Jinsi ya kuthibitisha kama mtu/mpenzi wako anakupenda kwa dhati

Ray model

JF-Expert Member
Jul 27, 2018
207
184
Ukweli ni kwamba, Hakuna njia kuu ya kukuwezesha kuthibitisha moja kwa moja kama mtu anakupenda kwa dhati, lakini zipo ishara chache za kitabia zitakazoweza kukusaidia kutambua kilichopo katika mawazo ya mpendwa wako. Ukitaka kujua kama unapendwa na mtu unayempenda zitazame tabia zake juu yako. Ingawa upendo una mana tofauti kwa kila mmoja wetu, zipo njia nyingi zinazoweza kukueleza kama kweli mtu anakupenda kwa dhati, Tena zinazoweza kukupa tofauti ikiwa kama mtu anakupenda kwa dhati au amekutamani tu!
Zifuatazo ni mbinu za kuthibitisha kama mtu anakupenda kwa dhati;
MBINU YA KWANZA:
Angalia Anavyofanya.
Angalia kama anaweza kutenda mambo kikawaida unapokuwa naye.
Moja ya sehemu muhimu katika mapenzi ni kuwa muwazi kwa Yule umpendae. Kama unapokuwa naye umeanza kuona baadhi ya tabia au mambo fulani ambayo huwa hayaoneshi hadharani, ujue kapenda huyo! Kwa mfano, kama mpenzi wako huwa ni mpole na mtaratibu sana anapokuwa na umma, lakini mnapokuwa peke yenu anakuonesha mbwebwe na utani wake mwingi, mambo ambayo hawezi kuyafanya hadharani, ujue wazi anafunguka kwako na ni ishara kuwa anakupenda kwa dhati.
Kama mtu anakushirikisha hisia zake kikamilifu na anajisikia huru kufanya hivyo, huo ni upendo!!!
Kama mtu anajisikia huru kutokuwa mkamilifu mbele yako, mfano; hajisikii vibaya ikiwa utabahatika kukiona chakula kimemkwama katikati ya meno yake la mbele, au kukohoa (kubanja) mbele yako, yupo huru kukushirikisha pande zote za maisha yake kwasababu anakupenda kwa dhati.
Chunguza uone kama huwa ni mwenye furaha anapokuwa karibu yako.
Inapaswa kuwa hivyo hata katika siku yenye changamoto kwake. Kama mpenzi wako alikuwa na siku yenye changamoto au siku mbaya kama wengine waiitavyo lakini unamuone mudi yake inabadirika na kuwa yenye furaha mara tu anapokuona, basi hiyo ni ishara ya upendo kwako. Kama kweli anaugulia penzi lako, sura au sauti yako vinatosha kumpa faraja na kuivuta furaha maishani mwake – hata kidogo.
Siku nyingine mpenzi wako akiwa na siku mbaya, pima uone anavyoichukulia kampani yako licha ya kuwa na changamoto zake binafsi.
Je, Anakutupia jicho la shauku kubwa?
Ingawa inaweza kuonekana kama kwamba ni uchizi, lakini nakushauri siku nyingine ukikutana na mpenzi wako, utazame uso wake na kisha uone kama anakutazama kwa shauku kubwa. Utajua tu ukimtazama kwasababu huwa hali hiyo haionekani mara zote! Unaweza kupata mwanya huo wakati wa asubuhi au muda wowote hasa wakati wa chakula cha mchana mkiwa mezani.
Unaweza pia kumkamata akiwa anakukodolea macho kwa shauku kubwa vilevile.
Angalia kama huwa anachizika unapokuwa kando yake.
Mapenzi huwafanya watu wajisikie kuchizika, wepesi na wakati mwingine wajisikie kucheka bila sababu yoyote. Kama ukimuona mtu anafanya hivyo unapokuwa kando yake jua kakuzimia huyo!
Kama ikitokea umeongea jambo ambalo hata si lakuchekesha kivilee alafu unamuona mpenzi wako anafyatuka kwa kicheko kikubwa, jua atakuwa ana homa ya mapenzi juu yako huyo!!!
Kama ukimuona mpendwa wako anajisikia na nguvu na furaha ya ajabu kira mara unapokuwa kando yake, ujue hayo ni mapenzi tu yanamuwasha.
Angalia kama huwa anahuzunika pindi unapokuwa na huzuni.
Kama unaumwa au una uchungu mkubwa moyoni kutokana na changamoto mbalimbali za kimwili au kiroho, si ajabu kumuona mpenzi wako akihuzunika kwa sababu ya hali yako. Kama kweli anakupenda lazima uchungu wako umwingie moyoni mwake pia kwasababu hakuna anachopenda zaidi ya kukuona ukiwa katika furaha yako ya siku zote.
