo katika utambuzi/ufahamu wetu, kumbuka kwamba kitu unachofikiria kwenye akili yako juu yako ndio kitu kitakachofanyiwa kazi .

Unapotaka kufanya tendo la ndoa ukaanza kuhofu kwamba hautaweza kufanya tendo vizuri Conscious mind inazichukua hizo hofu zako za kwamba hautaweza ndio zinazofanyiwa, taarifa hizo kwamba hataweza kufanya tendo zinaenda hadi kwenye mfumo wa Limbic sytem kwakua mfumo huu ndio unaamrisha homoni zinazohusika katika kuimarisha Uume ufanye tendo kwa muda mrefu na kwa viwango bora.

Jinsi ya Kufanya
Hofu ni ugonjwa mbaya ambao tunajiambukiza wenyewe pindi ukishaweza kuidhibiti basi mambo mengi ndani ya maisha yako yatatendeka kwa ufanisi, pindi unapotaka kufanya tendo la ndoa usiwazie video za utupu ulizotazama au maneno ya watu wanasema kwamba wao wanaweza kwenda mzunguko mmoja kwa saa nzima na kuunganisha, usikanie kufanya tendo chukulia ni kitu cha kawaida, vaa ujasiri iambie akili yako kwamba unaenda kufanya vyema.

Ukijiambia hivyo Concious Mind itaushawishi mfumo wa mwili kuachilia hormone mbalimbali zinazohusu na utendaji wa tendo hivyo itakufanya uweze kufanya kwa kiwango Fulani. Hakikisha mwanamke unayefanya nae tendo unampenda kwa dhati hii itakufanya uwe na hamu ya kurudia kufanya tendo , ukiwa unalifanya tendo la ndoa mara nyingi itakusaidia kuimarisha uwezo wako kumbuka kitu kisichotumika hua dhaifu na kinachotumika hua imara zaidi.

Dihydroxyphethylamine
Ni kemikali/homoni inayozalishwa katika ubongo wa katikati kisha kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya ubongo, kwa lugha rahisi kemikali hii huitwa Dapomine. Kazi yake ni kuhamasisha mwili uendelee kufanya jambo ambalo linaupa mwili raha kama vile kula au kufanya mapenzi , kemikali hii ikipungua mwilini husababisha mtu kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Kama unakua huna hamu ya kurudia tendo baada ya kumaliza mzunguko basi unaweza kutumia kemikali hii kukuongezea hamu kwa kuongeza kiwango cha uzalishwaji wake mwilini mwako. Unaweza kuiongeza mwilini kutumia njia zifuatazo.

Muziki
Tafiti zinaonyesha kwamba kusikiliza nyimbo unazozipenda husaidia Dapomine kuongezeka kwa 9%,Wakati unatenda tendo na mwanamke wako sikiliza nyimbo uzipendazo hii itakusaidia kuongeza hamu ya kurudia tendo.

Protein
Kula chakula chenye kiwango kingi cha protein kama vile maziwa,samaki,karanga,nyama, mara kwa mara. vyakula hivi vina amino acid, acid hii hupelekea uzalishwaji wa homoni ya dapomine kwa wingi pia huongeza wingi wa mbegu za kiume. Lakini pia kula vyakula vyenye Vitamin kama vile mbogamboga kwa wingi.

Mazoezi
Kufanya mazoezi japo dakika 30 itakusaidia kuongezeka kwa homoni hii ya dopamine, hivyo itakusaidia kupata hamu ya kufanya tendo mara nyingi lakini pia mazoezi yatakusaidia kua na pumzi ya kufanya tendo muda mrefo.

Hitimisho
Miili yetu imeumbwa kwa namna ambayo mwili wenyewe unajitosheleza na unaweza kujitibu wenyewe, muhimu ni kuuamini miili yetu na tuweze kushawishi nguvu zetu za kiroho zitibu matatizo mbalimbali ya mwili. Katika swala la kutoweza kurudia tendo zaidi ya mara moja mwanamke ana nafasi kubwa zaidi ya kumfanya mwanaume ahamasike kuendelea. Muhamasishe mpenzi wako na kumtia moyo kwamba anaweza kufanya vizuri, usimbeze wala kumcheka mfanye aone kuwahi kumaliza ni jambo la kawaida.

Kwa kufanya hivyo itamsaidia mwanaume kuondoa hofu kisha anaweza kutenda vizur zaidi siku za mbeleni, kumbuka kila kitu kinaanzia kwenye akili yako kisha kinaenda kuhifadhiwa kwenye ulimwengu wa kiroho matokeo yake yanatolewa kwenye mwili wako hivyo ukiamini utafanya vyema basi itakua hivyo na ukiamini kinyume chake itakua hivyo pia.

Binaadamu tunapenda tunapofanya kitu tuone matokeo ya haraka hivyo basi kuna wengine kufanya jambo hili nililoelezea wanaweza kuona ni usumbufu, Basi kwa wanaopenda kutumia miti shamba kutatua tatizo hili basi ningewashauri watumie mizizi ya mti huu.

Mti huu unapenda kuota kwenye vichuguu au sehemu yenye ardhi ngumu, una majani madogomadogo na unatoa matunda madogo ambayo ndani yana maji ya zambarau unaweza kuyala . Chimba mzizi wa mti huu safisha kisha uutafane muda mchache kabla ya kufanya tendo, itakusaidia kuchelewa kumaliza mzunguko.

Unaweza kuchukua shina la mti huu ukalipanda nyumbani kwako, kwetu miti hii ni mingi sana huna haja hata ya kwenda porini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa miti hii inapatikana kuanzia kisarawe, kimara,kibamba,ruguluni. Moshi wilaya ya mwanga niliwahi kuiona , tabora ipo pia.

IMG_20210511_092850_0.jpg
Ahsanteni.​
 
Unajua stress ni emotion, unaweza kuziblock tu hizo emotions halafu chukulia poa kabisa.. she's yours.
Ushauri wangu fanya uwe unakutana nae mara kwa mara hali yako itakua sawa kabisa hutaamini
Kumbuka Misuses na Use

Jean Baptiste De Lamarck's - Law Of Use and Disuse.
 
Plato, plotonus, proclus na Aristotle wanafalsafa wa zamani wa kigiriki walitoa concept inaitwa The Great Chain of Being ambapo ilikuja kuelezewa zaidi baadae kwenye Neoplatonism . walisema kwamba maisha yapo kwenye ngazi Fulani ambazo juu kabisa anaanza Mungu,wanafuta malaika, kisha mwandamu, wanafuta wanyama,wanafuata mimea halafu mwisho kabisa yupo shetani.

Davinci alichukua idea hii kisha pale katikati alipo mwanadamu akauweka mchoro wake wa The Vitruvian man. Aliuweka pale akiamini kwamba mchoro wake unamuonyesha mwanadamu kamili aliyeumbwa na jinsi mazingira yake yanayomzunguka anavyoweza kuyamudu, pia kigezo cha mwandamu kuwekwa katikati kwenye the great chain of being wanafalsafa hao wanaamini kwamba mwanadamu ni kiumbe kamili na mwenye hadhi kubwa kuliko viumbe wote.
 
Mwanadamu kwaumba na roho ambayo ni immortal na Mwili ambao ni mortal hivyo inamuwezesha mwanadamu kuweza kuishi sehemu yoyote ile, duniani au mbinguni ambacho ni kitu malaika,shetani au wanyama na mimea wamenyimwa. Mwanadamu kwakua ana roho yenye uungu na mwili wa kibanaadamu amepewa chaguzi la yeye kuweza kuishi uungu kwa kutenda mema maishani mwake au uushetani kwa kutenda ubaya maishani mwake. Hicho kitendo cha kuchagua ndio kinaufanya tuwe viumbe tuliopendelewa zaidi kuliko kiumbe chochote.

Kwakua roho ya Mwanadamu imetoka kwa Mungu ina Uungu basi anaweza kufanya lolote lile kwa kutumia uwezo wa akili/mind aliojaliwa.
Unaweza kujenga na kubomoa chochote kilicho ndani ya mwili waako au katika mazingira yako kwa kutegemea na unavyofikiria.
Stay on Postive lane/thought no matter how harshy environment are.
You're what you think!✌️
Huu ujumbe unanihusu👇👇

"Unaweza kujenga na kubomoa chochote kilicho ndani ya mwili wako au katika mazingira yako kwa kutegemea na unavyofikiria.
Stay on Postive lane/thought no matter how harshy environment are."
 
Cling it mate...
You're what you think
 
Utangulizi
Upungufu wa nguvu za kiume kwa wanaume/vijana ni tatizo ambalo limekua likizidi kukua hasa kwa watu walizaliwa miaka ya 80, 90 na 2000. Wahenga wanasema kwamba vita vingi tunavyovipigana ndani ya vichwa vyetu hua sio halisi, Kwamba mambo tunayoyafikiria na kuyahofu kwenye maisha halisi hua sio halisi ila ni sisi tunayafanya yawe halisi kutokana na vile tunavyofikiria katika mlengo hasi na kujenga hofu ndani ya maisha yetu.

Hofu ikishakuingia basi unaweza kua vyovyote vile unavyohofu mfano kama unahofu kwamba kitu fulani huwezi kukifanya basi unaweza kujikuta kweli usiweze au kama unahofu kwamba una ugonjwa mwilini mwako basi unaweza kuanza kuona dalili za ugonjwa huo mwilini mwako. Binafsi naamini kila mtu anazo nguvu za kiume ila tunashindwa tu jinsi ya kuiimarisha nguvu hizo kutokana na hofu tunayojiwekea vichwani mwetu

Hofu ndio chanzo kikuu cha tatizo hili kwa wanaume wengi, vichwa vya watu vimejaa hofu ya kushindwa kufanya tendo kwa ufanisi. Zifuatazo hapa chini ni sababu zisizo rasmi ambazo nimegundua zinaweza kupelekea mtu kujawa na hofu na kushindwa kufanya tendo kwa ufanisi sababu hizo nimezigawa katika makundi mawili ambayo ni…

Sababu za ndani ya mtu binafsi
Hizi ni sababu ambazo zipo ndani ya mwanaume ambazo zinaweza kuchangia kujenga hofu na kushindwa kufanya tendo la ndoa kwa ufanisi.

Mitandao ya kijamii; Utandawazi umefanya dunia kuwa kama kijiji kwa kuwaweka karibu, hii inawafanya watu kuelezeana mambo mbalimbali yanayohusuahusuyo mapenzi kupitia mitandao ya kijamii kama vile FB,YouTube,JF,Instagram nk. Mtu anaweza kuelezea jinsi anavyoweza kufanya tendo la ndoa kwa muda wa saa nzima bila kupumzika, mtu mwingine akiona maelezo hayo anayaweka kichwani na kuanza kuwaza kama ataweza naye kufanya tendo muda mrefu na kuunganisha mzunguko utakaofuta bila kupumzika.

Utazamaji wa video za ngono; kama ni mtazamaji wa video za ngono utaona mtu anafanya tendo kwa saa nzima, kama huna uelewa jambo hili linaweza kukutia hofu kama nawe utaweza kufanya kwa muda mrefu kiasi hicho lakini kumbe watu hao wao wapo kwenye biashara watafanya kila liwezekanalo biashara yao iwe yenye ubora ikiwemo kutumia madawa ya kuongeza nguvu.

Mwanaume kutokujitambua ujinsia wake; Kila mtu ana ujinsia (sexuality) wake, wengi hawatambui jambo hili wanaona kwakua mtu ni mwanaume basi atakua hivo kumbe sio kweli kila mtu ana jinsi anavyojisikia kuhusiana na jinsia yake . Mtu unaweza kua hupendi kufanya tendo la ndoa , au huwezi kufanya tendo la ndoa ipaswavyo kwakua wewe ujinsia wako ni Demisexual ambapo hisia za kufanya tendo zinakuja kwa watu ambao una mapenzi ya dhati juu yao.

Sababu zinazotoka nje ya mtu
Yafuatayo ni mambo baadhi ambayo yakiwepo kwa mwanamke iyanaweza kufanya mwanaume asifanye tendo kwa ufanisi.

Usafi wa mwanamke; Usafi ukiwa hafifu kwa mwanamke inaweza kumfanya mwanaume ashindwe kufanya tendo ipasavyo maana atakwenda mzunguko mmoja asirudie tena maana mazingira ya mwanamke sio rafiki kufanya tendo.

Upendo wa mwanamke; Mwanamke kama hana upendo kwako anaweza kufanya usifanye tendo ipasavyo maana mwanamke anayekupenda atakuvumilia na kukuhamasisha ili uendelee kufanya tendo.

Adui wa upungufu wa nguvu kiume kwa wanaume ni “Mindset” yaani hofu, ukishajaza hofu mwilini basi huwezi kutenda tendo la ndoa kama inavyotakiwa. Hivyo basi tukiweza kuiziwia hofu wakati wa tendo basi tunaweza kudhibiti tatizo hili.

