Foxhound
JF-Expert Member
- Dec 15, 2013
- 28,038
- 74,429
Nilikuwa sipendi ile mtu kunikingia mkono, bora aniambie nimnunulieDuh!!!mkuu kweli we mchoyo.
Nilikuwa sipendi ile mtu kunikingia mkono, bora aniambie nimnunulieDuh!!!mkuu kweli we mchoyo.
zangu hizo! mwenzio akwambia nmeitia mate ili usimuombe still nataka ivoivo! dahHahahah aisee wewe mchoyo hadi kwapani.
Kuna wengine walikua wakinunua tu wanaitemea sasa wale makauzu wanasema wee nipe hivyo hivyo
Mara nyingi wnaokuomba ni marafiki/watu wa karibuSasa utanunulia wangap maana wanakua wengi kweli.
Ila mi nilikuwa bosi mtoto kipindi hicho, nilikuwa na kampani ya marafiki wengi lakini nilikuwa nawanunuliaKuna wengine hata sio rafiki basi tu njaa inasababisha
Hahaha aisee na maandaz au sambusa mtu anakwambia nimetoka chooni unamwambia wee nipe tu
Wengine hata sio njaa, tamaa tu.Kuna wengine hata sio rafiki basi tu njaa inasababisha
Hata mimi nilikuwa sizipendi kwakweli, yes za viazi zilikuwa tamu.Sambusa za wali nilikua sizipendi,za viazi tamu sana
mkuu umeongelea vyote viwili barafu na ice cream au maana nijuavyo maziwa hutumika kwenye ice cream au inakuwaje hiiMahitaji
(kwa mahitaji haya utatoa zaidi ya pisi 200 za barafu ukitumia vifuko vya size 1¼ X 10)
Maji lita 7
Maziwa ya unga 1 cup (brand yoyote)
Unga wa wanga (corn starch) 2 cups uchanganye na maji lita 1.5 (unga wa wanga unauzwa supermarket) au sokoni unga wa ubuyu
Sukari kilo 1¾ (waweza punguza)
Chumvi ½tsp (ukipenda)
Utaweka ladha uipendayo (vanilla, mango, chocolate, pineapple, nk) Mifuko 300 ya kufungia ice candy (mifuko ya barafu)
HATUA:
1. Weka maji lita 7 kwenye sufuria kubwa na weka jikon yachemke, ongeza sukari na chumvi(ukipenda), kisha changanya vizuri hadi viyeyukie humo .
2. Ongeza ile corn starch na maziwa ya unga kwenye hayo maji yanayochemka, koroga vzr ili kusitokee mabujabuja, chemsha kwa dk 8, kisha zima jiko, acha ipoe kwa saa kadhaa kisha ongeza ladha uipendayo.
3. Funga kwenye vile vifuko na gandisha hadi ziwe barafu.
mkuu umeongelea vyote viwili barafu na ice cream au maana nijuavyo maziwa hutumika kwenye ice cream au inakuwaje hii
thanks sana mkuu ni biashara ndogo ndogo za kujiongeza nina work mate watu anauza kwa siku zaidi ya 200 hiyo home kwake watanzania tuamke tusidharau biashara kuingiza elfu ishirini kwa siku ni kubwa tena ukiwa umetulia home kwakoNimeongelea barafu za kawaida.
Kuna maeneo ukienda ukaulizia barafu wanakupa yale mabonge ya barafu,ila ukiulizia ice cream wanakupa hizi za kula. Ukitaka za maziwa wanaita koni(corne)
thanks sana mkuu ni biashara ndogo ndogo za kujiongeza nina work mate watu anauza kwa siku zaidi ya 200 hiyo home kwake watanzania tuamke tusidharau biashara kuingiza elfu ishirini kwa siku ni kubwa tena ukiwa umetulia home kwako
Baada ya ice cream hizo kuna hii nyingine.
Kwenye friji kuna zile set za kugandishia vipande vya barafu, sasa kwa mchanganyiko kama huo unamimina kwenye zile set unaweka na vile vijiko kama vya kulia ice cream za azam then gandisha
AhsanteHizo tunaita barafu za mti