Jinsi ya kutengeneza umeme kwa kutumia choo!

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Wadau kuna hii kitu nimekuwa nikisikia kwa miaka
mingi kuwa unaweza kuzalisha umeme kwa kutumia
choo (UMEME WA CHOONI),

Naomba mwenye maelezo ya jinsi unavyoweza
kutengeneza umeme huu anipatie kwani nafikiri kama
inawezekana basi ndio njia muafaka ya kumsahau Ngeleja
na Jairo.

Pia kama kuna njia nyingine nzuri ukiacha hiyo ya
chooni naomba tufahamishane.

Msaada wenu tafadhali!
 
Hii inabidi upate mtaalamu,huwezi kufanya mwenyewe. utahitaji kujenga matanki ardhini kwa mpangilio maalum. jaribu ku-google 'biogas', angalia pia 'carmatec', kama hawajapata kifafa hapo zamani walikuwa wanatoa hii huduma.

Ni uamuzi wa busara kujiunga nao, hapo unapata hata gesi ya kupikia. nadhani choo cha binadamu ndo kina gesi zaidi,angalia na hiyo option.
all the best.
 
Kuna haja ya kukusanya choo cha nchi nzima ili tupate umeme mwingi zaidi kwenye gridi ya taifa ambayo hadi leo haijafika mikoa kadhaa nchini
Bujibuji labda kuwe na utaratibu wa kila mkoa, wilaya au kijiji na si nchi nzima!
 
Nakumbuka mwaka 95, kuna mtu anaitwa Boke (Kwa sasa ni marehemu) alishawahi
kutengeneza hiyo kitu alitumia kwa siku tatu tu akaondoa kwa madai kuwa hairuhusiwi
na serikali!
 
Guys, these are just rumours, huo umeme una namna ya kupunguza gesi, kama ambavyo unatumia vent kwenye septic tank. Ni gesi salama na inaunganishwa kwenye jiko la gesi la kawaida kabisa, kulingana na idadi ya wanyama ulionao.

Nimeshuhudia watu wanatumia na wako very comfortable, hii kitu ilipata umaarufu sana Arusha (kwa sababu ya ufugaji na uwezo wa initial installation.)

Mtoa mada, usikate tamaa, watafute hao carmatec na upate maelezo ya kutosha. U freak me guys, kama wanaodai condom zimepandikizwa virusi vya HIV ili kuhalalisha kutembea peku.
 
Nakumbuka mwaka 95, kuna mtu anaitwa Boke (Kwa sasa ni marehemu) alishawahi
kutengeneza hiyo kitu alitumia kwa siku tatu tu akaondoa kwa madai kuwa hairuhusiwi
na serikali!
Mkuu unakusudia Marehemu Kelvin Chilumba? Yule alikuwa kichwa kaka sijui aliweka madudu
gani kule chooni. Halafu nasikia na wewe ulitengeneza wa kwako ulifanyaje? Maana nilimsikia
Yule X wa Arusha akikusifia!
 
Mkuu unakusudia Marehemu Kelvin Chilumba? Yule alikuwa kichwa kaka sijui aliweka madudu
gani kule chooni. Halafu nasikia na wewe ulitengeneza wa kwako ulifanyaje? Maana nilimsikia
Yule X wa Arusha akikusifia!
Ha ha haaa! Mkuu hayo mengine tutaongea kwenye simu. Niliyotengeneza mimi
haikuwa ya umeme wa chooni niliharibu UPS nikatengeneza kamashine kakuzalisha umeme
Nilibahatisha tu! Jioni nitakuendea hewani. Usiweke tena hadharani mambo ya X wa Arusha
Shem wako huwa anaingia JF Edit please asije kuona!
 
Umeme unaotokana na choo unatumia teknolojia ya biogas. hivyo kama uko serious nenda Arusha kwa watu wa CARMATEC wao wanashughulika na bio-gas itokanayo na vinyesi vya wanyama kama ng'ombe, mbuzi, binadamu, nguruwe n.k. Nasikia hata kwa mkuu wa kaya wamemfungia utaalamu huo kwa kutumia vinyesi vya ng'ombe anaowafuga
 
Mkuu, nimegoogle nimepata maelezo mazuri tu matumizi ya gesi-anuwai (si lazima itoke kwa kinyesi, inaweza kuwa miti, mabaki ya vyakula, maganda ya matunda, miti, nafaka n.k.
Angalia hapa: Biodigester Design & Construction: Building a Biodigester in Rural Costa Rica
Vile vile ukigoogle biogas kwenye wikipedia, kwenye zile endnotes, kuna mada za biogas kutoka Tanzania na Indonesia.
Pengine zitakusaidia kupata mawazo ya msingi.
 

Attachments

  • SNV - Domestic Biogas Brochure Tanzania.pdf
    111.7 KB · Views: 340
  • Indonesia Domestic Biogas Programme Brochure.pdf
    7 MB · Views: 559
Mkuu Kinyesi pamoja na waste products nyingine huwa zikioza huwa zinatoa methane gas..., ambayo inawaka.. (ndio maana hata uki - fart hio gesi inayotoka ukiweka moto inawaka..) hivyo basi ukiwa hata na ng'ombe wawili unaweza ukapata gesi ya kutosha kwa matumizi ya kupikia..., pia hata unaweza ukatengeneza mtambo mdogo kwa kutumia dumu la kawaida kuweza kuwashia jiko lako dogo la stove...

Umeme unaweza ukapatikana kwa kubadilisha mechanical energy kwenda kwenye electrical energy (hivyo basi unahitaji generator inayotumia methane gas au unaweza kutumia hio methane gas kuwasha moto kuchemsha maji (ili utengeneze steam engine)..

Kwahiyo utaona kwamba kwa kutumia hii Biogas na kuibadilisha kwenda kwenye electric energy sio efficient sana lakini hii Biogas ni very efficient kwa kuibadilisha kwenye heat energy moja kwa moja (yaani kupikia..) Kwahiyo mkuu unless utapata generator ambayo itatumia methane gas directly project yako haitakuwa efficient.. for more information angalia hapa chini wanajaribu kukuonyesha jinsi ya kutumia methane gas kutengeneza umeme

Electricity from a methane digester
 
Cheki hapa kuhusu Sweden Source Biogas: Producing Ultra-Efficient Fuel From Sewage >> MetaEfficient Reviews

In Sweden, 25% of all energy use is derived from biomass. In Linköping, Sweden's fifth biggest city, all the buses and garbage trucks run on biogas. The also have a biogas powered train line and some private taxis run on biogas.

biogas-powered-train-sweden.jpg


biogas-bus-sweden.jpg


kwahiyo mkuu ni kweli inawezekana kutumia hii biogas (methane) hatakuendeshea magari, train n.k. lakini cost ya kutumia hii gas kufanya hayo na performance yake sio nzuri sana...., ndio maana watu wanapenda kutumia Biofuel (methanol) kuliko Biogas kwenye kutengeneza mechanical energy, Biogas inabakia njia nzuri kuliko zote kwa kutumia kwenye matumizi ya kupikia na si vinginevyo (yaani kutengeneza moto)
 
Back
Top Bottom