Hofu (Mindset) inavyosababisha upungufu wa nguvu
Thalamus
ni kisehemu ndani ya ubongo wa mwanandamu ambacho kila upande kimezungukwa na kitu kiitwacho Paleomammalian Cortex kwa lugha rahisi hufahamika kama Limbic System, Limbic System ni mfumo ambao kazi yake ni kuratibu mfumo wa Tezi na mfumo wa Autonomic Nervous System, Autonomic Nervous System (ANS) ni mfumo ambao huratibu mambo mbalimbali ila moja ya jambo ambalo huratibiwa na mfumo huu ni Emotions yaani vile mtu anavyojisikia. Emotions ni kama vile hasira,upendo,ujivuni, wasiwasi, uogo, huruma, kuchanganyikiwa nk . ANS ndio inaratibu hisia moja ya hisia hizo ni upendo na na mfumo wa ANS unaratibiwa na Paleomammalian Cortex/Limbic System hivyo basi maswala yote yanayohusu mapenzi yanaratibiwa katika mfumowa Limbic System.

Mapenzi ni kama spika iliyounganishwa na Computer, spika hua inatoa sauti tu ila haijui inatoa sauiti gani bali CPU ndio hufahamu hicho kinachotoka ni kitu gani au kama macho yenyewe yanachukua picha ya kile kilicho mbele yake ila macho hayajui hicho ni kitu gani bali ubongo ndio hutambua hicho kilicho mbele ni kitu gani. Wengi hua tunasema kwamba moyo ndio humpenda mtu la hasha! moyo hauhusiki katika kupendai bali Ubongo, unapomuona mtu akakuvutia Limbic System inatoa homoni mbazo zinapelekea moyo kwenda mbio, halafu unasikia moyo unampenda sana huyo mtu lakini ukweli huo upendo upo kwenye ubongo.

Hisia unazisikia kwenye moyo sababu kuna Neva mbalimbali ndani ya moyo ambazo huhisi maumivu au hali yoyote kutokana na jinsi ubongo ulivyoamuru moyo uhisi juu ya mtu huyo alivyekuvutia. Kwa ujumla swala la kupenda au kupendwa halihusiani kabisa na moyo bali ni ubongo ndio huhusika ila moyo ni kwa ajili ya kuzitoa zile hisia zilizopo kwenye ubongo, kwa lugha ya kitaalamu tunaweza kusema kwamba kazi ya moyo katika mapenzi unatumika kama Output device.

Kwakua mapenzi yanaratibiwa na ubongo basi swala la nguvu za kiume tunaweza kulitatua kwa kutumia Akili (Mind) kumbuka kwamba Mind ipo ndani ya ubongo. Conscious mind ni sehemu ya Akili (mind) ambayo inahusika na kushughulikia mambo yote ambayo tunayafahamu kwa kuona,kusikia au kuhisia. Kiufupi Conscious mind inashughulikia yale ambayo yapo katika utambuzi/ufahamu wetu, kumbuka kwamba kitu unachofikiria kwenye akili yako juu yako ndio kitu kitakachofanyiwa kazi .

Unapotaka kufanya tendo la ndoa ukaanza kuhofu kwamba hautaweza kufanya tendo vizuri Conscious mind inazichukua hizo hofu zako za kwamba hautaweza ndio zinazofanyiwa, taarifa hizo kwamba hataweza kufanya tendo zinaenda hadi kwenye mfumo wa Limbic sytem kwakua mfumo huu ndio unaamrisha homoni zinazohusika katika kuimarisha Uume ufanye tendo kwa muda mrefu na kwa viwango bora.

Jinsi ya Kufanya
Hofu ni ugonjwa mbaya ambao tunajiambukiza wenyewe pindi ukishaweza kuidhibiti basi mambo mengi ndani ya maisha yako yatatendeka kwa ufanisi, pindi unapotaka kufanya tendo la ndoa usiwazie video za utupu ulizotazama au maneno ya watu wanasema kwamba wao wanaweza kwenda mzunguko mmoja kwa saa nzima na kuunganisha, usikanie kufanya tendo chukulia ni kitu cha kawaida, vaa ujasiri iambie akili yako kwamba unaenda kufanya vyema.

Ukijiambia hivyo Concious Mind itaushawishi mfumo wa mwili kuachilia hormone mbalimbali zinazohusu na utendaji wa tendo hivyo itakufanya uweze kufanya kwa kiwango Fulani. Hakikisha mwanamke unayefanya nae tendo unampenda kwa dhati hii itakufanya uwe na hamu ya kurudia kufanya tendo , ukiwa unalifanya tendo la ndoa mara nyingi itakusaidia kuimarisha uwezo wako kumbuka kitu kisichotumika hua dhaifu na kinachotumika hua imara zaidi.