Ingawa sio lazima ahuzunike kwa kiasi kikubwa kama wewe lakini ni lazima aguswe katika namna moja au nyingine kwasababu kwa kadri ya upendo wake kwako daima hukutakia furaha tu na si vinginevyo.
MBINU YA PILI: Zingatia Maneno Yake.
Angalia kama huwa anayazungumzia maisha yenu ya baadae.
Kama mtu anakupenda, wazo la wewe kuwa ndani ya maisha yake huwa halimtatizi kabisa. Kama mara kwa mara huwa unamsikia mtu wako akizungumzia jinsi maisha yenu yatakavyokuwa baadae miaka miwili au kumi mkiwa pamoja. Kuna uwezekano mkubwa mtu huyo anakupenda kwa dhati na anataka uwe wake siku zote.
Kujitoa kweli kwaajili ya mapenzi, maana yake kuamua kuwa naye daima. Kama mtu anapenda kuzungumzia maisha yake ya baadae hali akikujumuisha na wewe ndani yake, hiyo ni ishara tosha ya kuwa mtu huyo anakupenda na anakuhitaji uwepo maishani mwake siku zote za maisha yake.
Pia kama mtu wako anapenda kuongelea kuhusu watoto wenu watakavyo kuwa, au mahali mtakapo fanyia “honey-moon” yenu na mambo mengine yanayoendana na hayo, ni ishara kuwa anakupenda na anakuhitaji maishani mwake.
Angalia kama anakupa sifa za msingi.
Kuna tofauti kubwa kati ya kauli hizi “Napenda Muundo wa Nywele Zako” na “Unao Uwezo wa Kunifanya Nijisikie Vyema Katika Hali Yoyote Ile” Kama mtu wako anakupa sifa zinazoonesha kuwa anavutiwa na tabia na utu wako, upo uwezekano mkubwa kuwa mtu huyo anakupenda kwakuwa uzuri wa nje huleta mvuto lakini tabia na utu wako utauteka moyo wa mtu.
Sio lazima mpenzi wako akumwagie sifa muda wote – Kumbuka kuwa ni Ubora wa kitu ndio unaozingatiwa hapa na si idadi ya vitu.
Kumbuka na zingatia usemi huu – “uzuri wa nje huleta mvuto lakini tabia na utu wako vitauteka moyo wa mtu”
Tambua kama mtu wako anakutamkia neno “Nakupenda” kwa Kumaanisha.
Kuna tofauti kubwa kati ya mtu anayekutamkia nakupenda kwa kumaanisha na Yule anayekutamkia neno hilo hilo kwa lengo la kupata kitu fulani kutoka kwako. Ukiona mtu wako anakutamkia neno “Nakupenda” hali akiyatazama macho yako kwa kujiamini. Ni ishara ya kumaamaanisha upendo juu yako.
Mtu anayekupenda atakutamkia neno “Nakupenda” mara nyingi bila sababu yoyote, na si kwasababu anahitaji chochote kutoka kwako au anajiskia kuwa ni neno zuri kumtamkia mpenzi wake bali ni kwasababu anatoa kile kilicho ijaa nafsi yake – upendo wake wa dhati kwako.
Pia mtu anayekupenda haoni haya kukutamkia “Nakupenda” mbele ya rafiki na ndugu zake kwakuwa haoni sababu ya kuuficha ukweli uliopo nafsini mwake.
Angalia kama ni muwazi kwako.
Kama mtu anakupenda kwa dhati, daima atajitahidi kuwa muwazi kufunguka kwako kuhusu hisia zake, mawazo yake, kile anachokipenda, mambo asiyoyapenda, historia yake na hata matatizo yake binafsi. Hiyo yote ni ishara kuwa anakupenda hivyo yuko huru kukueleza chochote kwasababu anatambua kuwa wewe ni sehemu yake na hivyo basi una haki ya kutambua mazuri na mabaya yake yote.
Ukiona mtu wako anakwambia “Sijawahi mwambia mtu yeyote kuhusu jambo hili….” Ni ishara tosha kuwa anakupenda na anakuamini kiasi cha kukushirikisha siri zake.
Katika uwazi wake, kumbuka pia kuwa mtu anayekupenda hatoacha kukukosoa kwa busara pale unapofanya jambo kinyume na utaratibu, anafanya hivyo kwasababu anakupenda japo anatambua kuwa wanadamu si wakamilifu lakini anajua wazi ya kuwa anapaswa kukujunga katika msingi ulio bora kwasababu wewe ni baba au mama wa watoto wake, hivyo asipokukosoa ndivyo utakavyolirudia kosa hilo hata kwa uzao wenu.
Tarajia kukumbukwa hasa unapokuwa mbali naye.
