Jinsi ya kutengeneza juice ya embe

Mahitaji
1. Maembe
2.sukari
3. Tangawizi
5. Iriki

HATUA

1. Chemsha maji ya kutosha mf lita 2 hadi 5 kulingana na wingi wa matunda

2.chukua matunda yako na uyaoshe vizuri kwa kutumia maji ya vuguvugu yaliyowekwa chumvi kiasi ili kuua vijidudu

3. Menya matunda yako taratiibuuu bila kujikata vidole

4.katakata matunda katika vipande vidogo vidogo ili kuiwezesha blender yako kusaga matunda kwa urahisi.

5.chukua matunda, iriki na tangawizi kisha weka ktk brenda na anza kusaga kwa kasi uipendayo. Unaweza kuongeza maji yaliyochemshwa wakati wa kusaga ili kupata mchanganyiko wa wastani usio mzito sana.

6. Chukua maji yaliyochemshwa changanya na rojo la matunda kwa kiasi kulingana na wingi wa matunda kisha koroga.

7. Chukua chujio safi na chuja mchanganyiko wako huo.

8. Chukua sukari na uitie katika mchanganyiko wako. Kisha koroga hadi sukari yote iyayuke.

9. Chukua chombo safi maalum kwa kuwekea juice na anza kuitia juice ktk vyombo hivyo mf. Chupa za plastiki

10. Weka juice yako katika friji. Unaweza kunywa juice yako na vitafunwa mbalimbali unavyopenda
 
Umeme wenyewe hakuna ndugu yangu wananchi wanajiuliza wafanyeje wakati dhamana imewapa Serikali ya CCM kwa zaidi ya miaka 60 ya Uhuru
 
Mleta mada kama unatengeneza Juisi ya watu 2-3 Huna haja ya kutumia sukari.

Hata kama ni familia ya watu 10 na uko uwezo unitumie sukari.

Badala yake tumia nanasi kubwa kwa wingi.

Ratio ya nanasi iwe kubwa kuliko embe.
 
Mara nyingi Juisi tamu ya embe (the simple one)huchanganywa;
1. Embe
2. Nanasi la kutosha
3. Passions za kutosha
4. Tangawizi kidogo sana (optional)

Sukari itatoka humo nzuri na tamu tu.

Juisi ya embe peke yake sio tamu sana kivileee ukilinganisha na hiyo ya hapo juu
 
Mfano;
Nunua nanasi la shilingi 2000/-
Embe la buku
Passions za shilingi 2,000/-

Maji 600 grams ile chupa ndogo ya drew drop water.

Jumla shilingi 5,000/- tu hapo ni gharama lakini ni faida kiafya.

Utapata kama lita 2 hivi.

Usiweke sukari hata tone,

Ni tamu hujapata kuona.

Sukari itatoka kwenye nanasi , pasheni na embe kwa mbali.
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom