Jinsi ya kutibu penzi lililojeruhiwa

HorsePower

JF-Expert Member
Aug 22, 2008
3,612
2,566
Source: Mwandishi Joseph Shaluwa, GP.

Yes...sasa twende sawa katika mada yetu. Kama mtakumbuka vizuri wiki iliyopita, nilieleza kwa kirefu juu ya penzi lililojeruhiwa.

Kwamba ni ile hali ya kuachana na mpenzi wako kwasababu ya makosa ambayo unakuwa umeyafanya wewe, lakini baada ya muda akaamua kurudiana na wewe lakini mambo yake ukimtazama unagundua kabisa kwamba hayupo katika hali yake ya kawaida, huyo anakuwa na tatizo la jereha katika moyo wake.

Katika njia za kumtibu mpenzi wa namna hiyo, nilianza kwa kueleza kwamba kwanza kabisa unatakiwa kuonesha kwamba unajua kwamba mpenzi wako huyo hakuamiamini na anaumizwa na mambo yaliyotokea nyuma.

Pili, nilisema kwamba, pamoja na kufahamu huko, hata kama akikufanyia mambo mabaya ambayo wewe unafahamu kabisa yanatokanana historia iliyopita, acha kabisa kumlaumu juu ya hilo. Kuwa kawaida, tulia na utafute ufumbuzi wa tatizo, kuliko kuanza kumlaumu. Sasa tunaendelea na vipengele vilivyosalia. Unajua cha kufanya? Twende pamoja hapo chini...

USIMKUMBUSHE YALIYOPITA
Katika mazungumzo yako ya harakati za kutafuta amani kwa mpenzi wako huyo, katu usithubutu kuzungumzia juu ya mambo yaliyopita. Usiseme kwmaba: “Najua mpenzi wangu unakumbuka sana jinsi nilivyopasua kioo cha gari lako, najua ni gharama na nilikusababishia hasara...” kauli hii haifai kabisa.

Funga kinywa chako kabisa katika eneo hilo. Lakini unatakiwa utumia zaidi lugha ya sauti ya kimya zaidi kuliko kumwambia moja kwa moja. Kumbuka kwamba mpenzi wa namna hii ni rahisi sana kubadilisha mawazo au kuchukua uamuzi mbaya kwa haraka kwa jambo dogo, hii ni kutokana na kukumbuka historia yako, haamini kama unaweza kubadilika.

Kumkumbusha yaliyotokea ni sawa na kumtonesha maumivu au kumtambia kwamba, pamoja na yaliyotokea, bado kwako wewe huoni kama yana ukubwa sana, ndiyo maana bado yupo na wewe!

USIMLAZIMISHE AKUAMINI HARAKA
Ni wazi kwamba wakati huu hakuamini kabisa, lakini hupaswi kulazimisha kuaminiwa haraka. Kuwa mpole, kuwa msikivu zaidi, anza kuiga tabia mpya zaidi.

Msikilize kwa makini kila analoliongea na ulifanyie kazi, huu ni wakati wako wa kumwonesha kwamba umebadilika (kwa vitendo na si maneno) ili azidi kukupa nafasi
kubwa zaidi katika moyo wake.

ONESHA KWA VITENDO
Kujali wakati, kuwa naye karibu, kumpa pole baada ya kazi, kuwa na lugha laini ni kati ya mambo ambayo yatamfanya akuamini kwamba ni kweli umebadilika.

Wakati huu kauli yako haina maana sana kwake, kinachohgitajika zaidi ni wewe kufanya mambo kwa vitendo. Hata kama ulikuwa mkadi sana kwa anayokuambia, sasa hivi akikuambia anakuhitaji nyumbani saa 2:00 usiku, wewe fika saa 1:30 uwe umewahi nusu saa zaidi kabla ya muda mliokubaliana.

Mchana unaweza kuandika ujumbe mfupi unaosomeka: “Wewe ni wangu wa pekee mpenzi, pole sana na kazi. Jua yupo ambaye muda wote anakuwaza wewe.”
Bila kumwambia moja kwa moja, atajua hapa mpenzi amebadilika na kwa hakika utakuwa unaenda mbali zaidi katika kumtibu majeraha yake moyoni.

EPUKA HARAKA-HARAKA
Usiwe mtu wa haraka haraka, hata kama umemuomba akusaidie jambo fulani, usiwe wa kuulizia kila wakati. Kumwuliza sana, kutakuwa na tafsiri tofauti kabisa kwake, kwamba unampekesha.
Kumpelekesha wakati tayari ana majeraha ndani ya moyo wake, ni rahisi kwake kuzidi kuumia au kufanya maamuzi ambayo hutayapenda.

USIMSHIRIKISHE MTU
Hata kama ana matatizo kiasi gani, kumbuka kwamba wewe ndiyo chanzo cha yote, kuanza kuwashirikisha watu wengine matatizo yenu ni hatari hasa kama atajua umewaambia watu.
Kumbuka wewe ndiye mkosaji, lolote analolifanya ni kwasababu ya makosa ambayo umeyafanya wewe awali. Umenisoma?!

PANGA MTOKO
Njia zote hizo hapo juu kama hazitafanya kazi, basi utakuwa wakati wako wa kuzungumza naye, lakini si sehemu yoyote. Huu ni wakati wako wa kutafakari ni sehemu gani ambayo unaweza kwenda naye mkazungumza na kuelewana.
Panga mtoko, kisha mweleze. Mpe mwaliko lakini asijue ni kwanini unataka kutoka naye. Si vibaya kama akijua umetamani tu kutoka naye kwa nia ya kubadilisha mawazo na kusafisha macho.

ZUNGUMZA NAYE
Mkitoka, ni wakati wenu wa kuzungumza kwa makini na kumweleza ukweli kwamba
unajua ulimfanyia makosa makubwa na unatambua kabisa kwamba hana amani sana na wewe kwasababu yako.

Tambua makosa yako na umwombe msamaha wa dhati. Mwambie unataka muishi kwa amani katika ukurasa mpya wa mapenzi. Kwa njia zote hizo, atakuelewa na mtaanza maisha mapya. Hatakuwa na majeraha tena. Bila shaka hutarudia tena! Naweka nukta.
 
Nzuri sana!:A S-frusty2:

Back
Top Bottom