Kama mtu wako anakukumbuka kwa kukutumia ujumbe wa maneno kupitia simu yake, kukupigia simu, kukutumia barua pepe, kuchat na wewe mara kwa mara unapokuwa mbali naye hali akijaribu kukueleza jinsi alivyo kukumbuka, hiyo inamaanisha nini ? – Anakuonesha ni kwa jinsi gani hawezi kuyaendesha maisha yake bila ya wewe. Kama ukiona umekaa mbali na mtu wako kisha unaona ukimya tu! ndio unashamiri jua wazi hakuna mapenzi hapo.
Sio lazima akupigie simu mfurulizo akueleze kuwa amekumiss ndio ujue kuwa anakupenda. Kumbuka kuwa ana majukumu pia, hivyo kama na wewe unampenda zingatia uwiano wa mapenzi yenu na kazi.
Tarajia kukosolewa pindi unapokosea.
Kama kweli mtu wako anakupenda, ninaamini hawezi kuitunza picha yako ya kughushi kichwani mwake. Mtu anayekupenda kwa dhati daima atajijitahidi kukurekebisha na pia kukukosoa kwa busara pindi unapokosea. Hiyo ni ishara kuwa anakupenda jinsi ulivyo na pia anakubali mapungufu yako lakini anapenda uwe bora zaidi. Ingawa hatakiwi kukukosoa muda wote vilevile anayekupenda hawezi kukukosoa mbele ya watu kwakuwa anakuheshimu.
Kama mtu wako hajawahi kukukosoa au hata kukwaruzana na wewe kidogo, nakushari utafute mlango wa kutokea kwasababu hakuna mwanadamu anayeuweza wa kutenda kwa usahihi asilimia mia moja. Anayekupenda hatoyafuga makosa yako kwa kuitunza picha yako feki kichwanii mwake.
Angalia kama anaheshimu fikra zako.
Kama kweli mtu anakupenda daima ataziheshimu fikra zako. Haijarishi ni ushauri juu ya mavazi au matatizo yake binafsi daima atahehimu ushauri wako, atafanya hivyo kwasababu anakupenda na hivyo anataka utambue uthamani wako kwake.
Kumbuka kwamba sio lazima aombe ushauri katika kila kitu – atafanya hivyo hasa kwa yale mambo muhimu.
MBINU YA TATU: Tazama Matendo Yake.
Tarajia kusikilizwa.
Kama kweli mtu anakupenda kwa dhati, hawezi kuishia kuwa muwazi kwako bali atakusikiliza pia. Hata kama amewahi kuyasikia maneno hayo kabla lakini kama anakupenda atakutegea sikio tena na tena kwasababu anahesimu fikra zako. Ingawa hatokuwa kama mbwa wako lakini atajitahidi kwa kadri awezavyo kukutegea sikio.
Moja ya mambo muhimu unayopaswa kujifunza kabla na baada ya kuingi katika mapenzi ni usikivu, na si kuishi a kuongea tu! – Kama unavyopenda kusema na mwingine asikilize, vilevile uwe tayari kukaa kimya na kusikiliza maoni, maonyo na mafundisho ya mpenzi wako pia.
Angalia kama yupo kwaajili yako.
Hii inajumuisha nyakati nzuri na mbaya pia. Je, unapokuwa na huzuni na unahitaji faraja ya ukaribu au Unapokuwa mgonjwa, yupo tayari kutenga muda wake kwaajili yako? Na Vipi unapohitaji Kampani yake kutoka Out kupata chakula au kinywaji au unapohitaji kusikia sauti yake usiku wa manane, yupo tayari kuyaweka mambo mengine kando angalau hata kwa nusu saa kwaajili yako?
Kama mtu anajumuika na wewe nyakati unapokuwa na furaha tu na kisha kukutenga anapogundua una huzuni au unaumwa, huo sio upendo yupo hapo kutafuta kukidhi haja ya mwili wake na sio kutafuta penzi la milele.
Mapenzi maana yake kuwepo kwajili ya mwenzi wako, bila kujali chochote. Na upendo wa kweli maana yake ni kumkubali mtu katika mapungufu na mazuri yake bila kuchokan na kuwa naye katika nyakati nzuri na mbaya pia.
Angalia mambo mazuri anayokutendea.
Mtu anayekupenda kwa dhati atajitahidi kukutendea mambo mazuri kwa kadri awezavyo, kukufundisha mambo usiyoyajua, kukutembelea na kukuletea zawadi uwapo mzima au mgonjwa, kukupikia, kukufulia nguo au kukuoshea vyombo na mambo mengine mazuri ya siyo na kikomo, atafanya hayo yote kwasababu wewe ni furaha yake na hivyo hawezi kuiruhisu siku ipite pasipo kuiona furaha ikishamiri maishani mwako.
