maelezo safiMkuu nimetulia ngoja nikupe ABC japo kidogo kwa uzoefu wangu,
Mahitaji:
Freezer kubwa kutegemea na uhitaji wako lakini pia pesa uliyo nayo.
Mifuko ya plastic ya kufungia barafu,ipo ya barafu za hamsini na barafu za mia au kutegemea uhitaji na soko lako.
Pia kuna juisi za unga ambazo zinauzwa kwa jagi lenye packet 72,kwa mwanZa ambako Mimi huchukulia mahitaji,jagi huuzwa sh 6000
Lakini pia kuna tangawizi ambayo Mimi huweka ili kutia/ kuongeza radha ya barafu lakini sio mhimu sana au kuna chupa furani ambazo huwa na kimiminika chenye kuongeza radha( flavours)
Kwa Mimi jagi moja lenye packet 72 linauwezo wa kuniingizia faida ya shilingi 40 elfu ila inaweza kuzidi hadi kufikia 70 elfu hii hutegemea ukubwa wa ice cream zako,Mimi hutengeneza kubwa ili kuvuta wateja,na barafu huwa na wateja wengi wakati wa kiangazi ambapo jua Kali huwalazimu watu kupata kitu cha baridi ili kupoza koo,kama una freezer kubwa jagi moja lenye packet 72 laweza isha within a day na kukuacha na faida ya almost 40 to 70 thousands,
Biashara hii inafaida kubwa sana lakini wengi huidharau na kuona kama ni kupoteza muda lakini pia hakuna cha kusumbuliwa na government juu ya maswala ya kodi licha ya faida kubwa iliyonayo
Kama kuna. sehemu hujaelewa mkuu uliza nikueleweshe
Sent using Jamii Forums mobile app
Sent using Jamii Forums mobile app