Dihydroxyphethylamine
Ni kemikali/homoni inayozalishwa katika ubongo wa katikati kisha kusambazwa katika maeneo mbalimbali ya ubongo, kwa lugha rahisi kemikali hii huitwa Dapomine. Kazi yake ni kuhamasisha mwili uendelee kufanya jambo ambalo linaupa mwili raha kama vile kula au kufanya mapenzi , kemikali hii ikipungua mwilini husababisha mtu kukosa hamu ya kufanya mapenzi. Kama unakua huna hamu ya kurudia tendo baada ya kumaliza mzunguko basi unaweza kutumia kemikali hii kukuongezea hamu kwa kuongeza kiwango cha uzalishwaji wake mwilini mwako. Unaweza kuiongeza mwilini kutumia njia zifuatazo.

Muziki
Tafiti zinaonyesha kwamba kusikiliza nyimbo unazozipenda husaidia Dapomine kuongezeka kwa 9%,Wakati unatenda tendo na mwanamke wako sikiliza nyimbo uzipendazo hii itakusaidia kuongeza hamu ya kurudia tendo.

Protein
Kula chakula chenye kiwango kingi cha protein kama vile maziwa,samaki,karanga,nyama, mara kwa mara. vyakula hivi vina amino acid, acid hii hupelekea uzalishwaji wa homoni ya dapomine kwa wingi pia huongeza wingi wa mbegu za kiume. Lakini pia kula vyakula vyenye Vitamin kama vile mbogamboga kwa wingi.

Mazoezi
Kufanya mazoezi japo dakika 30 itakusaidia kuongezeka kwa homoni hii ya dopamine, hivyo itakusaidia kupata hamu ya kufanya tendo mara nyingi lakini pia mazoezi yatakusaidia kua na pumzi ya kufanya tendo muda mrefo.

Hitimisho
Miili yetu imeumbwa kwa namna ambayo mwili wenyewe unajitosheleza na unaweza kujitibu wenyewe, muhimu ni kuuamini miili yetu na tuweze kushawishi nguvu zetu za kiroho zitibu matatizo mbalimbali ya mwili. Katika swala la kutoweza kurudia tendo zaidi ya mara moja mwanamke ana nafasi kubwa zaidi ya kumfanya mwanaume ahamasike kuendelea. Muhamasishe mpenzi wako na kumtia moyo kwamba anaweza kufanya vizuri, usimbeze wala kumcheka mfanye aone kuwahi kumaliza ni jambo la kawaida.

Kwa kufanya hivyo itamsaidia mwanaume kuondoa hofu kisha anaweza kutenda vizur zaidi siku za mbeleni, kumbuka kila kitu kinaanzia kwenye akili yako kisha kinaenda kuhifadhiwa kwenye ulimwengu wa kiroho matokeo yake yanatolewa kwenye mwili wako hivyo ukiamini utafanya vyema basi itakua hivyo na ukiamini kinyume chake itakua hivyo pia.

Binaadamu tunapenda tunapofanya kitu tuone matokeo ya haraka hivyo basi kuna wengine kufanya jambo hili nililoelezea wanaweza kuona ni usumbufu, Basi kwa wanaopenda kutumia miti shamba kutatua tatizo hili basi ningewashauri watumie mizizi ya mti huu.

Mti huu unapenda kuota kwenye vichuguu au sehemu yenye ardhi ngumu, una majani madogomadogo na unatoa matunda madogo ambayo ndani yana maji ya zambarau unaweza kuyala . Chimba mzizi wa mti huu safisha kisha uutafane muda mchache kabla ya kufanya tendo, itakusaidia kuchelewa kumaliza mzunguko.

Unaweza kuchukua shina la mti huu ukalipanda nyumbani kwako, kwetu miti hii ni mingi sana huna haja hata ya kwenda porini. Kama kumbukumbu zangu zipo sawa miti hii inapatikana kuanzia kisarawe, kimara,kibamba,ruguluni. Moshi wilaya ya mwanga niliwahi kuiona , tabora ipo pia.

Ahsanteni.​
#VoteForVinci
 
I accept that, because everything start in the Cerebrum (Human Computer).

Sometimes we are experience low performance during Sexual Intercourse because we are not mentally fit or stronger. Lazima tujifunze kucheza na kucontrol ubungo wetu kabla ya tendo, wakati wa tendo na baada ya tendo. Hili kucreate harmony na wewe mwenye ambaye ndiye muhusika mkuu na for the long run itakusaidia kukuongezea hali ya kujiamini pindi unapotaka kufanya tendo na mwenzi wako.
 
17 Reactions
Reply
Back
Top Bottom