Mapenzi ya dhati hayaishii katika kile unachochukua kutoka kwa mtu bali kile unachoweza kukitoa pia kwaajili yake.
Mtu anayekupenda hatosubiri kuombwa ndio akutendee mambo mazuri .
Angalia kama anapenda kuwepo karibu yako.
Moja ya raha kubwa katika mapenzi ni ile hali ya kutaka kuwa karibu na Yule umpendaye nyakati zote. Mtu anayekupenda atajitahidi kuwa karibu yako kwa kadri awezavyo. Haina maana kuwa atakuganda kama luba, bali atajitahidi kuwa na wewe mara nyingi awezavyo na kwa kadri ya nafasi yake.
Je, anakupa uhuru?
Kama kweli mtu anakupenda kwa dhati atajitahidi kukupatia uhuru wa kufanya mambo yako mwenyewe bila hata kuambiwa au kuombwa. Kama watu wazima na mlio starabika mtatambua kuwa mnahitaji kupeana uhuru wa kufanya mambo yenu binafsi kutunza heshima yenu mbele ya jamii zinazowazunguka.
Kama unaona mtu wako anakuganda kuwa nawe muda wote ni darili ya kuwa hakuamini kama unaweza kusimama mwenyewe bila yeye kuwepo karibu yako, jambo ambalo haliashirii upendo kwasababu kuaminiana ni sehemu ya upendo wa kweli.
Angalia kama anakuelewa.
Upendo wa kweli ni maelewano thabiti. Kama mtu anakupenda kwa dhati anapaswa kukuelewa ili akupende zaidi, kutambua anachokitaka, unachokipenda na unachokichukia, mambo yanayokupa furaha, hata mabadiliko yako kihisia kwani kwa kufanya hivyo itampa wepesi wa kukupenda pasipo hali ya kudhani.
Simanishi kuwa mtu wako anapaswa kukuelewa asilimia 100%, najaribu kukupa mwangaza kuwa utambue kama anatambua hisia zako, unayoyapenda na unayayoyachukia? Na je, anaweza kukufurahisha?
Angalia kama anakutakia mema.
Hapa najumuisha hata yale mambo ambayo hayana faida kwake. Kama mtu anakupenda kwa dhati atakuwa mwelewa hata unapotakiwa kuwa mbali nay eye kwa kipindi cha muda Fulani ili uweze kufanikisha mamo yako, kwa mfano kama ni wewe ni mwanafunzi ataktakiwa kuelewa kwamba kuna kipindi utamuacha na kuelekea mikoa au hata nchi za nje kwaajili ya kukamilisha masomo yako, au kama wewe ni rubani, nahodha au dereva wa magari ya masafa malefu atatakiwa kutambua kuwa inakupasa ukae mbali naye kwa siku kadhaa ili utafute pesa badala ya kushinda tu mitaani.
Nina maana kwamba kama mtu anakupenda kwa dhati atajiongeza kwa fikra chanya juu ya majukumu yako kuwa yana faida kwenu wote na si kwako peke yako.
Angalia kama ni msaada kwako.
Kama kweli mtu anakupenda kwa dhati hatoishia kuwepo tu karibu yako bali atakusaidia katika shughuli zako ili ufanikishe ndoto zako na usonge mbele. Kama anakupenda atakusaidia kuandaa mpango wa biashara na mtaji pia ikiwa ana uwezo, atakusaidia kimasomo, atakusaidia kukuandaa na interview ya ajira, atakufundisha kupanga bajeti yako, atashiriki na wewe wajibu mbalimbali za kiroho na mambo mengine zaidi. Kwa ufupi ni kwamba atakuwepo kusikiliza jambo lolote linalokutatiza – kwaajili yako.
Kama anakupenda atakusaidia kufanikisha malengo yake hata kama katika namna moja au nyingine hayana faida kubwa kwake.
 
Upo likizo nini maana muda wa kuandika hii hotuba unaupata wapi kwa maisha haya ndg yangu
 
Angalia tabia na mienendo yake awapo kari au mbali naww.

Angalia kama anazungumzia maisha yenu, mipango ya familia ,watoto , na anakuonaje wee km sehem ya maisha yake?.. Kukukosa au kutokukosa nilipi jema kwake??

Angalia matendo yake linapokuja suala la mahusiano yenu .
Ulichokiandika ndio ufupisho au?
 
Umeandika vizur na mawazo yako yanaeleweka/umeyapangilia vizur na ni rahis kumfikia msomaji....watunzi wa fasihi tunasema umefaulu kimaudhui
 
Back
Top Bottom